Meya wa Moshi kuingia darasani kufundisha wanafunzi na kumsifia Rais Samia mbele ya wanafunzi ni sahihi?

Hivi ni "introduction to biology" au "introduction of biology"?

The former inakukalibisha katika ulimwengu wa Biology and the later inakupa utangulizi kuhusu Biology
 
Huyu mwanasiasa anafundisha utopolo kwa watoto . Halafu magenius wa Kaizirege ( KEMEBOS ) wakipata single digits darasa zima kwenye matokeo ya necta wanasema wameiba mitihani .
 
Aache kupotosha watoto sasa ameandika nn hapo ubaoni.
 
Moshiblog UpdatesView attachment 2087057
MOSHI: MICHANGO YAPIGWA "STOP" MASHULENI, MEYA RAIBU AINGIA DARASANI KUFUNDISHA BIOLOGY

Moshi Kilimanjaro

• Meya Raibu apiga marufuku michango mashuleni, adai walimu wakuu waache watoto wa Rais Samia wasome bila bugudha
• Awaonya wazazi wasiopeleka watoto shule kujiandikisha, adai wasiogope, Rais Samia amekwisha lipa ada yote
• Awapiga msasa wanafunzi wa kidato Cha Kwanza

Mstahiki Meya wa Manispaa Ya Moshi Ndugu Juma Raibu akiwa katika ziara ya kutembelea Madarasa yaliyojengwa Kwa ufadhili wa Fedha za Uviko 19 amezungumza na waalimu na wanafunzi akifafanua faida kedekede za ujenzi wa madarasa hayo.

Meya huyo amedai tayari Kwa asilimia kubwa ujenzi umekamilika na Madarasa hayo yameanza kutumika na yamekuwa msaada mkubwa katika Manispaa hiyo.

Amesisitisa walimu wakuu kuacha mara moja kuwarudisha nyumbani watoto kwa kisingizio Cha michango kwani Rais Samia amekuwa akitoa bilioni 28 Kila mwezi nchini kote kugharamia uendeshaji wa shule za serikali. Namnukuu.

"Ndugu zangu walimu Kwanza niwapongeze Kwa kufanya kazi njema na bora sana ya kuwafundisha watoto wetu, lakini pili niwatake mwongeze bidii ili Manispaa yetu ipae zaidi na zaidi kielimu katika nafasi za kitaifa na tatu niwatake walimu wakuu kuacha mara Moja kuwarudisha mjumbani wanafunzi kisa michango kwani hela hizi zimeshalipwa na Rais Samia Kila mwezi Bilioni 28"

Lakini pia Mstahiki Meya huyo amewataka wazazi wote wa Manispaa hiyo kuwaleta na kuwaandikisha mashuleni watoto wote wanaopaswa kuanza shule za msingi na sekondari, kwasababu ni Elimu bila malipo. Namnukuu

"Watoto Waambie wazazi wote wawalete watoto waliobaki majumbani waje kupata Elimu ili iwe Mkombozi wa maisha yao na taifa Kwa ujumla na hivi sasa Elimu ni bila malipo kwani serikali ya Rais Samia inamaliza yenyewe Kila jambo"

Pia Meya amewataka wanafunzi hao kusoma Kwa bidii ili waje kulisaidia taifa siku za usoni, na Kwa msisitizo zaidi Meya huyo aliwafundisha wanafunzi wa kidato Cha Kwanza Somo la Baiolojia katika mada ya Utangulizi (Introduction of Biology).

MoshiBlog Updates
Hiyo suti mpka itapauka yani kibaka nimemuona nayo sio chini ya mara 4..
 
Sasa kuna shida gani ukimsifia Rais wako? Au siku hizi kumsifia Rais ni kuvunja sheria?

We jamaa una nongwa 😄😋
 
Hivi ni "introduction to biology" au "introduction of biology"?

Njia rahisi ya kutukama sisi ambao si native speaker wa kiingereza, ni hapo kwenye matumizi ya the, a, an, to, for, at na mengine mengi!
 
Back
Top Bottom