Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,391
Charles Dunbar Burgess King alikuwa rais wa 17 wa nchini Liberia aliyeshinda kwa kura za udanganyifu zaidi pia alikuwa mshiriki wa mkutano wa kwanza wa Pan- Africanism mwaka 1919 mambo ya muhimu yaliyojadiliwa katika mkutano huo yalikuwa ni mapambano ya waafrika dhidi ya utumwa na ukoloni.
Charles dunbar alikuwa rais wa nchini Liberia kuanzia mwaka 1920 mpaka mwaka 1930.
Katika kitabu cha Guiness World Record Rais King aliorodheshwa kuwa ni kiongozi ambaye alishinda uchaguzi kwa udanganyifu zaidi kuwahi kuripotiwa katika historia.
Katika uchaguzi wa mwaka 1927 nchini Liberia Charles Dunbar Burgess King alikuwa akichuana na Thomas Faulkner
Inaelezwa kuwa King alishinda kiti cha urais dhidi ya Thomas Faulkner ambapo katika uchaguzi huo wapiga kura walioandikishwa walikuwa 15000 lakini katika matokea ya uchaguzi King alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata kura 234000 yaani mara kumi na tano zaidi ya watu waliojiandikisha kupiga kura, mpaka sasa rekodi yake haijavunjwa na mtu yeyote.
King alizaliwa Machi 12 mwaka 1871 huko Monrovia, nchini Liberia
pia alikuwa mwanachama wa chama kikongwa cha siasa cha True Whig kilichoongoza nchini Liberia mwaka 1878 mpaka mwaka 1980.
King alichukua masomo wa sheria na kufanya kazi katika mahakama kuu nchini humo pia alikuwa miongoni mwa watu waliosaini mkataba wa amani wa Versailles mwaka 1919 nchini Paris baada ya vita ya kwanza ya dunia lengo lilikuwa ni kuiwajibisha Ujerumani kwa kusababisha vita ya kwanza ya dunia.
Pia King alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoka mwaka 1904 mpaka mwaka 1912 alichaguliwa kuwa katibu wa jimbo mwaka 1912 ambapo alishika wadhifa huo mpaka mwaka 1919.
King tangu alipoanza kampeni mpaka alipokuwa Rais kulikuwa na kashfa nyingi sana ambazo zilikuwa zikimuelekea.
Baada ya kushinda urais kwa njia zisizo za halali alipata maadui zaidi kwani watu wengi hawakumpenda na hali ya uchumi wa nchi yake ulikuwa katika hali mbaya kwa wakati huo.
King alilazimika kutafuta mkopo kutoka katika serikali ya Marekani jambo ambalo halikuwa rahisi maombi hayo yalichukua miezi saba kujadiliwa kwani Bunge la nchini humo lilikuwa limesitisha utoaji wa mikopo kwa nchi nyingine za nje ya Marekani.
Hata pale Bunge lilipotoa idhini juu ya mkopo huo lakini ofisi ya Rais ilizuia mkopo huo hivyo kufungua milango kwa Uingereza na Ufaransa na ilipofika mwaka 1934 kampuni ya mpira ya nchini Marekani iliyofahamika kama Firestone Rubber Company ilianza kusafirisha mpira kutoka Liberia kwanda nchini Marekani na kusababisha Liberia kuwa na matumaini makubwa katika biashara hiyo.
Liberia ilijiunga na kundi la kimataifa la kidiplomasia lililokuwa likiitwa The League of Nations mwaka 1919, kikundi hicho kililenga kudumisha amani , kuzuia milipuko ya vita na kutatua migogoro baina ya nchi.
King alikabiliwa na tuhuma za kijihusisha na kazi za kulazimishwa kwa wananchi na biashara ya utumwa japo kuwa alipokuwa mahakamani alikana mashtaka hayo lakini uchunguzi ulipofanyika King alikutwa na tuhuma za kuhusika na biashara ya utumwa na rushwa.
Kutokana na makosa hayo Rais King na makamu Edwin Barclay walijiuzulu mwaka 1930 na mwaka 1931 Liberia alifanya tena uchaguzi wa Rais ambapo Thomas Faulkner aligombea tena kiti cha urais lakini alishindwa.
Huyo ndiye Charles Dunbar Burgess King Rais aliyeingia madarakani kwa udanganyifu mkubwa kwa kupata kura mara 15 zaidi ya idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura.