PreGE2025 Meya Mwanza alalamika kufanyiwa figisu na wana CCM wenzake

PreGE2025 Meya Mwanza alalamika kufanyiwa figisu na wana CCM wenzake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Constantine Sima ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mhandu amedai kufayiwa hujuma na fitina zinazofanywa na baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM kwa maslai yao binafsi.

Akieleza kazi zilizotekelezwa katika kata hiyo kwa kipindi cha mwaka 2020-2025, Sima amesema kuna baadhi ya wananchama na viongozi ambao wamekuwa chanzo cha kurudishwa nyuma katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
 
Apambane na hali
Yeye mwenyewe hakufanya figisu kuwa hapo? 😀
Ni zamu yake
 
Kuelekea uchaguzi muku,

Hakuna haja ya kiongozi kuibua visingizio ikiwa amesense kukataliwa na wananchi hasa baada ya kushindwa kuwatumikia wananchi hao kulingana na ulivyo waahidi. Hakuna muda tena 🐒
 
Kuelekea uchaguzi muku,
hakuna haja ya kiongozi kuibua visingizio ikiwa amesense kukataliwa na wananchi hasa baada ya kushindwa kuwatumikia wananchi hao kulingana na ulivyo waahidi. Hakuna muda tena 🐒
Chawa msimu wa kujipendekeza kwa viongozi huu.
 
Angela kairuki anagawa pesa kama njugu huko kibamba
Juzi katoa 70000 kwa kila mjumbe.
Mtenvu kazidiwa baada ya kutoa 30000
Ccm ni janga
Ila njaa bwana yaani mtu anaenda mtajirisha mwenzake kwa ujira wa 30k na 70k
 
Hiyo ni trela tu, siku zinahesabika za kulivunja bunge ndio mtayaita maji maaa
 
Kama shida ni kusaidia wananchi kwanini ung'ang'anie kwani yeye ndo lazima awe meya?

Ufisadi na Wizi tu, miaka mitano alipokuwa anakula alikaa kimya, ameona dalili cha kiti kupokonywa anaanza kulalama, kwani kabla yake si alikuweko mwenzake aliyempisha? Anataka ashibe yeye tu?
 
Angela kairuki anagawa pesa kama njugu huko kibamba
Juzi katoa 70000 kwa kila mjumbe.
Mtenvu kazidiwa baada ya kutoa 30000
Ccm ni janga
Wanapo zidiana katika hii minada; huyo aliyezidiwa anarudishiwa pesa yake au vipi?
 
Back
Top Bottom