Mfahamu Christina Charles Malema

Mfahamu Christina Charles Malema

Joined
May 20, 2017
Posts
24
Reaction score
15
Huyu ni diwani pekee mwanamke kuongoza kata kwa kuchaguliwa kwa kura 5789 mwaka 2010 tangu wilaya ya chunya ianzishwe mwaka 1941, awali alihudumu kama boharia wa duka la ujamaa la pembejeo yaani MBECU na baadae alikuwa karani wa kampuni ya tumbaku TLTC mpaka mwaka 2000 alipojitosa kwenye medali za siasa na kuhudumu kama diwani viti maalumu had 2010 alipochaguliwa kuwa diwani wa kata peke.

Mpaka sasa record hiyo anaishiria licha ya kushindwa kwenye kura za maoni za chama cha mapimduzi CCM kwa hira za aliyekuwa mwenyekiti wa CCM na halmashauri ya wilaya ya Chunya ambaye hakuwa anajua kusoma wala kuandika bwana mashoto

Nilimfahamu mama huyu shupavu na muwazi kwa kile anacho kiamini tofauti na wanalumumba wengi kwani aliwahi kulieleza baraza la madiwani kuwa mbunge victor mwambalaswa si mtu sahihi na anakwamisha maendeleo ya jimbo la lupa na wilaya ya chunya kwa ujumla

Alizaliwa tarehe 5 mwezi wa kwanza mwaka 1960 wilayani chunya kijiji cha Mapogolo, alihitimu shule ya msingi Mapogolo mwaka themanini na mbili kabla ya kujiunga na Songea Girls na kuhitimu elimu ya upili mwa 1985 na mwaka uliofuata alijiunga na CHUO cha uahirika MOSHI akisoma ngazi ya certificate ya community account and development.

Ana wanae wa kiume wawili yaani Geofrey na Joel na wakike wawili ambao ni Salome na Deborah

Siku zote amekuwa muumini wa ujamaa na elimu.Kwa sasa ameachana na masuala ya siasa huku mwanae Geofrey Mwambega kwa sasa ni mchambuzi wa masuala ya siasa na uchumi kusini kwa jangwa la sahara radio kama Baraka Fm ya Mbeya, Bomba fm na Mbeya Highland fm zote za mkoani Mbeya.
 
Dogo acha bi mkubwa apambane mwenyewe maana nina imani tangu ajitose kwenye hizo siasa za Chunya, hukuwa na msaada wowote ule kwake! zaidi tu ya kumpiga mizinga ili ukatanue na watoto waroho kwenye shule za sekondari ulizosoma huku ukijigamba ya kwamba mama ako ni tajiri na pia ni mbunge wa viti maalumu; kumbe alikuwa ni diwani tu wa viti maalumu!
 
Back
Top Bottom