Mexico imemkabidhi Marekani washukiwa wengine 37 wanaodaiwa kuwa wanachama wa makundi ya uhalifu wa madawa y, waziri wa usalama wa nchi hiyo amesema, hatua inayokuja wakati Rais wa Marekani Donald Trump akitoa vitisho vya kufanya mashambulizi ya ardhini dhidi ya magenge ya dawa za kulevya katika eneo hilo.
Uhamisho huo wa washukiwa wa magenge ya dawa uliofanyika Jumanne ni wa tatu kwa ukubwa ndani ya mwaka mmoja, na unafanya jumla ya waliokabidhiwa kwa Marekani kufikia 92. Waziri wa Usalama, Harfuch, alisisitiza kuwa hatua hiyo ilifanyika “kwa kuzingatia Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mexico na kupitia mifumo ya ushirikiano wa pande mbili na Marekani, huku heshima kamili kwa mamlaka ya taifa ikizingatiwa.” Aliongeza kuwa Mexico ilipata ahadi kutoka Marekani kwamba washukiwa hao hawatakabiliwa na adhabu ya kifo endapo watapatikana na hatia.
Rais wa Mexico, Claudia Sheinbaum, amepinga vikali uwezekano wa Marekani kuingilia kijeshi ndani ya Mexico katika vita dhidi ya magenge ya dawa za kulevya. Alieleza kuwa kukamatwa kwa dawa ya fentanyl mpakani kati ya Marekani na Mexico kumepungua kwa asilimia 50 kutokana na sera yake madhubuti ya kupambana na uhalifu wa dawa za kulevya.
==========
Mexico has sent another 37 alleged members of Mexican criminal organisations to the United States, the country’s security minister said, amid US President Donald Trump’s threat of ground attacks against drug cartels in the region.
The handover of alleged drug cartel members on Tuesday is the third major transfer to the US in the past year and brings the total number of suspects transferred to 92.
Source: Al Jazeera