sijui wangapi ambao wameisoma hii ripoti bado wataipigia kura CCM!
Kwanza Mzee mkjj ninashukuru kwa kuwa na moyo wa kizalendo na wenye nia ya kweli na kuleta mabadiliko.
Nadhani soluhisho muhimu ni kuondokana na na dhana a uchama uchama. tuchague watu.pia bungeni ile ajenga ya wagombea binafis ilurudishwe. naamini kuna wtu wengi safi hawataki kujihusisha na vyama kama wapiga kura wengi pia hatuna vyama.
Lakini pia tukisema tuchague watu na si chama linakuja tatizo lingine Viongozi waadilifu, wazalendo wa kweli kwenye pande zote mbili za shilingi( UTAWALA na UPINZANI) ni wachache. ndio maana suala la mgombea binafsi liluridhswe kurudisha imani kwa wapiga kura.
Mtazamo wangu ni kuwa tuanahitaji Rais awe wa CCM na wabunge wengi zaidi watoke upinzani au wawe binafsi
Wananchi wanachagua au tunachagua CCM si kwasababu ni chaguo letu bali ni ile kauli ya zimwi likujualo. Wapinzani wanahitaji kufanya kazi zaidi ya wanayofanya sasa. TRUST kwa wananchi ni ndogo.
Mimi nadhani vita nzuri sio kuhangaika kuwang'oa CCM madarakani. itatuchukua muda sana kwa hali halisi. Vita nzuri ni kufunua uozo kama huu. Kuanika utendaji kazi mbovu za taasisi kama tume za maadili, Jeshi, EPA, Richmond. meremeta nk.
CCM Wao wenyewe huko jikoni kwao watanyoosheana vidole, kuchambuana na baadae kutengana.Kwa syle hii CMM original aliyoitaka mwalimu nyerere itarudi na labda tunaweza kuanza kujikongoja tena baada ya kuchechema kwa zaidi ya miaka 40 sijui ni ya uhuru au ufungwa?