Kuhama kwa Messi kutoka Barcelona kwenda PSG kumeongeza thamani zaidi kwa ile kampeni ya Rwanda. Kutambulishwa kwa Messi kumeiongezea PSG kiasi cha followers millioni 2 na yeye binafsi ana zaidi ya 200M kwenye Instagram ambao kuanzia sasa neno Visit Rwanda litakua likionekana kwao mara kwa mara. Nadhani Warwanda watakua na furaha zaidi katika huu uhamisho wa Messi.
Kama mdau wa utalii nimefurahi sana kuona wenzetu wakijitahidi kufanya yaliyo bora kwa sekta yao muhimu ya uchumi. Hopefully na sisi one day neno Visit Tanzania litaonekana zaidi ya kwenye jezi ya Simba.