Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Udhibiti wa bangi katika kata za Uwiro na Oldonyowas halmashauri ya Meru mkoani Arusha, unawaweka hatarini watendaji wa kata hizo, wakidai kukabiliwa na vitisho kutoka kwa baadhi ya wananchi.
Watendaji hao wameeleza changamoto hiyo jijini Arusha, wakiwa kwenye mafunzo ya Uraia na Utawala Bora kutoka wizara ya Katiba na Sheria, yakihusisha watendaji kata na wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri za Jiji Arusha, Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na Halmashauri ya wilaya ya Meru.
Mtendaji wa kata ya Uwiro, Minah Yonazi, amesema “Mpaka watu wameshatumwa nyumbani kwamba huyu mtendaji spidi yake ni kubwa, apunguze ataumia..” ameeleza juu ya vitisho anavyovipata.
Ameongeza kuwa “Mtakamata mtu mtamuweka ndani baadaye akarudi tayari ni maadui wa moja kwa moja, ambapo hata kama utaenda sokoni na watu tunaishi nao bado itakuwa ni changamoto kiusalama kwamba huyu mtendaji utakuwa kwenye hali gani.”
Naye Mtendaji wa kata ya Oldonyowas, Maliaki Lukumay, amesema katika oparesheni za kukamata bangi wanakuwa hatarini kujeruhiwa au kudhuriwa kutoka kwa watuhumiwa kutokana na kutokuwa na silaha, huku watuhumiwa wakiwa na silaha.