Tetesi: Meya wa Ilala aipa kampuni ya Kenya kazi ya kukusanya ushuru wa maegesho

Tetesi: Meya wa Ilala aipa kampuni ya Kenya kazi ya kukusanya ushuru wa maegesho

kazi ya kukusanya kodi za maegesho manispaa ya ILALA ambayo meya wake na naibu meya ni UKAWA imepewa kampuni ya Kenya airports parking service ya kenya ambayo haina usajili Tanzania.Hivi hizi kazi wazawa hawawezi fanya hadi apewe mkenya?

Mkuu YEHODAYA sidhani kama bandiko lako limebeba ukweli.Kampuni ya Kenya haiwezi kupewa tenda iwapo haina usajili Tanzania.Katika kujaza makabrasha ya tenda kuna vipengele kama certificate of incorporation,Licence,VRN & TIN lazima viambatanishwe.Pili mchakato wa kutoa tender kuanzia uchambuzi ufanywa na wataalamu wa Jiji mara nyingi maafisa biashara,wahasibu na kadhalika baada ya hapo hatua ya mwisho upelekwa katika ngazi ya madiwa hasa zile kamati zao husika.

Makampuni ya Kenya yapo mengi Tanzania lakini lazima yafanye taratibu za usajili kabla ya kuanza kazi mfano Equity,KCB na nk.Jiulize ni watanzania wangapi wamefaidika na huduma za mabank toka Kenya ?.Mbona serekali yako ya CCM iliwahi kuwapatia kampuni ya kikaburu tender ya kuendesha TANESCO haikuwa nongwa ?.

Tuache chuki za kisiasa linapokuja suala la kitaalamu tuweke kando siasa za maji taka.
 
kazi ya kukusanya kodi za maegesho manispaa ya ILALA ambayo meya wake na naibu meya ni UKAWA imepewa kampuni ya Kenya airports parking service ya kenya ambayo haina usajili Tanzania.Hivi hizi kazi wazawa hawawezi fanya hadi apewe mkenya?
Acha siasa chafu kama wasingekuwa na leseni walipataje vibali...?
 
Mkuu YEHODAYA sidhani kama bandiko lako limebeba ukweli.Kampuni ya Kenya haiwezi kupewa tenda iwapo haina usajili Tanzania.Katika kujaza makabrasha ya tenda kuna vipengele kama certificate of incorporation,Licence,VRN & TIN lazima viambatanishwe.Pili mchakato wa kutoa tender kuanzia uchambuzi ufanywa na wataalamu wa Jiji mara nyingi maafisa biashara,wahasibu na kadhalika baada ya hapo hatua ya mwisho upelekwa katika ngazi ya madiwa hasa zile kamati zao husika.
.

Hapo sasa hilo la BRELA ndilo kaa la moto kwa UKAWA.Watatwambia mbivu na mbichi kwenye hilo kuhusiana na hiyo kampuni kusajiliwa BRELA
 
sasa kama walishinda ulitakaje? si biashara hii? sioni tatizo labda ulikosa wewe au ni mambo ya wivu wa kike.
 
Hapo sasa hilo la BRELA ndilo kaa la moto kwa UKAWA.Watatwambia mbivu na mbichi kwenye hilo kuhusiana na hiyo kampuni kusajiliwa BRELA

Mkuu YEHODAYA usikimbilie BRELA pekee yako.Ukishapata Certificate of Incorporation unakwenda TRA kwaajili ya TIN na baadae VRN kutegemeana na ukubwa wa biashara yako kama inafikisha 100 million per year zamani ilikuwa 20 million per year baada ya huo mchakato unakwenda Jiji kwa afisa biashara ukiwa na clearance certifate from TRA kwamba huna madeni unapewa leseni na hao hao Jiji (afisa biashara).

Mpaka hapo madiwani hawahusiki,sana sana watakuja kuhusika katika hatua za mwisho mwisho baada ya uchambuzi kufanywa na wataalamu wa Jiji.
 
sasa kama walishinda ulitakaje? si biashara hii? sioni tatizo labda ulikosa wewe au ni mambo ya wivu wa kike.
Kampuni zilizoshinda zabuni ona zilivyopangwa kiujanja

Kenya Airport Parking Services Yenyewe imepewa Ilala ambako ndiko noti nyingi za maegesho zipo.Kwani kila siku maelfu ya magari huegeshwa Ilala na wafanyakazi,wafanyabiashara nk

Kampuni za kiswahili zimepewa uswahilini kusiko na biashara kubwa. Manispaa ya Kinondoni imepewa kampuni ya kiswahili ya UBAPA, wakati Temeke imepewa kampuni ya kiswahili ya UPAUKA.

Kampuni za kiswahili za UBAPA na UPAUKA hizo zimesokomezwa uswahili ambako ukipaki gari akija kudai ushuru mfanyakazi aweza kimbizwa na vibao.Kampuni zenyewe si unaona hata majina? UBAPA na UPAUKA.

Hiyo ya Kenya imepewa palipo panono ILALA
 
Watanzania ni wavivu mno bora wapewe hao wakenya walio serious na kazi.
 
Ninauhakika hii habari sio tetesi naibu meya KATAMKA MWENYEWE KIPINDI CHA ASUBUHI RADIO ONE kuwa hiyo kampuni haijasajiliwa BRELA
Hivi anayetoa tender ni Meya .....ni utashi wake au ...............
 
Hinawezekana izo kampuni za kibongo zilishindwa kuchukua ilala kwa sababu ya iyo pesa ya dhamana ambayo hata iyo kampuni ya kenya bado haijalipa ilikuweza kuanza kazi
 
Kazi ya kukusanya kodi za maegesho manispaa ya ILALA ambayo meya wake na naibu meya ni UKAWA wameipa kampuni ya Kenya airports parking service ya kenya ambayo haina usajili Tanzania.Hivi hizi kazi wazawa hawawezi fanya hadi apewe mkenya?
Wametekeleza ahadi ya Rais magufuli ya kuwataka "Wakenya waje kuwekeza Tanzania hata leo hii"
 
Mkuu inabidi upanuke katika kufikiri kwako. Kwani kwa mfano, Swissport ni Watanzania? Sijui hata unajua Swissport ni kitu gani na inafanya kazi gani muhimu inayuhusu mabilioni ya fedha hapa nchini.

Hatuwezi tukawa tunaongelea kuongeza ufanisi wa huduma nchini na wakati huo huo tunataka tugawe kazi hata kwa watu wasio na sifa kwa sababu tu ni Watanzania wenzetu. Hiyo mentality ni ile ya wewe ukiwa kabila au dini fulani kuajiri watu wa kabila lako au dini yako tu, hata kama hawana sifa. Hujaona matokeo ya hilo hapa nchini? Muhimu zaidi kutumia soko la East Afrika. Kufikiri kwako kunaweza kusababisha hata huduma za mabasi ya abiria kati ya Dar es salaam na Nairobi ziwe zinaishia Namanga kwa kila upande.
Umemjibu vizuri. Niongeze kuwa sula la tenda ni lakitendaji zaidi na linasimamiwa na idara ya manunuzi ambao ni waajiriwa wa serikali. Hivyo haiwezekani kwa utaratibu wa sheria ya manunuzi ukawa na such a free hand. Ukawa wanajua wanavyowinda hawawezi kufanya such an obvious mistake. Wanaoweza kufanya hivyo ni watu wa chama tawala tu na wanafanya kweli maeneo mengi tu.
 
Kazi ya kukusanya kodi za maegesho manispaa ya ILALA ambayo meya wake na naibu meya ni UKAWA wameipa kampuni ya Kenya airports parking service ya kenya ambayo haina usajili Tanzania.Hivi hizi kazi wazawa hawawezi fanya hadi apewe mkenya?
Kampuni za bongo nyingi magumashi, hawana commitment kwenye kazi. Mara nyingi tumezoea wanaoingia kwnye madaraka wanafungua campuni zao then wanazipa izo tender, sasa ukawa mambo ni tofauti. Em acheni arguments zisizo na umuhimu wacha professionals wapige kazi.
 
Back
Top Bottom