Mfahamju balozi Job Lusinde na kisa cha kusisimua wakati wa vuguvugu la mwaka 1994

Mfahamju balozi Job Lusinde na kisa cha kusisimua wakati wa vuguvugu la mwaka 1994

Kirikou1,
Naomba na mimi niweke hapa katika jamvi historia ya Balozi Lusinde kama
nilivyoiandika katika kitabu cha Abdul Sykes:
1953
''...mwaka wa 1953 Nyerere alipokwenda Dodoma kuhudhuia mkutano wa Kamati ya Elimu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Nyerere alifikia kwa Hassan Suleiman mmoja wa viongozi wa TAA na Nyerere akatambulishwa kwa wazalendo wengine waliokuwa wakiondokea katika siasa kama Oscar Kambona, wakati huo akifundisha katika Kikuyu Secondary School, Nsilo Swai na Kanyama Chiume ambao wote hapo baadae walikuja kuwa mawaziri katika Tanganyika huru. Kanyama Chiume naye vilevile alikuja kuwa waziri Nyasaland (Malawi) ilipopata uhuru.

1955
Haruna Taratibu, Omari Suleimani na marafiki zake wachache waliunda kamati ndogo kisha wakaandika barua kwenda makao makuu ya TANU Dar es Salaam kuomba ruhusa ya kufungua tawi la chama. Katibu mwenezi wa TANU, wakati ule Oscar Kambona, aliwaandikia kuwaeleza kuwa Hassan Suleiman tayari alikuwa ameshaisajili TANU na ikiwa uchaguzi wa viongozi haujafanyika basi waonanena na yeye pamoja na Ali Ponda. Omari Suleiman na Haruna Taratibu hawakuridhika na majibu kutoka makao makuu ya TANU kwa hiyo walikwenda kutafuta ushauri kwa Edward Mwangosi, aliyekuwa mwanachama mkongwe wa African Association. Mwangosi aliishauri kamati ile iitishe mkutano Community Centre ili kujadili kufungua tawi la TANU, na Hassan Suleiman na Ali Ponda waalikwe kuhudhuria. Kadhalika Mwangosi aliishauri kamati ile kuwaalika walimu waliokuwa wakifundisha Kikuyu Secondary School, wengi wao wasomi kutoka Makerere kuhudhuria mkutano huo. Mwangosi aliwaambia wajumbe wa kamati ile ndogo kuwa wasomi wa Makerere walikuwa ni muhimu sana kwenye chama kwa kuwa wangetoa uongozi uliokuwa unatakiwa.


Karibu ya watu arobaini pamoja na wale wasomi wa Makerere, miongoni mwao Job Lusinde walihudhuria mkutano ule. Lusinde alikuja kuwa waziri, na Amon Nsekela, alikuja kushika nyadhifa muhimu katika serikali na vilevile kuwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza. Hassan Suleiman na Ali Ponda hawakutokea mkutanoni. Wakati wanakusanyika kwa ajili ya mkutano, afisa wa Community Centre aliwaambia kuwa alikuwa amepokea amri kutoka kwa DC kuwa mkutano huo usifanyike. Kufuatia amri ile watu walitawanyika mara moja. Alexander Kanyamara aliyekuwa Mwafrika tajiri mjini Dodoma na rafiki wa John Rupia, wakati ule makamu wa rais wa TANU, aliwataka kuahirisha mkutano huo kwa sababu ya kutokuwepo kwa viongozi wa juu wa TAA, Hassan Suleiman na Ali Ponda. Kutokana na sababu hii na vile vitisho vya DC, mkutano uliahirishwa bila kupanga tarehe ya mkutano mwingine.

Asubuhi iliyofuata Taratibu alikamatwa na polisi na kupelekwa kwenye ofisi ya DC, (hivi sasa ofisi hiyo ni ofisi ya Waziri Mkuu). Taratibu alimkuta Hassan Suleiman pale ofisini akizungumza na DC, Bwana Smith. DC alianza kumsaili Taratibu kwa kumuuliza kama alikuwa akijua kuzungumza Kiingereza. Taratibu alijibu kuwa yeye hakusoma. Akizungumza Kiingereza Hassan Suleiman alimwambia DC kuwa yeye ndiye katibu wa TANU mjini Dodoma. DC, Bwana Smith, alimshutumu Taratibu kwa kuunda chama haramu na kwa kuitisha mkutano usio na idhini ya serikali katika Community Centre jana yake ambao ulielekea kuvuruga amani. Bila woga Taratibu alijibu kwamba yeye alikuwa na mamlaka ya kuitisha mkutano kwa sababu alikuwa mwanachama wa chama cha siasa kilichosajiliwa kihalali. Taratibu aliichomoa kadi yake ya TANU kutoka mfukoni kwake yenye rangi nyeusi na kijani na kumwonyesha DC. Bwana Smith alimuuliza Hassan Suleiman kama ikiwa na yeye pia alikuwa na kadi ya TANU. Hassan Suleiman hakuwa nayo. Hassan Suleiman na DC walizungumza Kiingereza kwa muda baada ya hapo aliwataka wote wawili kuandika maelezo yao. Baada ya kuandika maelezo yake Taratibu aliruhusiwa kurudi nyumbani. Inasadikiwa kuwa wakati ule mwanachama pekee wa TANU mjini Dodoma walikuwa Haruna Taratibu na Alexander Kanyamara ambae yeye alikata kadi yake Dar es Salaam.

Wasomi wa Makerere, ambao Mwangosi aliwaamini sana katika kuunda TANU, walipopata habari kuhusu mkasa wa Taratibu na DC, Bwana Smith, waliogopa. Waliamua kujiweka mbali kabisa na mambo ya siasa na kuendelea na kazi yao ya kufundisha. Haruna Taratibu na Omari Suleiman sasa waliamua kugeuza mbinu, waliitisha mkutano wa siri usiku nyumbani kwa Swedi bin Athumani. Mkutano huu uliamua kuwa Taratibu lazima aende makao makuu ya TANU Dar es Salaam akazungumze na Nyerere ana kwa ana kuhusu matatizo yaliyokuwa yakiikabili TANU Dodoma. Mahdi Mwinchumu aliyekuwa mwanachama wa TANU Dar es Salaam alijitolea kufuatana na Taratibu hadi makao makuu ya chama Dar es Salaam kwa kuwa alikuwa akijuana na viongozi wa TANU. Said Mussa mjumbe mwingine wa ile kamati ya siri alijitolea vilevile kufuatana na Taratibu na Mwinchumu hadi Dar es Salaam. Siku ya kuondoka Job Lusinde alikwenda stesheni ya gari moshi kuagana na ule ujumbe uliokuwa ukielekea Dar es Salaam, makao makuu ya TANU. Lusinde aliuambia ule ujumbe kuwa jamaa wa Makerere wanaunga mkono maamuzi yote yatakayoamuliwa na ile kamati ya siri...''

DrNIjpGaL-qZqZfcqbB44TA8TC5lhvae0QJjej80boqn77v0IX7NpkxdlHyd7X49sSvlpuQpRdNoSmf-w3Av-miVXaxwGF5lq_8CQbfJf95VdKW4E1uJeQz-ull-a_pGeP-fLrkpM04sACikNT3xuXLEpGdhi5j71iFmQPgxVGvEymXr6tDoY2_eB367L9UZ5Dm0I5WLdf9WE_VsdRG6_pjpV9__ihwo83JwOXUwoPV58RyP7K6dirQxdyZtDa8R0F2nDw0_foUa_DOoZJdn_TecwLzfVwJha8Fokeb_ihc2GdKwLlXAGWg3CPXOXqbmXBVAo01Bg3IwQLQZvrGe9eyoqXpCTG_N_Rpr80fcu5y_9gIsVOg7j_JeUTNaj1HXvlwL7VbnCg-wp2U85K_wNtIJ26jPfAOlovkJglLAW68XWVQgFNbfXrvdBoYTBUsqO6LUvPTr57_qkGXghXlebcxgDnqmf0o9DobzIptt19_oSoz7FuIaYCZA_xToMXX68L4ZMS5VGucnhIUBpznokgohXCbOaJACnt4APInT7DILY6eVQDLIAFRmmL4KnrFRa2I-D2MdMStKopv8GR_0RgnNwO06cxQ3-EGWVjY4WIab7npJ8sfiMg=w488-h629-no


Kushoto wa kwanza ni Ali Ponda
historia safi sana Mohamed Said
maka sasa tuna sintofahamu kuhusu nani alietengeneza ngao ya taifa ni kwa sababu kama hizi historia tumeitupa
 
Kirikou nikikutana na Mzee Lusinde Makaburi ya Kisutu nikenda kumwamkia na nikampa kitabu cha Abdul Sykes kisha nikamuomba nimpige picha akakubali. Nikiipata maktaba nitaiweka hapa Majlis.

8RRHlvGDAKCjxoGRK_vk5NW-9MkLr-xicfNGxeO-aQJL5C2fiOC_eMHKaKd9LI_JrExgZuCxnINleISKcyEreesap531KD7iVAMaN35szK8UZQ1gjHGFM4gocG2yiNPdr4gBl2HhooxhoeNgz3Kf69G8_RD2MkRAtRwxGq-tTF5W-HolEmTky7Mmk2ifhXqDaBL4geHcj0uv8K9KafLMdUiz3vl_qXGhQH_ccyWxbt00kVCuImfPB3oLJ3GM78JgUurNC-g_BED88jW8b3vEEWzNB6uQXzAa4y_drJ233LqQnHaf7qRoGu2h6gKkJ1dLAsCPefBXK4fclpz5fjGyS_PPkDmlfkXF1qX5g69xehCrtzeghq5N6UuCQtU4ewQVHhsfnSlLyDHIaGkBCoIrep652ffdcOKPh2p2Ua9WHdOE3lG29aqJjeMm8CGKFYDEZQMON2y73oCi3WEfSD1Oaa2qUl7uDCSmf7DyGHavfAMy1IviuoGY0oVsqqj8pXEftIbSwEoTSQSQkybHFI2l5FBEoUE3G4fDYbMfP8iKovOCZDYKP8v-PGUNOZc1w19p7LspJpKllM7oRD2HHH5IaH4VwKNU6qiAHLLOP9hcbI5crm4rlWzlbg=w338-h629-no

Job Lusinde Makaburi ya Kisutu
 
Huyo Mzee aliyevaa Suti
MeinKempf,
Naam ndiye Ali Juma Ponda kabila Mmanyema.

Katika kitabu alichohariri John Ilife, ''Modern Tanzanians,'' kuna historia ya
Ali Ponda na Hassan Taufiq Suleiman.

Historia yao inasisimua.

Hassan Suleiman alitoa nyaraka zake zote za TAA na kumkabidhi Rashid
Kawawa
kwa ajili ya Maktaba ya CCM Dodoma.
 
Hakuna Jaribio la Mapinduzi Duniani ambalo halilengi kumpindua Rais wa Nchi kasoro hili la Tanganyika 1964[emoji12][emoji12][emoji12]
 
Back
Top Bottom