Mfadhili wa kitu fulani anafaidika vipi?

entry

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2018
Posts
286
Reaction score
539
Habarini wakuu, naomba niongeze maarifa, hivi mfadhili wa kitu fulani mfano NBC walivyofadhili ligi kuu wanafaidikaje, au unasikia mwanasiasa fulani kafadhili kitu.
Nia yangu nataka kujua faida anazopata iwe kifedha na sio za kifedha.
Naamini majibu yenu yatatusaidia vijana tuweze kuongeza nguvu ya ushawishi(kutaja faida atakazo zipata mfadhili) katika proposal zetu za kutafuta wafadhili katika shughuli zetu
Asanteni nawasilisha
 
Bila shaka huwa wanaanza kuweka hela na baadae wanachukua hela yao na faida baada ya ligi kuisha

Faida inapatikana kutokana na viingilio vya mashabiki pamoja na ile haki ya matangazo inayouzwa kwa aneonesha ligi kama azam

Faida ambayo ni nje ya pesa wanaamini ni njia ya kujitangaza zaidi na kuongeza namba ya wateja
 
Kuna faida nyingi sana mojawapo kubwa ni kujitangaza, kama nbc anatangaza biashara yake kwenye matangazo live ya nbc premier league.
Hapo anatapata wateja wapya na brand yake inakua sana si unajua biashara matangazo.

Kampuni pia za vinywaji na vitu vingine zinaongeza mauzo kupitia matangazo kuwavutia wateja wapya, unaweza kuwa na product nzuri lakini bila ya kuitangaza ni kazi kuwa na mauzo ya kueleweka.
 
Sasa mfano mfadhili wa asas za kiraia (NGOS) ambayo yeye ni mtoaji tu ananufaika vipi?
 
Nimekupata kiongozi shukrani
 
Reactions: Cpp
Hakuna kitu kama hiko.


mdhamini huwa ni mtu anayetoa huduma flani au kuuza bidhaa flani.
So yy anatangaza biashara yake. Anapata wateja unapoangalia mpira wa ligi kuu utaona matangazo yake kila sehemu kuanzia jezini, uwanjani hadi kwenye tv.
Pia ni moja ya njia ya kurudisha kwa jamii.
 
Sasa mfano mfadhili wa asas za kiraia (NGOS) ambayo yeye ni mtoaji tu ananufaika vipi?
Baadhi ya NGOs ni ustaarabu tu wa wazungu au watu weupe kuamua kusaidia wa afrika,yaan naona mungu huwa anaingia ndani mwao kuamua tu kutusaidia,maana unakuta huko hzo NGOs zilipoundwa ni kikundi cha watu wanaamua kukata vipato vyao kwa asilimia fulani na kuchangia kwenye NGOs

Lakin pia kuna baadhi ya NGOs zinaundwa na nchi fulani au taasisi fulani za watu wa huko nje unakuta wanamalengo yao binafsi,unakuta wanajifanya kufadhili ili waweze kufanya mambo yao ambayo yanaweza kuwa ni kuingiza tamaduni za kijinga kama ushoga au wanakuwa na lengo la kupata urahis wa kuwekeza biashara zao au kuiba rasilimali zetu
 
Kuna kampuni ambazo zinaweza kufanya kurudisha kwa jamii ila sio bank

Bank huwa wanautaratibu wa pesa izae pesa
 
Utanisahihisha kama nimekosea.
Kutokana na maelezo yako akili imeniambia inaitwa corporate governance( ile ya kurudisha fadhila kwa jamii inayozunguka hiyo biashara) na nafikili kuna sheria kabisa inayotaka wamiliki wafanye hivyo, ila ufadhili si jambo la hiari?
 
Kuna kampuni ambazo zinaweza kufanya kurudisha kwa jamii ila sio bank

Bank huwa wanautaratibu wa pesa izae pesa
me nimezungumza kwa jumla.
inaweza isiwe bank ikawa kampuni ya simu, maji, beer etc.
 
Ni hiari mkuu. Na ni mnatakiwa kushinda tenda. mfano board ya ligi wanakuwa na vigezo vyao.

hii dhana ya kurudishà kwa jamii ni kama mbinu ya kidiplomasia yaani kutafuta feva flani kwa jamii na serikali inayokuzunguka.(sina hakika kisheria kama unalazimika au ni moja ya masharti ya mkataba wa leseni)

mfano ww unachimba dhahabu halafu jamii inayokuzunguka hujengi hospitali hudhamini team Au taasisi nyingine zilizopo eneo lako etc.

ikitokea unahitaji eneo lingine utanue biashara yako unadhani serikali itampa kipaumbele nani kati yako na yule anayerudisha kwa jamii.
 
Bila shaka huwa wanaanza kuweka hela na baadae wanachukua hela yao na faida baada ya ligi kuisha
Tunahitaji mdhamini tupate pesa kuendeshea ligi sio tuje tena kumpa pesa.
 
Sasa mfano mfadhili wa asas za kiraia (NGOS) ambayo yeye ni mtoaji tu ananufaika vipi?
Kikubwa ni kujitangaza pia kutengeneza goodwill katika biashara

Kuhusu watu binafsi mara nyingi ni hatua katika mfumo wa maisha ya binadamu hierarchy of needs ambapo kuna hatua ya mafanikio hukifikia lazima urudishe kwa jamii

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Ili kuaminika na wateja na kupata wateja wapya, na pia miamala mingi itapitia benk yake kwaiyo faida kem kem
 
Sasa mfano mfadhili wa asas za kiraia (NGOS) ambayo yeye ni mtoaji tu ananufaika vipi?
Kwa nini wamagaribi wanafadhili NGOs?
1. Kutafuta ushawishi wa mambo yao kufanikiwa kirahisi.
2. Waliacha mali nyingi afrika so wanatumia hizo NGOs kama zuga ya kuleta mashushu wao kuzihamisha hizo mali kwa jina la NGOs/ufadhili/utaalamu nk.
3. Wanatumia ngos kufanya tafiti ili kuoba namna gani wanaendelea kufaidika na resources za afrika.
4. For future influence.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…