Messi ndio huyo na Visit Rwanda

Kuhama kwa Messi kutoka Barcelona kwenda PSG kumeongeza thamani zaidi kwa ile kampeni ya Rwanda. Kutambulishwa kwa Messi kumeiongezea PSG kiasi cha followers millioni 2 na yeye binafsi ana zaidi ya 200M kwenye Instagram ambao kuanzia sasa neno Visit Rwanda litakua likionekana kwao mara kwa mara. Nadhani Warwanda watakua na furaha zaidi katika huu uhamisho wa Messi.

Kama mdau wa utalii nimefurahi sana kuona wenzetu wakijitahidi kufanya yaliyo bora kwa sekta yao muhimu ya uchumi. Hopefully na sisi one day neno Visit Tanzania litaonekana zaidi ya kwenye jezi ya Simba.​
 
we jamaa embu hakikisha kwanza Data zako kabla huja andika ama utupe source tukasome maana ume tulisha tango naona
psg ilikua na followers 19 M wame ongezeka karibu mara mbili yake sasa yaan ongezeko la 22 M sio 2 M kama ulivo andika
Pia umesema Messi yeye kapata wafuasi wapya 200M kitu ambacho sio sahihi kwa kua messi kabla alikua na followers 200M+ hivo kama ameongeza 200 M wengine alipaswa awe na 400M+ kitu ambacho sio sawa kwa kua mess bado ako na followers 247M+
 
Hiyo namba ya followers ya PSG kutoka 19M mpaka 40M haina uhalisia ni propaganda tu za mitandao ila so far hadi sasa ni 2M+.
Na kuhusu Messi nimeandika yeye binafsi anazaidi ya followers 200M which is equivalent na ulichoandika 200M+. Nadhani utakua hukuweka umakini katika nilichoandika
 
Hapa kwetu tunaendelea kupambana na ^magaidi^ kwanza, then tukiwa salama, milango itakuwa wazi tu hivi karibuni! πŸ™‚
Hata Rwanda PK anawafinya wapinzani wake walio nje na ndani ya Rwanda,tena anawauwa kabisa,anawaita magaidi,bila hivyo Rwanda isingetulia na kupata maendeleo makubwa kama inavyoonekana sasa.Kagame akili kubwa angecheka na nyani Rwanda pasingekalika.
 
Sisi Kingwangala alisema timu kubwa za huko ulaya(Man u,Chelsea,Man City) zenyewe ndio zinatutumia maombi zikiomba tuweke neno visit Tz kwny jezi zao.

Kwahio bado tunapitia maombi yalitumwa na timu hizo,tukimaliza zoezi Hilo tutatangaza team tukayoitumia kuweka tangazo letu,kuweni wavumilivu.

πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Yani we na utimamu wako mkuu unaamini team yenye neymar na mbape Hadi Leo hii iwe na followers 19ml serious?
 
Mkuu,una maanisha baada ya Messi kujiunga PSG wameongezeka followers 22M? hapo sijakusoma vizuri.
 
Rwanda wanailipa PSG Kiasi gani kwenye huo mkataba?
 
NINGETAMANI MAMA SAMIA AONE UZI HUU NA MAAFISA WA MALI ASILI ZETU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…