Messi vs Ronaldo: Nani zaidi?

Ronaldo anatamani angezaliwa zama tofauti na Messi ila walau awe mchezaji bora duniani, hayo si maneno yangu - ni ya anayemjua!

PS. Maurinho kaja na jipya majuzi, eti anadai hatuwezi kuwalinganisha kwa kuwa wote wanatoka sayari nyingi - ila ukweli anaujua, toka akiwa Chelsea amekuwa akiwaagiza mabeki wake wampige mabuti (yaani kamfanya hata Ozel mpole ampige kiatu)!
 
Ni sawa na kumfanansha dr slaa na dovutwa.. Ndio kusema messi ni hatariiiii hakuna binadamu kama yule kwa sasa kwnye football
 
Ozil ni mpole hadi wengine samahani waamfananisha kama mrembo acha niseme handsome tu tusiende mbali,ila gemu el clasico anabadilika kabisa hadi anataka kupigana mjerumani mwenye asili ya Uturuki.
 
Messi hana mfano kwa sasa, ronaldo ni bora kama messi asingekuwepo na pia anapenda sana amfikie messi kwa kutumia mabavu na uchoyo wa pasi za mwisho vitu ambavyo vinamfanya messi awe juu zaidi

upo sahihi mkuu ila kwa sasa naamini Iniesta ni zaidi ya Ronaldo.
 
Messy ni kitu ingine kabisa kwa karne hii,achana nae apite tu!
 
Wote ni wachezaji wazuri sana kwenye klabu zao hasa kwa ufungaji,kila siku wanavunja rekodi za ufungaji,lakini wote hawafanyi vizuri kwenye timu zao za Taifa.Messi ana advantage ya kucheza kwenye kikosi bora kabisa kilichowahi kutokea ambacho kimebebwa na backbone ya Wahispania(Busquet,Xavi,Iniesta).Miaka 2 iliyopita Messi alikuwa amemwacha Ronaldo kwa mbali sana lakini kwa sasa gap inazidi kupungua.Messi ni zaidi ya Ronaldo but tofauti ni ndogo sana
 


Heshima Mbele Belo...
Unaposema Messi amebebwa na kikosi Bora kilichowahi kutokea unamaanisha kwa Mji wa Catalan, Spain, Ulaya ama Dunia kwa ujumla?
Mkuu hebu fafanua tafadhali
 
Ronaldo ni mchezaji mzuri sana na angekuwa mchezaji bora hata kwa miaka 5 mfululizo kama Messi asingekuwepo na anafanya vizuri pia..kwa kifupi Tatizo kubwa sasaivi alionalo Ronaldo ni KUWEPO MESSI- Luis Felipe Scolari

Ronaldo na Messi ni wachezaji wazuri sana hakuna kama wao katika sayari hii ila Jamani unapomzungumzia Messi ni habari nyingine-Dino Zoff

Maoni yangu: Messi ni massive football Talent na Ronaldo vile vile ila Ronaldo anafanya Training sana kuwa hapo alipo...MESSI is slightly ahead of CR7
 
Heshima Mbele Belo...
Unaposema Messi amebebwa na kikosi Bora kilichowahi kutokea unamaanisha kwa Mji wa Catalan, Spain, Ulaya ama Dunia kwa ujumla?
Mkuu hebu fafanua tafadhali
Gang Chomba, kwa kipindi cha miaka 5 Barca wako kwenye peak duniani,hiki ni mojawapo ya vikosi bora ambavyo vimetokea Rijkard aliikuta Barca ikiwa hoi akaipandisha then Pep Guardiola akaendeleza kuipeleka mbele.Tangu Messi ameanza kuchezea Barca timu haijawahi kuwa kibonde
 
Last edited by a moderator:
Kusema kweli messi ni sayari nyingine, ronaldo hamfikii hata del piero enzi zake...

Del piero play for 19 season with juventus na hajawai kupata redcard..

A champions league winner, WORD CUP WINNER 2006, finalist of uero 2000 with a bronze medal, europa league winner with juventus, YOUTH world cup winner with italy 1995,,, a most paid footballer in year 2000,

Amepata standing oviations in santiago barnebeu from madrid fans in 2008, dunian ni wachezaji wawili tu waliopata hiyo heshima barnebeu del piero na ronaldinho, akaipata tena standing oviations old trafold in 1996 kwenye champions league na late 2009 kwenye neville fare way match, amepata standing oviations in dortmund 96 wakati huo dortmund ni bingwa mtetezi,, bila kusahau akaja kuwaua wajeruman hapo hapo dortmund katika signal iduna park kwenye world cup semi finals 2006 kwa goli tamu late..

Sasa ronaldo hata del piero hamzidi tutamlinganisha vipi na messii
 
MKATA KIU

  1. Del Piero ni bora zaidi ya Ronaldo sababu hajapata red card,hivi Zidane alipata red card ngapi na still ni one of the best
  2. Del Piero hajawahi kuwa mchezaji bora wa dunia wakati Ronaldo alikuwa mchezaji bora mwaka 2008
  3. Kweli Del Piero amebeba World Cup,Je Messi amewahi kubeba World Cup?
  4. Del Piero na Ronaldinho ndio wamepata standing oviation Santiago,Messi vipi?
  5. Ukipata Standing avation Santiago Bernabeu wewe ndio the best?
  6. Unajua kuwa CR7 anachezea Real Madrid,atapata vipi hiyo standing ovation
Tuache unazi usio na mantiki tuongee ukweli
 
Last edited by a moderator:
Messi ni moto ronaldo anafuatia


mi nashangaa sana watu wanapomlinganisha Ronaldo na Messi, kwanza kabla hatujaenda mbali hivi ushaona Mesi anavozingwa na kuwasasambua mabeki kama 4 au 5 hv,the guy is talented, Ronaldo huwa wala hakabwi kihivyo. Messi is another level bana jamani, mumpime na wakina de lima angalau au Zinaden hivi, au hata gaucho enzi zake walau
 

Kaka weka CV chini, mi del piero nimeweka CV weka na ya ronaldo sasa tulinganishe,, ronaldo hana lolote zaidi ya mchezaji bora wa dunia ambayo hata canavaro anayo,, ronaldo kacheza zama ambazo hakuna vipaji, del piero kavuma miaka hiyo kuna zidane, ronaldo di lima, beckham, rivaldo wapo kwenye peak tena wanatisha hasa na bado akawatingisha.. Sasa Taja CV ya ronaldo hapa ana nini zaidi ya hiyo uliyosema.

Tubishane kwa hoja kaka je zama hizo ronaldo angegusa hata tuzo yeyote.. Kupata standing oviations kwa opponents sio kazi rahisi lazima uwe kiwango cha juuu sanaaaaaaa.. We mashabiki wa simba wote wasimame kupigia makofi mchezaji wa yanga kwamba wamemkubali unafikiri mchezooo.. Sasa del piero kazipata zote za kumwaga hizo respect

Weka cv ya ronaldo hapa tulinganishe.. Unafikiri WORLD CUP glory NI KAZI mchezo nini,,, plus respect zote hizo
 
Last edited by a moderator:
Umetoa hoja ,nikakujibu kila hoja yako ,toa fact kupinga hizo hoja zangi sio unaleta ubishi usio na maana,kama humepndi Ronaldo sema humpendi kuliko unashindwa kabisa kutoa hoja ya maana.Halafu mdahalo ni Messi na Ronaldo wewe unazungumza habari ya Del Piero
 
Safi Sanaaaaaaaaa.CR7 Rules in two different Leagues in two different Clubs with different philosophy.
 

messi mercilessly messes ronaldo up!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…