Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,273
- Thread starter
- #21
SteveD,
Hoja yako ina mantiki sana. Kupanga mstari wakati wa kupanda bus hata wazee, wagonjwa, walemavu na wasiojiweza wataweza kutendewa haki iwapo kutakuwa na utaratibu mzuri wa kupanda bus. Asante kwa kumbusha enzi za UDA. Yale ma-'Ikarus Kumbakumba' huu ndio ulikuwa wakati wake mwafaka kabisaa. Yakipita mawili matatu kituoni yanaondoa umati mzima. Lakini basi uwepo mwamko uliokuwepo enzi hizo wa kuweza kuwapisha viti watu wazima, wanawake wajawazito, na walemavu. Nakumbuka miaka ya 60 na 70 mwanamke akiingia kwenye bus kama hujapata kiti mwanaume bila kuombwa anasimama kumpisha kiti mwanamke - huo ulikuwa ustaarabu babu kubwa. Leo hii hata mjamzito hapishwi!! Aibu.
Yote haya yanatokana na uongozi mbovu wa walioshika/kukalia viti wanawaza starehe na matumbo yao na watoto wao na ilimradi wao na watoto wao wanapanda magari yenye viyoyozi they don't care a hoot!
Wazee, wagonjwa na na wengine wasiojiweza wananyanyasika sana. Kwa kweli bila magari makubwa yenye hadhi na uwezo wa kupakia abiria wengi na wale wasiojiweza, nchi yetu inajitengenezea wingu zito la kimaadili lisiloweza kurekebishika kwa takribani kizazi kizima. Tabia zinapojengeka tabia hizo kubadilika ni vigumu na huchukua muda.
Kama alivyosema Kibunango, watu wenye vipanya wanaweza wakawekewa mipango ya kununua hisa kwenye kampuni kubwa, sema - tatu au nne hivi zinazoweza kuanzishwa kwa ajili ya usafiri mijini. Mbona Saccos zimewezekana badala ya kila mmoja kuanzisha mfuko wake mwenyewe?! Shirika la UDA lilitufaa sana. Kwenye mabasi kulikuwepo na hewa safi na nafasi za watu kusimama, hata wenye mizigo walikuwa wanaweza kupanda nayo bila matatizo. Leo hii hata begi lako kwenda safari ya karibu tu katika kuunganisha safari ni kero. Mtu inabidi ukodishe teksi.
Ongezeko la vipanya na watu kuvichukia kutokana na kero zake ndiko huko in return kunafanya kuwe na haja ya kila mmoja ajitahidi kununua gari yake. Ambapo hilo nalo linaleta ongezeko la magari na msongamano wa magari usiokuwa na suluhisho maana miundombinu tuliyonayo haikidhi mahitaji. Na panapokuwa na misongamano ya magari, ina maana watu wanachelewa makazini, muda mwingi unatumiwa mabarabarani badala ya kuwa katika uzalishaji, uchafuzi wa mazingira kutokana na moshi wa magari, ongezeko la mahitaji ya mafuta unnecessarily kwenye supply zetu, lakini pia ni ongezeko la kero na chanzo cha hisia chafu (rages and frustrations) miongoni mwa wanajamii, ambapo jambo dogo tu linaweza kusababisha a big revolt dhidi ya watu na serikali.
Jamii nzima inajikuta imeingia kwenye a cycle of poverty kutokana na baadhi ya wachache tu, hususan viongozi kutowajibika katika majukumu yao.
This country deserves better!