Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 855
Uchunguzi mpya wa ThisDay au Vipi ni ripoti ya MEREMETA inatolewa kwa mafungu?
hii ndio THIS DAY journalism...nikisema niliambiwa nina chuki binafsi na MENGI lakini hawa ndio ma journalists na media ambao uongozi wa JAMII FORUMS unaona aibu kuwa out kisa sikijui lakini kuna theories kuwa ni bedfellows wa JF!
Nothing new walichokifanya wamechukua ripoti ya Mwanakijiji from Jamii Forums na kujidai eti wamefanya "FINDINGS"...findings my arse!
Sasa mnaogopa nini kuwaaanika hawa? Zipo namna nyingi tu za kuwaweka in their rightful places lakini hilo hamtaki!
Katika ripoti ya MwanaKijiji kuna barua ya IKULU? kama hii?
Mmoja wa wasomaji alisema hivi, "Nimeisoma ripoti ina mapungufu kadhaa ikiwa ni pamoja na kutohusisha kuwapo kwa barua ya Ikulu. Raia Mwema walikwisha andika kuhusu hiyo barua."
Nadhani Raia Mwema walikwisha andika, hilo nadhani ndilo ungetumia kama kigezo cha kuwasema Thisday lakini si vinginevyo.
http://www.raiamwema.co.tz/index.php?d=24
Lakini RAIA MWEMA wao si walishasema kuwa wameipata JF ama?
Sasa hawa THIS DAY waomeona ubaya gani kusema kama source yao ni JF?
Hapa tunapa wider picture kuwa inawezekana wahariri wenyewe inawezekana walipokuwa chuo kikuu walikuwa wana palagarize course works zao na haya ndio matokeo yake wakiwa kazini wanaumbuka
Kumbukeni kuna ambao iliuzwa na haikuwa na masharti yoyote yale na ile ambayo iliwekwa hapa tatizo ndio hilo
Mkuu GT umekwenda haraka kabla ya kusoma hilo Raia Mwema, si la mwaka huu lililosema http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=1577 ni la muda mrefu ambalo lilisema http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=619
Na ndio maana hata This Day walipoandika kwa jamii yetu inaonekana mpya.
Kumbukeni kuna ambao iliuzwa na haikuwa na masharti yoyote yale na ile ambayo iliwekwa hapa tatizo ndio hilo
Unapofanya kazi yoyote ile huwa tunacknowledge watu wengine waliofanya hiyo kazi. Siamini kuwa This day hawakuioona report ya MJJ, kwa hiyo walipokuwa wanaandika kazi yao ilibidi waseme kuwa katika habari walizozifanyia uchunguzi zinazoshabihiana na kazi za MJJ alafu wanataja hayo mambo muhimu.
Tatizo sio Journalism, tatizo ni shule zetu TZ, unajua shule zetu hazina Essay na tukiwa tunaandika Essay hawatuaambii habari ya kuacknowledge, suala la Paragilism halitiliwi mkazo kabisa, ndio maana unaweza ukachukua kazi ya mwingie ukabadirisha kava na kuiuza upya bongo kweli tambarare
Halisi, nadhani watu wanajaribu kutofauti mgongano ambao haupo. Kuna taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa kwa muda mrefu kuhusu Meremeta; taarifa ambazo tumeweza kuzionesha kuwa zinagongana na kutokana na kugonangana huko zinazua maswali zaidi kuliko majibu.
Lakini wakati huo huo kutoka na ile ripoti maalum tumeenda zaidi ya "official government position and correspondences". Watu wajaribu kufuatilia Iran Contra na Arms to Africa Affair na jinsi gani official gvt positions zilikuwa. Sasa hivi unaweza kuona kuhusu Meremeta serikali imekuwa na positions tatu kubwa ambazo zimekuwa zikibadilika kwa kadiri ya muda unavyokwenda:
a. Ilikuwa kwa ajili ya kusaidia wachimbaji wadogo
b. Ilikuwa kwa ajili ya uzalishaji wa dhahabu mkubwa kusaidia uchumi wa nchi (thus the quoted letter)
c. Ilikuwa kwa ajili ya kupata fedha za kufadhili kiwanda cha magari cha jeshi (Nyumbu).
d. Wapinzani wana sababu yao ya nne ambayo ni fedha zilichukuliwa kuingia kwenye uchaguzi mkuu 2005
Bahati mbaya ripoti yetu imeenda nje ya hizo sababu nne na kuongeza sababu ya tano na labda ya sita vile vile. Hiyo sababu ya tano ndiyo Enigma ya hili lote.
Usemayo uko sahihi kabisa, lakini kwa bahati mbaya sana ni kwamba hujui undani wa hiyo story ya Thisday na pengine hujui kabisa undani wa Ripoti Maalumu, sasa unapotaka Thisday waseme walipata JF ama kwa Mwanakijiji unakwepa ukweli ambao umeelezwa hapo juu. !!
Ahsante sana nakushukuru mno kwa kuniongozaNenda kwenye post ya kwanza kabisa, mwanzoni mwa hii thread au mwanzoni mwa kila ukurasa mpya utaona files mbili za pdf. Chukua chako mapema ufaidi jasho la Mwanakijiji. MIMI nimefaidika sana na inshallah siku tukikutana kijijini tutatesa na kopo moja la kangaa!
Mkuu angalia hiyo content za barua na hiyo story waliyoandika kama hiyo barua imetaja yote waliyoandika humo, je barua inataja 50:50 ya share, inawataja wakurugenzi? kuna mambo kibao ukiyasoma kwenye story ya This Day na hiyo source yao ya barua haitoshelezi kuwa habari yote imetoka kwenye barua na kama wanavielelezo vingine vilivyowapa hizo habari mbona hawajasema?