Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Aliyekuwa Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime ameteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa kituo cha kuibua, kuzalisha na kulea vipaji vya soka cha Cambiaso Sports Management.
Akizungumza leo mapema kwenye Hotel ya Serena mbele ya viongozi wa Cambiaso Sports Management, Wanahabari na wadau mbalimbali wa soka nchini, Mecky Mexime amesema kuwa ameamua kupumzisha kichwa chake na kujikita katika soka la vijana na kuachana na timu za ligi kuu Tanzania.
"Nimeamua kupumzisha kichwa changu nitulie na soka la vijana kwasababu mpira wetu unaongozwa na wajinga wajinga ndo maana mpira hauendelei.
Kocha anafukuzwa na watu wajinga wajinga wasiojua mpira, huwezi kuongoza mpira wakati hujacheza mpira au taaluma hiyo huna.
Siku zote mpira unaongozwa na watu wa mpira, nenda Ujerumani kama hujacheza mpira, huna mambo ya mpira huwezi kuongoza mpira, nitajie Kiongozi gani ambaye hajacheza mpira Ujerumani lakini anaongoza mpira". amesema Mexime.
Kauli hii ya Mecky Mexime umeipokeaje Mdau wa Kandanda..?