Meta Yakabiliwa na Mashtaka Mapya Kuhusu Ukiukwaji wa Faragha Kupitia Miwani Yake ya AI

Meta Yakabiliwa na Mashtaka Mapya Kuhusu Ukiukwaji wa Faragha Kupitia Miwani Yake ya AI

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Kampuni ya Meta inakabiliwa na kesi mpya ya kisheria nchini Marekani kuhusiana na miwani yake ya kisasa ya AI (AI Smart Glasses) baada ya kuibuka kwa madai mazito ya ukiukwaji wa faragha za watumiaji. Kesi hii imekuja baada ya uchunguzi wa kina kufichua mambo ya kushtusha kuhusu jinsi data za wateja zinavyoshughulikiwa.

GettyImages-2173579322_694e93-e1774556179469.webp


Uchunguzi uliofanywa na magazeti ya nchini Sweden ulibaini kuwa wafanyakazi wa kampuni ya ukandarasi iliyopo nchini Kenya wamekuwa wakipitia na kutazama picha na video zilizorekodiwa na miwani ya wateja. Kitu cha kushtusha ni kwamba, maudhui hayo yalihusisha matukio ya faragha sana ya wateja, ikiwemo watu wakiwa watupu, wakifanya mapenzi, na wakiwa msalani.

Ingawa Meta ilidai kuwa mfumo wao huweka ukungu (blur) kwenye sura za watu ili kulinda utambulisho wao, vyanzo mbalimbali vilipinga vikieleza kuwa mfumo huo haufanyi kazi kwa ufanisi wakati wote. Taarifa hizi tayari zimeifanya Mamlaka ya Udhibiti wa Taarifa nchini Uingereza (Information Commissioner’s Office) kuanzisha uchunguzi wake dhidi ya Meta.
  • Matangazo ya Kupotosha: Walalamikaji wanadai kuwa Meta iliinadi miwani hii kwa ahadi kama vile "Imebuniwa kwa ajili ya faragha yako, na inadhibitiwa na wewe." Ahadi hizi ziliwafanya wateja waamini kuwa wapo salama na wasidhanie kabisa kuwa matukio yao ya siri yangeweza kutazamwa na wafanyakazi (binadamu) waliopo nchi za ng'ambo.
  • Ukubwa wa Tatizo: Kesi hii inaangazia ukubwa wa jambo hili kwa kueleza kuwa mwaka 2025 pekee, zaidi ya watu milioni 7 walinunua miwani hii. Inadaiwa kuwa maudhui kutoka kwenye miwani hiyo huingizwa moja kwa moja kwenye mfumo wa mapitio (review) bila wateja kuwa na chaguo la kujiondoa (opt-out).

  • Kwa upande wake, Meta imejaribu kujitetea kupitia sera zake za faragha na matumizi.
    • Kampuni hiyo iliileza BBC kuwa, pale watumiaji wanapoamua kutuma maudhui yao kwenye mfumo wa Meta AI, kampuni hutumia wakandarasi kupitia taarifa hizo ili kuboresha uzoefu wa watumiaji.
    • Meta inasema kuwa uwepo wa watu (binadamu) wanaopitia taarifa hizo umeelezwa kwenye Sera zao za Faragha (Terms of Service) hasa toleo la Marekani linalosema: "Katika baadhi ya matukio, Meta itapitia mwingiliano wako na AI... na mapitio haya yanaweza kufanywa na mfumo kujiendesha au na binadamu."
    • Msemaji wa Meta, Christopher Sgro, alisisitiza kuwa isipokuwa tu kama mtumiaji ameamua kutuma (share) picha au video hizo kwa Meta AI au watu wengine, maudhui yote hubaki kwenye kifaa chake pekee, na kwamba kampuni inachukua hatua za kuchuja data hizo kuzuia taarifa binafsi za utambulisho zisipitiwe.
 
Hilo jambo ni la hatari haya hiyo miwani bado magari ya self driving.
 
Back
Top Bottom