Mexico: Mikataba ya ukimya na malipo ya damu za waandishi wa habari

Joined
Jul 1, 2024
Posts
5
Reaction score
4
KAMA ANGEJUA KINACHOKWENDA KUMTOKEA BILA SHAKA ASINGEKUWEPO KATIKA ENEO SAHIHI KWA WAKATI USIO SAHIHI… LAKINI ANGEJUAJE, WAKATI KIFO NI FUMBO LA IMANI?

Sina uhakika kama asubuhi hii aliaga familia yake kwamba anakwenda kazini au la. Taarifa nyingi kuhusu maisha yake binafsi hazijulikani; kama hazikupotea, huenda hazikurekodiwlabda kwa sababu watu waliogopa kujihusisha naye au kwa sababu nyingine.

Lakini jambo moja nina uhakika nalo.

Asubuhi hiyo yenye mvua kiasi, yapata saa tatu na robo, alikuwa akiendesha gari lake aina ya Ford LTD, modeli ya 1980, katika barabara ya Avenida López Velarde (Ramón López Velarde) katika kitongoji cha Calonia Montebello jijini Tijuana jimboni Baja California kuelekea kituo chake cha kazi, ofisi za gazeti la ZETA.

Hakujua kwamba kulikuwa na magari mawili yaliyokuwa yakimfuatilia kwa muda mrefu.
Ghafla, gari aina ya Pontiac Trans-Am lilimpita na kwenda kumzuia mbele yake. Gari jingine likasimama nyuma yake.
Katika hali ya mshangao na kuzubaa, mwanaume mmoja mwenye silaha aina ya Calibre 12 Shotgun alitokea na kumfyatulia risasi mbili.

Moja ilimpiga shingoni na kutokea begani nyingine ikampiga tumboni.
Kifo kikamchukua pale pale.

Magari hayo mawili yakatoweka kupitia barabara ya Boulevard Agua Caliente, yakimuacha kifoni.Safari yake ya miaka 47 duniani ikafikia ukomo kikatili sana.
Aliacha simanzi kubwa kwa ndugu, jamaa na marafiki; kwa wananchi waliokuwa wakifuatilia makala zake za uchunguzi, na kwa bosi wake, Don Jesús Blancornelas.

Ilikuwa Aprili 20, 1988—miaka minane tangu kuanzishwa kwa gazeti la ZETA, ambalo alikuwa mkurugenzi mwenza na mwandishi nguli wa habari za kiuchunguzi.

Lakini swali kubwa likabaki:
Alikuwa nani?
Nani walimuua?
Na kwa nini aliuawa?

Vipi kuhusu Mafia Jorge Hanks Rhon?Kwa nini serikali zilikataa kumchunguza?

Majibu kamili ijumaa hii.
Usikose.
 
Hii ni AI?
 
Back
Top Bottom