Mexime: Tunafeli kwasababu viongozi wetu ni wajinga ndo maana mpira hatuendelei

Mexime: Tunafeli kwasababu viongozi wetu ni wajinga ndo maana mpira hatuendelei

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Aliyekuwa Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime ameteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa kituo cha kuibua, kuzalisha na kulea vipaji vya soka cha Cambiaso Sports Management.

Akizungumza leo mapema kwenye Hotel ya Serena mbele ya viongozi wa Cambiaso Sports Management, Wanahabari na wadau mbalimbali wa soka nchini, Mecky Mexime amesema kuwa ameamua kupumzisha kichwa chake na kujikita katika soka la vijana na kuachana na timu za ligi kuu Tanzania.

"Nimeamua kupumzisha kichwa changu nitulie na soka la vijana kwasababu mpira wetu unaongozwa na wajinga wajinga ndo maana mpira hauendelei.

Kocha anafukuzwa na watu wajinga wajinga wasiojua mpira, huwezi kuongoza mpira wakati hujacheza mpira au taaluma hiyo huna.

Siku zote mpira unaongozwa na watu wa mpira, nenda Ujerumani kama hujacheza mpira, huna mambo ya mpira huwezi kuongoza mpira, nitajie Kiongozi gani ambaye hajacheza mpira Ujerumani lakini anaongoza mpira". amesema Mexime.

Kauli hii ya Mecky Mexime umeipokeaje Mdau wa Kandanda..?
 
Kuna ukweli lakini,unajua mambo yetu sisi wabongo ni ya figisu nyingi sio soka tu hata kwenye biashara,elimu,kazi maofisini na mambo mengine,ishakua kama hulka yetu sisi wabongo kufanyiana mizengwe.hata malalamiko yake ni sehemu ya hulka za wabongo kulalamika.

Lakini pia unapokua kocha kufukuzwa ni kawaida kabisa wala sio ajabu.
Kama anataka afanikiwe ni vema apambane au akuze elimu yake ya ukocha kisha afungue mipaka atoke nje ya Tanzania ili afanikishe malengo yake.
 
Kwenye mpira wa Tanzania Kuna viongozi mambumbumbu Tena wenye kiburi, ivi katika Hali ya kawaida unamfungiaje mtu miaka mitano na fain million tano? Ni magenge ya wahuni ndio yanayo ongoza Mpira wa Tanzania.
 
Msimu uliopita Kagera Sugar walicheza play Off, mwaka huu wako nafasi ya chini kwenye msimamo wa VPL

Hata kama viongozi wako hawajacheza mpira lakini siku zote, timu ikifanya vibaya anayetimuliwa ni kocha.

Weka akiba ya maneno bado una safari ndefu kwenye ukocha, je Cambiaso Sports wakikutimua utasema kauli hii..?
 
Nadhani umelenga issue ya Makamu M/Kiti wa Yanga, lakini na yeye alihusika kuzitunga hizo sheria wakati yupo TFF, ambazo leo zimemhukumu.
 
Msimu uliopita Kagera Sugar walicheza play Off, mwaka huu wako nafasi ya chini kwenye msimamo wa VPL

Hata kama viongozi wako hawajacheza mpira lakini siku zote, timu ikifanya vibaya anayetimuliwa ni kocha.

Weka akiba ya maneno bado una safari ndefu kwenye ukocha, je Cambiaso Sports wakikutimua utasema kauli hii..?
Kwanini Kagera Sugar walicheza play off mwaka jana na kwanini mwaka huu pia wanaelekea huko?
Uwenda kuna mambo kwenye club Mexime kama kocha hakutimiziwa au aliingiliwa kimaamuzi kwenye taaluma yake ya ukocha ndo maana kakwamishwa na hao anaowatuhumu kuwaita hawajui kitu kwenye soka(wajinga wajinga).
 
Huenda kuna mambo hayaendi sawa pale Kagera Sugar.

Lakini ametumia maneno makali mno kufikisha huo ujumbe wake,

Japo ujinga ni kutofahamu jambo, lakini ameshindwa kuwaheshimu waajiri wake wa zamani ndo maana wamejibu kwenye Page Official ya Kagera Sugar.
 
Haya mambo yamesemwa toka kipindi cha akina Muhidin Ndolanga na FAT.

BTW:Mashirikisho ya ngumi nchini (BFT&TPBO) huwa naona viongozi wake wote wana mapengo ikiashiria pengine nao ni watu wa ngumi ila nako hamna kitu.

Au hayo mapengo ya akina Yassin Abdalah "Ustaadh" ni matokeo ya "Sapele water"?
 
Mexime aache hoja zisizo na mashiko, wachezaji anaozungumxia wa ujerumani wao wana elimu na uelewa mkubwa ndio maana wakiingia kwenye uongozi wanafanya vizuri.
Wachezaji wetu wengi walikimbia shule mfano mzuri kaonyesha Tenga kacheza mpira lakini kichwani zinachaji ndio maana alifanya vizuriangalia ceo wa Simba hajacheza mpira lakini ananuelewa mkubwa wa mpira.
Nilimshanga sana alipofukuzwa kagera sugar akasema anapumzika.badala ya kwenda kuongeza ujuzi au kutafuta hata timu nje ya nchi kiwaonyesha waliomfukuza walikosea lakini hawa ndio walewale wanqtaka wqpewe timu ya taifa kwa kigezo cha uzawa.
 
Wapo wengi tu ambao hakucheza mpira lakini wamepata mafanikio orodha ni ndefu

Huyu hakuridhika kutimuliwa kwake
 
Sema ni kweli mtu wa kutolewa mfano ni MWAKALEBELA, huyu jamaa anawakilisha viongozi wajinga tulionao kwenye soka la Tanzania.

Kwakweli mambo aliyokua akiyafanya Yanga afu unakuja kufikiria alikua kiongozi mkubwa pale TFF unabaki unashangaa sana.
 
Hii kauli yake jamaa mwanzo niliielewa baadae nikaikataa, mabosi wengi kwenye vilabu wanaoajiri makocha sio watu wa mpira ni wafanyabiashara, (Abramovich, MO, Sheikh Mansour (Man City), Khalid Khaldoon (PSG) etc) sasa wakikupa kazi ukashindwa kufikia malengo lazima wakufukuze, hapa sioni kosa lao.

Kama anawalaumu viongozi wa TFF sidhani kama hao ndio walimfukuza kazi vilabu alivyowahi kupitia, tatizo la Maxime alikaa hizo timu (Mtibwa na Kagera Sugar) muda mrefu sana, karibia miaka 20 akaridhika akajiona yupo nyumbani, wakati mabosi wake walikuwa na vision zao.
 
Umemaliza mkuu denooJ wala siongezi kitu hapo.
 
Ni bora ametumia neno 'wajinga' na sio 'wapumbavu' maana kuna kufauti kubwa.
 
Back
Top Bottom