Mfahamu Afande Sele

Mfahamu Afande Sele

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Afande Sele ni nani?

Seleman Msindi au Afande Sele (amezaliwa tar. 24 Aprili 1976) ni msanii wa muziki wa hip hop na Bongo Flava kutoka Mkoani Morogoro, Tanzania.

Amewahi kushinda tuzo ya (mkali wa ryhmes) mwaka [2003] kutokana na wimbo yake wa "Darubini Kali" aliyomshirikisha Dogo Ditto kwa sasa Lameck Ditto. Ni muasisi wa makundi ya 'Ghetto Boys' na 'Watu Pori', yaliozaliwa na kufia mjini Morogoro kwa kufuatana na alikuwa msanii wa kwanza kuujaza uwanja wa mpira wa miguu wa JAMUHURI mjini morogoro alipozindua albam yake ya kwanza ya 'MKUKI MOYONI'.

Aliongoza kampeni ya maleria mwanzoni mwamiaka ya 2005 na 2007. Mwanzoni wa mwezi wa 11 mwaka 2012 alitangaza rasmi kufanya kazi kama kundi jipya la watu pori baada ya kufanya kazi na MC KOBA ambaye ni miongoni mwa waliokuwa wakiunda kundi la watu pori miaka ya nyuma.

Ametoa Nyimbo nyingi kali ikiwemo MTAZAMO, Amani na Upendo, SIMBA DUME Na nyingine nyingi.Afande Sele kwa sasa ana video ya wimbo wake Soma Ule ambayo imeongozwa na mtayarishaji Raph Tz (upcoming video director) aliyepewa heshima na msanii huyo kufanya video hiyo ambayo imekidhi maudhui ya wimbo.

Huyo ndiye afande Sele wa Morogoro.
 
Anafaa kuwa the next Vice President of Tanzania. Na ikiwezekana President mbeleni kwani mabeberu hayawezi kumyumbisha. Au nasema uongo ndugu zangu?
Harafu washamdaka yupo central
 
Bado maelezo yako hayajajitosheleza Kwann anaitwa afande?
 
Back
Top Bottom