Meya Raibu kaa kimya usifiwe au tenda haki uchukiwe

Meya Raibu kaa kimya usifiwe au tenda haki uchukiwe

zanku

Member
Joined
Jun 9, 2020
Posts
70
Reaction score
152
KINACHOMTESA MEYA JUMA RAIBU NI KAZI ZAKE

Anaandika Mwinjilisti Mathayo Chamshama


Trending news ya sasa katika siasa za kaskazini ni Juu ya kinachoitwa "Uchotwaji wa Milioni 150 za Benki ya KCBL" ambapo anatuhumiwa Mstahiki Meya wa Moshi Mhe Juma Raibu Juma, ambae ni mteja wa Benki hiyo wa muda mrefu hata kabla ya kuingia kwenye Siasa.

Mimi nimemfahamu Raibu akiwa hana "Uheshimiwa" wowote ule, alikuwa mfanyabiashara anaekuja kwa kasi sana katika Manispaa yetu, na nimeifatilia hii habari kwa undani nimembulia kung'amua mambo kadhaa yaliyonipa jibu ya Chanzo cha ili suala la uzushi na uongo lililopikwa kwa ustadi ila likakosa timing na angle nzuri, Hakika lingewekwa kwenye angle na timing sahihi lingeweza kumzima kisiasa Raibu kama ilivyokuwa imekusudiwa hasa kumwondoa kwenye cheo cha Umeya wa Manispaa.

Nimeongea na rafiki yangu wa KCBL amenidokeza kuwa Meya ni Mteja wao na hilo suala linalotumika sasa ni tukio la mwaka 2013 ambapo benki hiyo ilifanya makosa ikawaingizia wateja zaidi ya 30 wa (Fixed Deposit) Faida ya Riba ya kiwango kikubwa tofauti na mikataba yao hivyo Raibu wa miaka hiyo nae alikuwa mnufaika japo hakuwahi kuitoa ile fedha, Suala hilo liliisha kwa KCBL kutoa milioni 154 zilizozidi kwenye akaunti ya Mteja wao huyo na wengineo kwa viasi sahihi.Takukuru katika kuzipitia kesi hizo za wateja hao hawakumtaja hawakutoa taarifa ya kumshutumu Meya huyo kwa suala hilo ila kuna baadhi ya "Vigogo Ngazi ya Mkoa" maadui wa Mhe Raibu waliponasa kuwa nae ni mteja wakaamua kutengeneza hii tension mitandao kwa maslahi yao.

Tatizo kubwa linalofanya Meya huyu apitie haya ni kazi zake anazozifanya kwa wananchi wa manispaa hiyo hasa zile za sakata la kurejesha zaidi ya milioni 90 zilizokuwa zimeporwa na Saccos za Wahalifu fulani wenye nguvu ya pesa mkoani hapa, Sakata la kuwadhibiti wazabuni uchwara, Sakata la kudhibiti taasisi zisizowasilisha makato NSSF, urejeshaji wa mashamba,viwanja vya wanyonge na lile la kuvunja majengo yaliyojengwa kinyume cha sheria ya mipango miji. Hayo ndio yamemjengea maadui wakubwa wanaokesha na kuungana kuhakikisha anang'oka kwenye cheo hicho ambacho kimekuwa mwiba wa upigaji dili wa miaka yote.

Wosia wangu kwa Meya huyu either akomae kupigania wanyonge ili achukiwe au aungame kwa wapiga dili asalimike, kazi kwako Meya Juma Raib.

Mwinjilisti Chamshama
 
Jamani si umwache tu, atajitea mwenyewe bila kutumia nguvu, ama sivyo utafanya watu wazidi kuhoji.
 
Wewe Juma Raibu umesharudisha pesa zetu ulizokwapua hatuna shida na wewe chapa kazi sasa!
 
Back
Top Bottom