BilioneaPATIGOO
JF-Expert Member
- Jun 23, 2012
- 12,320
- 11,327
Maneno meng ya nini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lakini vile vile inawezekana pia huko Camp nou akachezea goli nyingi tu! Usibase sana matumaini yako na kuyaweka kwenye upande mmoja tu,Mpira ndivyo ulivyo mkuu au wewe ni mgeni kwenye soka?? Hebu nikuulize swali timu ngapi zimewahi kufungwa nyumbani na bado zikaenda ugenini na zikaibuka na ushindi?? Jibu ni rahisi sana, hiyo imetokea mara nyingi tu na haitakuwa mara ya kwanza kwa Chelsea. Isitoshe Chelsea hakupoteza mechi ya kwanza, hivyo bado anaweza kwenda kupata goli la ugenini na kupindua matokeo.
Juzi na jana kabla ya mechi mlisema Chelsea atachezea tatu sijui dozen. Baada ya mechi mmekuja na jingine tena.....Hakuna kitu kama hicho
Bado unawaza miujiza itatokea kama 2012Tarehe 14 March saa 22:45 siyo mbali mkuu. Baada ya hiyo mechi tutakutana hapa hapa kwenye huu "uzi" wako. Kwa sasa weka akiba ya maneno yako.
Yeah mkuu, historia huwa inajirudia.Bado unawaza miujiza itatokea kama 2012
Hakuna ajuaye ni maneno gani aliyoyasema Lionel Messi mara baada ya kufunga goli la kusawazisha dhidi ya Chelsea. Pengine kwa kuhisia yawezekana alifarijika sana baada ya kufunga goli kwenye mechi hiyo ngumu nyenye ushindani wa hali ya juu. "Nisiwafunge kwani wao kina nani?" yawezekana hayo ndiyo yalikua maneno aliyoyasema mara baada ya kufunga goli safi lililotokana na pasi murua ya Kiungo Andres Iniesta.
Messi amekua akibezwa sana hasa kutokana na kucheza mechi takribani saba dhidi ya Chelsea bila kufunga goli.. Ameifunga Real Madrid, ameifunga Manchester United, ameifunga Bayern Munich, ameifunga Juventus, ameifunga Paris Saint-Germain... Kwani hao Chelsea ni kina hasa mpaka asiwafunge?.
Wakati mwingine ili uwe bora inabidi uoneshe ubora kwenye mechi zenye ubora.... Ufanye vizuri dhidi ya timu kubwa. Ni kama Cristiano Ronaldo alivyozifunga Bayern Munich na Juventus msimu uliopita, akaonekana bora sana licha ya kwamba hapo kabla hakua amefunga magoli mengi.. Hichi ni kitu ambacho Neymar inabidi akifanye kama kweli ana dhamira ya kupambana na kina Messi na Ronaldo.
Eden Hazard kwa upande wake anapambana sana, anafanya vizuri kwenye mechi kubwa, mechi ambazo timu nzima inamtegemea yeye.. Mara nyingi amekua akifanya vizuri, hii imemfanya aendelee kua bora siku zote... Hazard anawafunga Man United, anawafunga Arsenal, anawafunga Tottenham Hotspur, anawafunga Manchester City na hata mechi hii dhidi ya Barcelona alicheza vizuri sana, pasi yake ndiyo iliyozalisha goli tamu la Wiliian.. Pengine Neymar nae ajifunze hiki kitu.
Messi na Ronaldo wanaendelea kua bora kwa sababu wanafanya vizuri kwenye mechi kubwa, mechi ambazo zinatazamwa na watu wengi duniani. Wakati kukiwa na maneno mengi kuhusu umri wa Ronaldo na uwezo wake kupungua, ghafla anaibuka kwenye mechi moja kubwa dhidi ya PSG anafunga magoli mawili muhimu na kuwanyamazisha wote waliokua wakibeza uwezo wake. Ni kama Messi alivyofanya kwenye mechi hii dhidi ya Chelsea, kabla ya mchezo wengi wanambeza na kusema... Hawawezi Chelsea... Hawezi kufunga dhidi ya Chelsea. Ghafla anaibuka na kufunga goli muhimu na wote waliokua wanambeza wanakaa kimya.
Hivi ndiyo mchezaji bora inabidi awe. Umuhimu wako unaweza usionekane kwenye mechi za kawaida, lakini kwenye mechi ngumu ni lazima uoneshe kua wewe ni bora. Ni kama alivyofanya Hazard, ni kama alivyofanya Messi, ni kama alivyofanya Ronaldo. Neymar bado ana nafasi ya kutuonesha kwamba yeye ni bora, hata Kama timu yake haitafuzu inabidi aoneshe kwamba alipambana kuhakikisha timu yake inapata matokeo na si kucheza soka lisilo na manufaa, soka ambalo watoto wa uswahilini husema kucheza na jukwaa.
Pengine Barcelona anaweza asifuzu, pengine Real Madrid wanaweza wasifuzu lakini Messi na Ronaldo wameonesha uwezo wao, wameonesha ni kiasi wanapambana kuhakisha timu zao zinafanya vizuri hasa kwenye mechi ambazo wanahitajika kwa kiasi kikubwa. Ni kama ilivyo kwa Eden Hazard, pengine Chelsea wanaweza wasifuzu lakini tayari ameonesha ni kwa namna gani amepambana na kujitoa kuhakikisha timu yake inafanya vizuri.
Sasa tujiulize vipi kama PSG hawatafuzu? Nadhani lawama zote zinamwendea Neymar. Na hawezi kuzikwepa kwani yeye ni mchezaji staa inabidi aoneshe ustaa wake pale anapohitajika, sio kufunga magoli matatu kwenye mechi ambayo timu yako imefunga magoli saba.. Hapo ina maanisha hata usingekuwepo timu ingeshinda Tu.
Pamoja na hayo yote, pongezi kubwa ziende kwa Lionel Messi, kwa miaka mingi sasa amekua msaada mkubwa kwa Barcelona. Messi anafunga kadiri atakavyo, anafunga kwenye Copa De Ley hadi kwenye UEFA Champions League, hachagui habagui. Anawafunga Alaves... anawafunga Real Madrid... Anawafunga Olympiacos... Anawafunga Chelsea. Huyu bado ataendelea kuwa mfalme pale Nou Camp pengine kwa miaka mingi ijayo kwani anaoneka si wale Leo wala kesho huyu.
Juzi na jana kabla ya mechi mlisema Chelsea atachezea tatu sijui dozen. Baada ya mechi mmekuja na jingine tena.....
Kwan kuna sheria inayozuia mchezaji asizungukwe na walinzi?.
Ivi ulitazama mechi lakini!! Ulimcheki messi alizungukwa na defennders wangapi?? Wengine walikuwa wanaogopa hata kumkaba/kumfata wanajua hili jamaa litatudhalilisha tuonekane mafala kama alivyowafanya FERNANDINHO, BOATENG,MARCELO,RAMOS,CASEMIRO manusura awavunje viuno. Messi hakubakiza mtu ktk hii dunia, omba ukutane na mchezaji yeyote wa zamani na wa sasa but sio kiumbe hiki kuwahi kutokea utajuta baba.
Kwan kuna sheria inayozuia mchezaji asizungukwe na walinzi?.
Mbona unaleta ujuaji hata angezungukwa na timu nzima suala ni nn wanatarget!.
Siwez kuacha kuangalia mechi kubwa kama ile boss!.Hakuna sheria inayozuia, but Messi kama unavyomjua ni mzee wa kukusanya kijiji.hata umkabe vipi laini atatumia njia yeyote usiyoijua wewe atakudhalilisha na atapenya...."waulize wakina marcelo na vijana wa Guardiola kilichowakuta hawatakisahau katika maisha yao" So mchezaji kama Messi anaandaliwa kabisa mabeki wakubwa wa kumzunguka anytime. Ndio maana nimekuuliza ulicheki mechi?
Ile suluhu haiwezi kumvusha chelsea wakipiga mpira kama ule wa pale darajan chelsea anaweza kusongaSiwez kuacha kuangalia mechi kubwa kama ile boss!.
Nadhan hatuelewan kitu kidogo tu mkuu.....kabla ya mechi yalikuwa maneno meeeeeeengi mara Chelsea anakufa,oooh watapigwa 3 na kejer kibao yaan tulikosa amani. Tukawaambia sio rahisi hivyo Chelsea kufungwa na Barcelona kama mnavyodhan na ndicho kilichotokea.
Baada ya mechi mmegeuza tena tutaua Camp Nou mara oooh Messi sijui nini na nini!. Hivi kuna mtu asiyemjua Messi na ubora wake?,iwaje leo ndo mtoe sifa nyiiiiingi as if ni kitu kipya kumbe ni kawaida kwa Messi kuwa bora.
Siwez kuacha kuangalia mechi kubwa kama ile boss!.
Nadhan hatuelewan kitu kidogo tu mkuu.....kabla ya mechi yalikuwa maneno meeeeeeengi mara Chelsea anakufa,oooh watapigwa 3 na kejer kibao yaan tulikosa amani. Tukawaambia sio rahisi hivyo Chelsea kufungwa na Barcelona kama mnavyodhan na ndicho kilichotokea.
Baada ya mechi mmegeuza tena tutaua Camp Nou mara oooh Messi sijui nini na nini!. Hivi kuna mtu asiyemjua Messi na ubora wake?,iwaje leo ndo mtoe sifa nyiiiiingi as if ni kitu kipya kumbe ni kawaida kwa Messi kuwa bora.
Ile suluhu haiwezi kumvusha chelsea wakipiga mpira kama ule wa pale darajan chelsea anaweza kusonga
Fact namaanisha wakizuia kama walivyozuia kule kwao wakifunguka ni msala.Wafanye kile wanachofanya kila siku huko epl "wapaki bus" lakini wasitegemee eti kuifunga Barca. Ndoto za mchana hizo...
Messi namkubali na barca ni chama langu, Ila ukweli huwa siupindishiLeo umeshusha nondo kweli kweli na umekiri mwenyewe kuwa MESSI NI MFALME. but unakosea kusema mfalme wa camp nou,,, unatakiwa umtambue kuwa yeye ni MFALME WA SOKA DUNIANI' hapo ningekuwelewa kamanda. Sasa just delete hicho kipande and then andika "MFALME WA SOKA DUNIANI KUWAHI KUTOKEA"
Kitu kingine Kamanda!
Messi kafunga magoli 6 kwa man city
Messi kafunga sio chini ya goli 9 kwa Arsenal.
Ahsante! Mungu akubariki.....