Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Mchezaji bora wa soka duniani, Lionel Messi amewaongoza Argenina kuwasambaratisha Colombia kwa mabao 3-0 katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 kwa nchi za Amerika ya Kusini. Katika mechi hiyo kati ya Argentina na Colombia iliyochezwa alfajiri ya leo, Messi alifunga bao moja kwa mpira wa adhabu na kutengeneza mabao mengine mawili yaliyofungwa na Pratto na Di Maria.
Hiyo ilikuwa ni mechi ya 12 kwa Argentina na sasa wamebakiwa na mechi 6 kukamilisha mechi za kufuzu. Argentina sasa imepanda hadi nafasi ya tano kati ya timu kumi zilizopo katika michuano hiyo ya kufuzu. Akicheza kama Nahodha na katika kiwango cha juu, Messi aliibeba vya kutosha Argentina na kuwarejeshea matumaini ya kufuzu Waargentina wote.