Methali zangu mpya: Mchango kwa lugha ya Kiswahili

Methali zangu mpya: Mchango kwa lugha ya Kiswahili

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
kila mpiga kasia hatulii mtumbwini na kila anayelima lazima anyanyue jembe! -
 
Kila atwangae ni lazima ashike mchi, na kila kitwangacho lazima kiwe kinuni.
 
Kila atwangae ni lazima ashike mchi, na kila kitwangacho lazima kiwe kinuni.

Jiko la shamba halichagui kuni
Mwana mwenzio kizushi akizuka mkatae
Pengo ni kulichekea ukilipa nyama latafuna
Alie juu mfate hukohuko
 
Kitanda cha misumari hakitungishi mimba!

Busu la kushtukiza halina maswali!
 
Mtoto wa samaki hafundishwi kuogelea.
Kiongozi juha haishi kupotoshwa na wasaidizi wake.
 
Ushikwapo shikamana

Upendwapo pendana

utishiwapo tishana?

Udanganywapo.........?

Uibiwapo.................?
 
Jiko la shamba halichagui kuni
Mwana mwenzio kizushi akizuka mkatae
Pengo ni kulichekea ukilipa nyama latafuna
Alie juu mfate hukohuko

Hi zi methali zimeegemea zaidi kwenye mambo yetu, kwa maana nyingine zinafanana.
 
kuzijua nyingi tambo.................si kigezo cha ujuzi wa mambo!
 
kula na kuliwa havitangamani

kula kabla hujaliwa

kilacho huliwa
 
Kila aendaye mbele lazima katoka nyuma, na yule abakiaye nyuma hajui tamu ya mbele.
 
haba na haba, haba mbili
mtaka cha uvunguni ajue ataumiza kiuno na mugongo
mpenda makuu, anataka kufaidi.
mgeni njoo, mwenyeji afilisike.
alalae usimuamshe, ukimuamsha; mtagombana/mtakesha wote.
 
Back
Top Bottom