Meya jiji la Arusha: Tutahakikisha tunafunga CCTV Camera mitaa ya Arusha

Meya jiji la Arusha: Tutahakikisha tunafunga CCTV Camera mitaa ya Arusha

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Meya wa Jiji la Arusha, Maxmillian Matle Iranqhe, amesema Halmashauri ya Jiji hilo imetenga zaidi ya shilingi bilioni 4 kwa mwaka wa fedha 2025 kwa ajili ya kuboresha miundombinu, ikiwemo ununuzi wa mitambo ya kutengeneza barabara.

Akizungumza na waandishi wa habari Februari 26, 2025, Meya Maxmillian amesema fedha hizo ni sehemu ya bajeti ya jumla ya shilingi bilioni 52.2 iliyopitishwa na Baraza la Madiwani.

Mbali na barabara, Meya amesema bajeti hiyo pia itatumika kuboresha usalama wa wananchi kwa kufunga CCTV camera kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha pamoja na kuweka taa za barabarani kwenye maeneo yenye giza.

 
Back
Top Bottom