Meremeta 00:00:00. EXTRA

Meremeta 00:00:00. EXTRA

Status
Not open for further replies.
bado siamini mbona guests wamekuwa wengi hivi!!!!!
 
Nyamizi, ni PM kwani ripoti naona sold out....
Tolu

Mkuu Umemuuliza MJJ akasema hawezi kukupa nakala za akiba? Peleka $.30 mwambie afanye fanye naju hawezi kukosa akiba.
 
Mwanakijiji ndio Githongo (mkenya aliyeibua ufisadi Anglo Leasing) wetu!! I salute him.
 
Ina maana kweli tuishie kunusa tu? mie nimenunua vocha za Tsh 30,000/= ili nimtumie Max, kufungua computer nakutana na...... 00, sasa najiuliza ndio kweli na mie ntaishia kula kwa namna ya kipare? najiuliza nini maana haswa ya kuandaa nakala 100 tu wakati chakula chenyewe kinanukia uriuri mpaka mtaa wa saba? Nahisi kuna wanajamii hatutendewi haki

Mambo mazuri hayataki haraka. Subiri fungulia mbwa!. Umeshawahi hudhuria viwanjani wakati huna kiingilio, inabidi usubiri dk za majeruhi ukaangalie jezi za wachezaji zina rangi gani. Sasa MMK ameshaweka Jezi zote basi subiri recorded utaangalia utakuwa tayari unajua matokeo ya mchezo
 
Huu ni wizi mtupu hakuna lolote hapa kama mna nia njema na umma wa watanzania toeni bure hiyo ripot hapa kwa forum mnapoomba fedha hivyo mnajionesha kuwa mu wafisadi kama wao tu no difference najua mtachukia mnataka sifa msizostahili.

Phd umenena nimesikitika sana kwamba ripoti hiyo haina jambo jipya zaidi ya kunukuu taarifa mbalimbali kama zilivyowahi kuripotiwa na vyombo vya habari, vyama vya upinzani na mashirika ya wanaharakati. siyo kwamba napuuza ripoti hii lakini haikustahiriki kuuzwa kwa madai kuwa ni ya uchunguzi kwa kina. MZEE MWANAKIJIJI ni kama umejishushia hadhi kwa kuamua kuuza ripoti hii. Wengi tulisubiri kuona kitu kipya. I beg to differ.
 
Phd umenena nimesikitika sana kwamba ripoti hiyo haina jambo jipya zaidi ya kunukuu taarifa mbalimbali kama zilivyowahi kuripotiwa na vyombo vya habari, vyama vya upinzani na mashirika ya wanaharakati. siyo kwamba napuuza ripoti hii lakini haikustahiri kuuzwa kwa madai kuwa ni ya uchunguzi wa kina. MZEE MWANAKIJIJI ni kama umejishushia hadhi kwa kuamua kuuza ripoti hii. Wengi tulisubiri kuona kitu kipya. I beg to differ.
 
Hayo ni maoni yako na una uhuru wa kuamua utakavyo!!!!! Mimi naona it was a wise decision kufuata utaratibu huo walioufanya akina mwanakijiji na consortium
 
Huu ni wizi mtupu hakuna lolote hapa kama mna nia njema na umma wa watanzania toeni bure hiyo ripot hapa kwa forum mnapoomba fedha hivyo mnajionesha kuwa mu wafisadi kama wao tu no difference najua mtachukia mnataka sifa msizostahili.
Kutaka vya bure kila siku ni ufisadi mkubwa zaidi, zaidi ya ule wa kulipia kila huduma unayopata.
 
Phd umenena nimesikitika sana kwamba ripoti hiyo haina jambo jipya zaidi ya kunukuu taarifa mbalimbali kama zilivyowahi kuripotiwa na vyombo vya habari, vyama vya upinzani na mashirika ya wanaharakati. siyo kwamba napuuza ripoti hii lakini haikustahiriki kuuzwa kwa madai kuwa ni ya uchunguzi kwa kina. MZEE MWANAKIJIJI ni kama umejishushia hadhi kwa kuamua kuuza ripoti hii. Wengi tulisubiri kuona kitu kipya. I beg to differ.

Hamkosekanagi!!
 
Yawezekana ndio tuliosikia wanaitwa uwt sasa wameanza kazi🙂

Phd na Shapu mko sahihi kusema yaliyo moyoni mwenu lakini yote hayo nilikuwa nayategemea. sijawahi kumkosoa kijana wetu mzalendo wa kweli MZEE MWANAKIJIJI lakini najua kuwa ukithubutu kukosoa kazi zake ni vyema ukajiandaa na rungu zito toka kwa washiriki ambao kila jambo aliloaandika na kunena mwanakijiji haitakiwi kwenda kinyume. Angalia sasa ukienda kinyume unaitwa UWT wapi na wapi? je tutafika?

MZEE MWANAKIJIJI heshima mbele, lakini ninathubutu kusema kwa jinsi ulivyoitangaza kazi yako hii na watu wamekuunga mkono kwa kulipia 30,000. Hata hivyo kumbuka hii ndiyo kazi itakayokujenga au kukubomoa kwa kipimo cha kwamba ni kazi nzuri ambayo haina maudhui mapya ilitakiwa isambazwe bure.

Naomba wanaojibu haya ni muhimu wawe wamepitia na kusoma ripoti hiyo na kutueleza ni kitu gani kipya tangu kashifa ya Meremeta ilipoibuka. Ninachoweza kumshukuru Mwanakijiji ni kukusanya taarifa mbalimbali na kuweka katika makala moja. Pole kwa kazi nzito na ndefu.
 
Yawezekana uko sahihi. inawezekana ripoti haina chochote. lakini hata kuikusanya kuiweka pamoja ni kazi ngumu sana, na hata wewe unakubali kuwa ni nzito. je asifidie kidogo baadhi ya gharama walizotumie?
kwako wewe waona haina jipya mie kwangu ni kitu kikubwa sana.
Huo ni mtizamo wangu.
 
MZEE MWANAKIJIJI heshima mbele, lakini ninathubutu kusema kwa jinsi ulivyoitangaza kazi yako hii na watu wamekuunga mkono kwa kulipia 30,000. Hata hivyo kumbuka hii ndiyo kazi itakayokujenga au kukubomoa kwa kipimo cha kwamba ni kazi nzuri ambayo haina maudhui mapya ilitakiwa isambazwe bure.

Mwanajamii,

Kazi hii licha ya kukusanya makala nyingi sana kuhusu sakata la Meremeta na kulikweka katika taarifa moja comprehensive, imejaa masuala mapya mengi sana. To appreciate kazi hii soma kitabu kinaitwa The Arms Deal (mtunzi nimemsahau jina, ni cha Afrika Kusini kuhusu Zuma etc). Kuna mambo mapya na yameunganishwa na mtandao hatari sana duniani. Kuna masuala mapya mengi sana.

Nimemwambia MwanaKijiji kuna taarifa moja muhimu sana aipate na kuichambua na ku-update Taarifa hii. Hapo atakuwa amemaliza kazi.
 
Huu ni wizi mtupu hakuna lolote hapa kama mna nia njema na umma wa watanzania toeni bure hiyo ripot hapa kwa forum mnapoomba fedha hivyo mnajionesha kuwa mu wafisadi kama wao tu no difference najua mtachukia mnataka sifa msizostahili.

pole sana ndiyo ukubwa wenyewe huo.
 
Phd umenena nimesikitika sana kwamba ripoti hiyo haina jambo jipya zaidi ya kunukuu taarifa mbalimbali kama zilivyowahi kuripotiwa na vyombo vya habari, vyama vya upinzani na mashirika ya wanaharakati. siyo kwamba napuuza ripoti hii lakini haikustahiriki kuuzwa kwa madai kuwa ni ya uchunguzi kwa kina. MZEE MWANAKIJIJI ni kama umejishushia hadhi kwa kuamua kuuza ripoti hii. Wengi tulisubiri kuona kitu kipya. I beg to differ.

sasa kwanini na wewe usinukuu hizo taarifa mbalimbali na kuziweka kwenye pdf file na kuzituma bure!?
 
Phd umenena nimesikitika sana kwamba ripoti hiyo haina jambo jipya zaidi ya kunukuu taarifa mbalimbali kama zilivyowahi kuripotiwa na vyombo vya habari, vyama vya upinzani na mashirika ya wanaharakati. siyo kwamba napuuza ripoti hii lakini haikustahiri kuuzwa kwa madai kuwa ni ya uchunguzi wa kina. MZEE MWANAKIJIJI ni kama umejishushia hadhi kwa kuamua kuuza ripoti hii. Wengi tulisubiri kuona kitu kipya. I beg to differ.

Sina Uhakika sana kama ni wa kujibiwa, maana wapo ambao hata kama utawajibu unakuwa unatwanga maji kwenye kinu kwani wameshaamua wawe upande gani.

Inawezekana kwa mtazamo wako uko sahihi (hatuwezi jua labda upo kwenye position uliyoweza kuaccess hizi information kabla au hata kufaidi mgao wa Hiyo biashara kwi kwi!). Lakini wengi unatakiwa kutupa nafasi na sisi ya kupima alichotuletea MMM.

Hata kama ni taarifa ambazo wengi walishazisema zimewahi kuwa published kuwa kwenye Document moja? Maana ya report ni nini? Ni kukusanya pamoja ushahidi na kuuweka kwenye mpangilio. Kwa mfano report ya Bw. Utoh (CAG) juu ya kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo aliyokabidhi jana kwa PM Unadhani itakuwa na jipya?

Itakuwa inajibu hypothesis zetu tulizo nazo, Itakuwa inajaribu kusema hili ni kweli hili si kweli, na itakuwa na mapendekezo. Vivyo hivyo hata report ya Mwanakijiji juu ya Meremeta ni report inayotaka kusema juu ya Hypothesis tulizokuwa nazo. Kuwa na Hypothesis haimaanish umeshakuwa na results, report yako baada ya uchunguzi inaweza ikasema tofauti na hypothesis.

Pia jambo lingine la Msingi ni kuwa kama hakuna kitu, watu hawapati mahali pa kuanzia kujadili Hoja. Si unaona waraka wa Wakatoliki umetukumbusha mambo mengi, umetukumbusha ugawaji wa rasilimali zetu, katiba, madaraka ya Rais na mambo mengine mengi. hata hii Report inategemewa kutoa kianzio cha waTanzania kujadili mstakabali wa nchi yao. Itatuapa nafasi ya kujua wapi tuliteleza, na tukisha kujua tutajua tufanye nini ili tusimame tena.

Sinema ya Darwin Night mare, ilikuwa haina jambo lolote jipya, ilionyesha watu wanakula mapanki (ni kweli) ilionyesha malaya wanajiuza (ni kweli). Unaweza ukaniambia kwanini mh. Rais JK alichachamaa mpaka kufoka sana huko mwanza? Nini Kilimkasirisha kwenye ile documenatary? Kwanini watu walilazimishwa kuandamana? na baadaye kukawa na mjadala mkubwa sio Bongo tu na sehemu zingine Duniani.

Kwa hiyo Vitu kama Darwin night mare huwa hazina kitu kipya lakini zinawafanya watu wafikirie zaidi mbali zaidi ya urefu wa pua yao. Baada ya ile Documentary imewafanya watu kama akina Mwanakijiji na sisi wengine tujiulize kuwa kuna nini nyuma ya hii pazia la samaki na mapanki? kwanini JK amechachawa hivi, hata Ulaya na sehemu zingine duniani kote wanauza K. Sasa amekasirika nini?

Unaona ile katuni ya kipanya akijiuliza kuwa kwanini viwanda vya samaki vipo Mwanza tu na wakati Tanga mpaka Mtwara kuna bahari na hakuna Viwanda? kwanini Kigoma lake Tanganyika hakuna Viwanda? watu makini Tukiona katuni kama ile huwa tunaenda maktaba kujaribu kutafuta majibu, na huko hatutegemei kusema tunayoamini kutoka moyoni mwetu bali kuoona tafiti za wenzetu zinasemaje, kwa hiyo ndizo tunazitumia kutengeneza jibu kwa kuzi-review. (Katika Ulimwengu wa sayansi inakubalika) na baadye kufananisha na majibu ya wakati huu.

Kwa hiyo watu kama Mwanakijiji wamechukua hatua kubwa sana ambayo wasomi wengi Tanzania wameshindwa kufanya, Mashirika mengi yameshindwa kufanya. Tunashindwa kufanya kwasababu tunahesabu gharama kwanza au tunaogopa (sio vibaya)

Kama UWT wangeifanya hii kazi tungewapongeza lakini ikifanywa na raia wenzetu wasio tumia kodi zetu tunapaswa kufanya zaidi ya kuwapongeza, Mwanajamii tunapaswa kuwaunga mkono, Tuwaunge mkono tuwapunguzie gharama za kukusanya hizi data na kuziweka in a presentable form, tuwaunge mkono kwa kuanza kujadili na kusema wazi, tuwaunge mkono kwa kuwaambia wengine wasio jua kweli waijue, na kusimama na kusema sasa inatosha, Enafu iz Enafu! INATOSHA.

Tumedanganywa kiasi cha kutosha, tumedharauliwa kiasi cha kutosha, sasa ni wakati wetu wa kuwa na taifa la watu walio sawa na Huru, ni wakati wa kila aitwaye Mtanzania kupata nafasi ya kujadili mstakabali wa nchi yake, ni wakati wa kila mbongo kupata nafasi kuvuna kilichopandwa shambani mwetu, kwenye shamba letu la familia ya watanzania. Tusikatishane tamaa, kama huwezi kuwa upande wetu lakini unaamini kuwa hupo upande wao, basi tulia, tuache tuvipige vita, tukishinda tutakualika kwenye karamu ya kufaidi matunda ya nchi.

Ijueni Kweli nayo Kweli Itawaweka Huru.
 
PhD said:
Huu ni wizi mtupu hakuna lolote hapa kama mna nia njema na umma wa watanzania toeni bure hiyo ripot hapa kwa forum mnapoomba fedha hivyo mnajionesha kuwa mu wafisadi kama wao tu no difference najua mtachukia mnataka sifa msizostahili.

Kuzoea vitu vya bure ni hatari sana!

Ni kweli kabisa, PhD usipende vya bure. Toa pesa upate hiyo report.
 
MZEE MWANAKIJIJI heshima mbele, lakini ninathubutu kusema kwa jinsi ulivyoitangaza kazi yako hii na watu wamekuunga mkono kwa kulipia 30,000 lakini kumbuka hii kazi ndiyo itakujenga au kukubomoa kwa kipimo cha kwamba ni kazi nzuri ambayo haina maudhui mapya na ambayo ilitakiwa isambazwe bure kwetu.

Ilitakiwa na nani isambazwe bure?

Naomba wanaojibu haya ni muhimu wawe wamepitia na kusoma ripoti hiyo na kutueleza ni kitu gani kipya tangu kashifa ya Meremeta ilipoibuka. Ninachoweza kumshukuru Mwanakijiji ni kukusanya taarifa mbalimbali na kuweka katika makala moja. Pole kwa kazi nzito na ndefu.

una uhakika na unachokisema? mnaruhusiwa kujadili contents zake; siyo siri.
 
Mwanajamii,

Kazi hii licha ya kukusanya makala nyingi sana kuhusu sakata la Meremeta na kulikweka katika taarifa moja comprehensive, imejaa masuala mapya mengi sana. To appreciate kazi hii soma kitabu kinaitwa The Arms Deal (mtunzi nimemsahau jina, ni cha Afrika Kusini kuhusu Zuma etc). Kuna mambo mapya na yameunganishwa na mtandao hatari sana duniani. Kuna masuala mapya mengi sana.

Hapa anazungumza mtu aliyeisoma siyo anayehisi kuwa kaisoma!

Nimemwambia MwanaKijiji kuna taarifa moja muhimu sana aipate na kuichambua na ku-update Taarifa hii. Hapo atakuwa amemaliza kazi.

aisee I'm working on that; na I'm glad I missed it the first time kwani tukiipata tu ile basi ni kama kuweka kachumbali pembeni ya pilau!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom