Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,046
- 3,971
Nahodha Lionel Messi ana kazi ngumu kuivusha Argentina katika fainali hizo katika mchezo wa mwisho dhidi ya Ecuador itakapokuwa ugenini mjini Quito.
Endapo Argentina itashindwa kukata tiketi, itakuwa ya kwanza kutokushiriki fainali hizo tangu mwaka 1970.
Brazil tayari imekata tiketi na katika kundi lake inafuatiwa na Uruguay (pointi 28), Chile (26), Colombia (26), Peru (25), Argentina (25) na Paraguay (24).
Argentina wanashikilia nafasi ya sita katika msimamo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia katika Amerika Kusini kukiwa na mechi moja ambayo imesalia kuchezwa.
Nchi zinazomaliza nne za kwanza ndizo hufuzu moja kwa moja
Atakayemaliza wa tano atacheza dhidi ya New Zealand na mshindi afuzu.
Wakati huo huo
Mabingwa wa Ulaya, Ureno wanatakiwa kushinda katika mchezo wao na Uswisi na jukumu kubwa lipo kwa nahodha Cristiano Ronaldo.
Ureno inahaha kukata tiketi kucheza fainali hizo ikiwa nafasi ya pili kwa pointi 24 nyuma ya Uswisi yenye pointi 27.
Endepa Ureno itashindwa kushinda mechi hiyo na kumaliza nafasi ya pili itasubiri kuchagulia katika timu nane bora zilizomaliza nafasi ya pili kwenye makundi na kucheza mechi mbili (play-off) za nyumbani na ugenini na mshindi kufuzu kucheza michuano hiyo ya kombe la dunia