Meya Issaya Mwita atoa tamko

Naomba ufafanuzi wa haya.
1. Theluthi mbili ya akidi ya wajumbe wa kumtoa Meya haikufika kikanuni , sasa ni kwa nini kikao kikaendelea?
2. Ni kwa nini Waziri mwenye dhamana na Tamisemi hajatoa tamko lolote hadi sasa?
2/3 ya wajumbe inatafutwa kwa kura , na ilishindikana kupatikana kwa vile waliopiga kura ya kumkataa meya walikuwa 16 tu badala ya 17 wanaotakiwa kikanuni , kwahiyo ilikuwa lazima kura zipigwe tu ili kujaribu kuona kama wanaweza kupata wanachokitaka .

Lingine unalotakiwa kujua ni kwamba ndani ya awamu ya 5 hakuna waziri yeyote mwenye mamlaka ya kupinga yaliyopangwa na ccm hata kama yatamdhalilisha waziri binafsi , hawa mawaziri wote unaowaona kazi yao ni kujibu maswali bungeni tu , waziri wa wizara zote ni yule aliyewateua .
 
Binafsi Nilikuwa Nahesabu siku tu huyu Meya kwenda CCM sababu alikuwa karibu Nao sana mpaka siku moja akaambiwa unafanya nini huko njoo uunge mkono juhudi sijui walipishana nini mpaka Wameamua kumfanyia uhuni huu hivi akienda mahakama ya jadi Mtamlaumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We endelea kuota tu
 
Wajumbe nane ambao hawakuhudhuria ni kina nani na ni wa chama gani? Kuna haja ya kuanza kushughulikiana kichama
 
Wazee wa kugushi hawajaanza leo wala jana. Kihiyo mnamkumbuka?
 
Watanzania tujenge tabia ya kuheshimu sheria na katiba.Utamu wa madaraka ni kuzingatia hayo mawili.Tusijenge taswila kwa vijana wetu kuwa waweza kupata madaraka kwa kuteuliwa bila ya kuchaguliwa,waweza kutoa maamuzi bila kushirikisha wadau wahusika,waweza kuvunja katiba usihojiwe nk
 
Naomba ufafanuzi wa haya.
1. Theluthi mbili ya akidi ya wajumbe wa kumtoa Meya haikufika kikanuni , sasa ni kwa nini kikao kikaendelea?
2. Ni kwa nini Waziri mwenye dhamana na Tamisemi hajatoa tamko lolote hadi sasa?
Unasubiri waziri wa Ccm atoe tamko juu ya maamuzi ya ovyo ya ccm wenzake? Au hukumsikia waziri mwezi April akikemea maDc kutoingilia fedha za jimbo na waziri huyohuyo akiwa Hai mwezi January mwaka huu akasema mwamuzi wa mwisho fedha za jimbo ni Dc?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wananchi wamejua hili. Hawamjali aliyetumwa bali aliyemtuma. Na wao kila mwanzo wa kauli zao humtukuza yule aliyewatuma ili kutafuta uhalali na mapambio ya sifa na utukufu ni mengi tu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…