Messi awarejeshea matumaini Argentina, aisambaratisha Colombia

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Mchezaji bora wa soka duniani, Lionel Messi amewaongoza Argenina kuwasambaratisha Colombia kwa mabao 3-0 katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 kwa nchi za Amerika ya Kusini. Katika mechi hiyo kati ya Argentina na Colombia iliyochezwa alfajiri ya leo, Messi alifunga bao moja kwa mpira wa adhabu na kutengeneza mabao mengine mawili yaliyofungwa na Pratto na Di Maria.

Hiyo ilikuwa ni mechi ya 12 kwa Argentina na sasa wamebakiwa na mechi 6 kukamilisha mechi za kufuzu. Argentina sasa imepanda hadi nafasi ya tano kati ya timu kumi zilizopo katika michuano hiyo ya kufuzu. Akicheza kama Nahodha na katika kiwango cha juu, Messi aliibeba vya kutosha Argentina na kuwarejeshea matumaini ya kufuzu Waargentina wote.

 
Kuna mchezaji duniani kama messi? Binafsi sijaona na hatatokea, labda baada ya 300 yrs......jana nimecheki game aise huyu mtu Mwenyezi Mungu kampa kipaji kwa kweli, kila mechi anatuletea kitu kipya...yani jana alikuwa anakokota mabeki kama kapuliza vile😀 na ndio kawaida yake wala sio kitu cha ajabu kufanya vile....
 
Huzungumzii Brazil ambayo tangu ipate kocha mpya hii ni mechi ua 6 haijapoteza na juzi kati imewapiga hao Wakina Mesi 3 bila
 
Mbona juzi akicheza na Brazil hajawakokota beki w Brazili? Hahaaa
 
Kila shetani na mbuyu wake.. Bado sijaona mchezaji bora wa kumzidi cr7..
 
Mbona juzi akicheza na Brazil hajawakokota beki w Brazili? Hahaaa

Mkuu MURUSI! umesahau Brazil walichapwa 4 na messi akapiga hat trick! au ndo juzi umeangalia mechi moja tu 😀😀
 
Reactions: PNC
Huzungumzii Brazil ambayo tangu ipate kocha mpya hii ni mechi ua 6 haijapoteza na juzi kati imewapiga hao Wakina Mesi 3 bila
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] hao tushawazoea ni mbio za sakafuni hizo
YUKO WAPI DUNGA NA JINS ALIVYOANZA
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] hao tushawazoea ni mbio za sakafuni hizo
YUKO WAPI DUNGA NA JINS ALIVYOANZA
Unaelewa unachoandika?unajua nani anaongoza?unajua ni mashindano gani......hao jamaa sakafu yao kombe la dunia Russia 2018.....kuna dogo anaitwa G.Jesus...ingia you tube uone walivyo.
 
Unaelewa unachoandika?unajua nani anaongoza?unajua ni mashindano gani......hao jamaa sakafu yao kombe la dunia Russia 2018.....kuna dogo anaitwa G.Jesus...ingia you tube uone walivyo.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] sasa kama hujui nilichoandika y? hujaniuliza nilipokuchanganya inaonekana ww ni mfuatiliaji wa Brazil mwaka huu
hao ndivyo walivyo subir Russia 2018 hawatafika hata nusu

KINGINE ALIYEKWAMBIA YOUTUBE KUNA MCHEZAJI MBAYA NI NANI
INGIA YOUTUBE MUANGALIE GIROUD HALAFU MFATILIE LIVE[emoji1] [emoji1] utachoka kabisa
 
Unaelewa unachoandika?unajua nani anaongoza?unajua ni mashindano gani......hao jamaa sakafu yao kombe la dunia Russia 2018.....kuna dogo anaitwa G.Jesus...ingia you tube uone walivyo.


Mkuu made taratibu! Mechi ya juzi tu ila za nyuma hukumbuki tulivyowafanya! Unakumbuka lile game wamekutanishwa new jersey marekani 2012?tukawapiga 4 messi akapiga hattrick umesahau? Kule Qatar nako umesahau tulivyowafanya? messi kama kawa akawaburuza mabeki marcelo alishindwa afanye nini huku mpira unampita anabaki kutoa mimacho tu huku messi anachomeka goli la mbali baada ya kuwapita mabeki,na hilo pia umesahau? 2005 fifa world cup south American kipindi cha akina requelme,crespo na tevez tuliwafanya nini?yapo mengi ya kuyaelezea lkn ntaishia tu hapo kamanda! Mi nadhani Argentina bado hatujapata tu kocha wa kuiweka sawa tim,kama ni mafundi wa mpira tunao wengi sana kuzidi tim yeyote ile duniani na wengine wanakosa hata nafasi ya kucheza... ila i hope tutafanya wonders 2018....tuombe uzima tu
 
Mguu wa kushoto wa Messi una akili nyingi kuzidi vichwa na miguu yote ya angalau nusu ya wazechaji wa Mourinho wa sasa.

Yeah ni kweli..messi kila mechi anavumbua vitu vipya ambavyo havijawahi kutokea kwa mchezaji yeyote yule....u know that raha ya messi anahitaji timu ishinde hayupo kwenye nafasi ya kufunga atatoa pasi wafunge wengine.
 
Kwani unazungumzia kipi maana sijaelewa ndg.....!km ni performance kwa sasa Brazil ndo yupo top ya table kwa tofauti ya point NNE..na zimesalia mechi sita tu....bina Shaka safari yao ya kuwa ni miongoni mwa mataifa ambayo hayajawahi kukosa ktk world cup bado ipo palepale......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…