Dr am 4 real PhD
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 20,877
- 43,633
Katika bara la ulaya Karne ya 19 Jina moja lilikua linatisha...
Chancellor Klemens matternich alitawala kwa miaka 27 (1821-1848)
Huyu bwana alitengeneza mtandao mkubwa wa upelelezi, uliosukwa kwa ustadi wa ajabu.
Woga ulienea kila mahali kila neno lililozungumzwa lilipaswa kupimwa kabla ya kutamkwa. Wanaharakati wa siasa mpya, waandishi wa magazeti, na wanafunzi walijua
“Metternich anasikia kila kitu.”
Mfumo huu wa ujasusi ulikuwa silaha kuu ya MATTER NICH kudhibiti mawazo mapya ya uhuru na demokrasia.
Hofu hii ilitengeneza jamii ya ukimya. Waandishi walijipiga marufuku wenyewe kuandika kuhusu siasa, wanafunzi walijiepusha na mijadala, na wanamageuzi walilazimika kuzungumza kwa mafumbo.
Mfumo wa upelelezi wa Metternich ulifanikiwa kwa kiwango kikubwa si kwa sababu ya teknolojia, bali kwa kutumia hofu kama silaha. Alijenga “utawala wa woga” unaotegemea taarifa, si risasi..
Maafisa wa serikali, wanajeshi wastaafu, wahudumu wa migahawa, na hata waandishi wa habari walijikuta wakiwa sehemu ya mtandao wa wapelelezi. Barua zote zilifunguliwa kisiri, vikao vya wanafunzi vilisambaratishwa, na hata mazungumzo ya faragha yaliripotiwa kwa mamlaka.
Wapelelezi walitembea mitaani wakiwa kama raia wa kawaida, lakini walijua maneno gani ya kuandika, nani wa kufuatilia, na nani wa kunyamazishwa..
Lakini kila mfumo wa hofu huwa na mwisho wake. Kadri mawazo ya uhuru yalivyoenea, hasira ya umma ikawa kubwa. Mwaka 1848, mawimbi ya mapinduzi yalilipuka kote Ulaya. Watu waliokuwa kimya kwa muda mrefu walisimama na kupaza sauti. Na hatinae UTAWALA WA MATTERNICH UKA ANGUSHWA RASMI 1848
MATTERNICH ERA 1821-1848 HIVYO MATTERNICH ALITAWALA KWA MUDA WA MIAKA 27 MFULULIZO MPAKA NGUVU YA UMMA ILIPO MTOA MWAKA 1848.