Mfahamu Gen Noriega na operesheni Nifty Package ya wamarekani

Mfahamu Gen Noriega na operesheni Nifty Package ya wamarekani

Jc Simba

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
300
Reaction score
423
upload_2017-7-31_16-13-43.png



General Manuel Antonio Norriega

Manuel Antonio Noriega Moreno (Spanish pronunC.I.A.tion: [maˈnwel noˈɾjeɣa]; February 11, 1934 – May 29, 2017) alikua mwanasiasa na mwanajeshi wa nchi ya Panama pia infoma wa C.I.A. wa kipindi kirefu. Alikua mtawala wa kijeshi wa Nchio ya Panama na dikteta 1983 mpaka 1989 wamarekani walipovamia nchi hiyo kijeshi na kumuondoa madarakani.

Alizaliwa jijini Panama na kusoma katika moja ya shule za kijeshi mjini lima na baada ya hapo ya sekondari ya Americans. Baada ya hapo alijiunga na jeshi la Nchi hiyo na kuwa mmoja wa maafisa wa jeshi,alifanya kazi kwa karibu na mkuu wa intelijensia wa jeshi la nchi hiyo na kupanda vyeo ambapo baada ya Omar Torrijo ambaye ndiye aliyekua mkuu wa intelijensia wa jeshi kufanya jaribio la mapinduzi na kushinda alipewa nafasi hiyo mwaka 1968.Baada ya kifo cha torrijo mwaka 1981,Norriega alijiimarisha kiutawala mpaka akawa kiongozi wa panama ingawa sio rasmi mwaka 1983 (de facto ruler of panama). kuanzia mwaka 1950 mpaka karibu na kipindi ambacho Marekani walikuja kumvamia, Norriega alikua akifanya kazi kwa karibu sana na C.I.A. Norriega alikua moja ya vyanzo muhimu vya kuamnika vya C.I.A. kwenye masuala ya intelijensia, pia ilikua ndio sehemu muhimu ya kuanzishia, kupanga pamoja na kupitishia silaha na fedha linapokuja suala la operasheni yoyote inayohusu masuala ya kijeshi marekani ya kati na kusini.

Norriega pia alijihusisha na biashara ya madawa ya kulevyahas cocane kwa kiwango cha hali ya juu kitu ambacho wamarekani walikifahamu fika kwa miaka mingi, ila waliliruhusu suala hilo liendelee kwa sababu za umuhimu wa Norriega kwenye masuala ya kijeshi na kiusalama katika ukanda huo wa marekani ya kati na kusini.

Utawala wa Norriega katika Nchi hiyo uligubikwa na ukandamizwaji wa vyombo vya habari, uimarishwaji wa jeshi, pamoja na uteswaji na ukandamizwaji wa mahasimu wa kisiasa. Noriega aliweza kusimamia uchaguzi wowote na kupata matokeo anayotaka yeye, alijitengenezea utajiri mkubwa kupitia biashara yake ya madawa ya kulevya. Taratibu mahusiano yake na Nchi ya marekani yalianza kupungua kwa sababu ya vitendo hivyo pamoja na kuanza kuuza taarifa za kiintelijensia kwa mahasimu wa marekani. Mwaka 1988 Norriega alibainishwa kwamba ni mmoja wa watu wanaosafirisha madawa ya kulevya katika miji ya Miami Florida. Marekani waliiivamia Panama 1989 na kumuondoa madarakani na kumpeleka marekani kama mfungwa wa kivita.

alisomewa makosa nane yanayohusiana na kuuza madawa ya kulevya kupanga na kusafirisha madawa ya kulevya na utakatishaji wa fedha haramu. Mwaka 1992 alihukumia kifungo cha miaka 40 jela mbapo kilipunguzwa na kuwa miaka 30 jela.

Kifungo cha Norriega nchini marekani kilisitishwa mwaka 2007 baada ya Nchi ya Panama pamoja na Ufaransa kuomba kumuhukumu bila yeye mwenyewe kuwapo mahakamani kwa mauaji mwaka 1995 na utakatishaji wa fedha mwaka 1999. ufaransa ilikabidhiwa mtuhumiwa huyu mwaka 2010 mwezi wa nne baada ya ombi lao kukubaliwa na alifikishwa Paris 27|4|2010 na baada ya kesi yake kusikilizwa upya alihukumiwa kifungo cha miaka saba, mwezi wa saba 2010. Makubaliano ya kumhamisha gereza kutoka Ufaransa na kumpeleka Panama kutumikia kifungo cha miaka 20 yalifikiwa ikiwa ni vifungo vyote vilivyomkabili nchini marekani pamoja na ufaransa hivyo alipelekwa panama 23|09|2011. Norriega alifariki katika hospitali ya Santo Thomas katika jiji la Panama 29|05|2017 miezi miwili baada ya uperation ya ubongo.

MAISHA YA MWANZO NA FAMILIA

Noriega alizaliwa katika jiji la panama,katika familia ya kimasikini ya mestizo au mchanganyiko wa rangi ambayo inajumuisha wazawa wa marekani,waafrica na waspaniola.Mama yake anazungumziwa kuwa mpishi na dobi na baba yake alikua muhasibu na hakuishi muda mrefu na mama yake alifariki kwa maradhi ya kifua kikuu wakati Noriega akiwa mdogo.Noriega alilelewa na bibi yake katika apatimenti ya chumba kimoja katika makazi ya watu wengi holela (slum) za mji wa Terraplen.Waandishi wa habari na wa vitabu wanasema kwamba sio mtoto halali wa Ricaurte Noriega bali ni mtoto wa house boy wao ambaye uinasadikiwa alitembea na mama mwenye nyumba ,houseboy huyo alijulikana kwa jina la Moreno.

Norriega alipata elimu yake ya mwanzo Escuela República de México, na baadae katika shule ya sekondari inayoheshimika sana jijini Panama kwa kuzalisha wanamapinduzi wengi na viongozi wa kisiasa ya Instituto Nacional . Akiwa katika shule hizi alikua naelezewa kama kijana ambaye yuko makini muda wote. Pia anaelezewa kama kijana aliyependa sana kusoma na alikua anavishwa vizuri na mlezi wake.

wakati akiwa Instituto Nacional, alikutana na kaka yake luis ambaye ni nduguyake na alikua mwanaharakati katika shule hiyo ,norriega kabla ya hapo hakuwahi kukutana na ndugu wa kuzaliwa kwa upande wowote sio mama wala baba. Huyu Luis ndiye hasa alimleta Norriega kwenye siasa na kumpeleka kwenye chama cha kijamaa upande wa vijana. Kuna wakati alikua akiishi pamoja na kaka yake. Wakati akiwa katika chama hicho upande wa vijana alishiriki katika maandamano na pia kuandika baadhi ya makala ya kukosoa uwepo wa Mrekani katika Panama.Katika wakati huu ndio inasadikiwa kwamba ndipo wamerekani walimchukua katika kitengo chao cha intelijensia na alikua akitumiaka katika kuwapa taarifa wamarekani za kikundi cha wanaharakati wenzake akiwemo kaka yake. aliendelea kufanya kazi na wamerekani katika sehemu mbalimbali mpakamwaka 1980 na inasadikiwa aliwahi kulipwa kiasi cha usd 10.70 mwaka 1955 ambapo ilikua ni moja ya malipo ya awali ambayo aliendelea kulipwa kwa mda mrefu kwa kutoa taarifa hizo.

Baada ya kumaliza katika shule ya Instituto Nacional alipata scholarship kwenye chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Chorrillos Military School kilichopo Nchini Peru mjini Lima kwa kusaidiana na Luis ambaye tayari alikua anafanya kazi katika ubalozi wa panama nchini Peru.Alikua na ndoto zilizoota mbawa za kuwa daktari ila alishindwa kupata nafasi katika chuo kikuu cha Panama. Akiwa nchini peru alitengeneza urafiki na Roberto Díaz Herrera, ambaye baadae alikuja kuwa rafiki wa karibu na muhimu sana.

Norriega baadae alioana na Felicidad Sieiro de Noriega, ambaye walikutana mwaka 1960 na walifanikiwa kupata mabinti watatu ambao ni Lorena, Sandra and Thays Noriega. Siero alikua ni mwalimu wa shule na Norriega alikua mwanajeshi. familia ya mkewe Norriega haikufurahishwa na ndoa hiyo, pamoja na hayo Norriega anaonekana hakuwa na utulivu katika ndoa yao na mara kadhaa mkewe alisikika akitaka ndoa hiyo ivunjwe ingawaje baadae alibadili mawazo na kuendelee na mumewe. wahusika hawa wanne wa familia hii ya Norriega wanaripotiwa kwamba walikuwepo wazima wa afya wakati wa kifo cha Norriega.

ITAENDELEEAAAA
 
kiongozi endelea kutushushia vitu vya huyu jamaa maana nilikua namsikia tu kwamba ni katili .
ingawaje I am the first to reply
 
Alijificha ubalozi wa vatican, wanajeshi wa marekani wakaenda kupiga mziki kwa sauti ya juu sana baada ya siku tano jamaa ikabidi atoke mwenyewe
 
Shirikinaa na Marekani kwa akili,wanakutumia wakikuchoka wanakufanyizia
 
NORRIEGA AKIWA JESHINI
Norriega alihitimu chuo kikuu mwaka 1962 na alisoma maswaala ya injinia. Alirudi panama na alipewa kazi ya uanajeshi katika jeshi la nchi hiyo Panama National Guard, na kupelewa Colon ambapo alikupewa commission na kuwa sublieutenant mwaka 1962. Bosi wake katika ofisi zao hapo Colon alijulikana kama Omar Torrijo na alikua major katika jeshi.Muda mfupi badae alikua mfuasi wa karibu wa Torrijo, ingawaje tabia yake ya kunywa kupita kiasi na ukorofi bado kidogo ingewagombanisha na Torrijo ambaye alikua pia mtetezi na mentor wake.
pamoja na hayo yote torrijo aliendelea kuulinda na kuuendeleza urafiki wao kuhakikisha walikua wapo kwenye mstari mmoja pia alimleta Díaz Herrera kwenye uniti moja.Diaz na Norriega wakawa marafiki washindani kwa feva ya Torrijo.Mwandishi mmoja nayejulikana kwa jina la Galvan anasema kwamba torrijo alimsaidia aache tabia yake ya kuwabaka machangudoa. Pia Galvan anaendelea kwamba Norriega alikua na tabia ya kihuni ambapo kuna kipindi alisadikiwa kumbaka binti wa miaka 13 na kumpiga kaka yake binti huyo na kwa kosa hilo waliondolewa kwenye mji huo kwa miezi mpaka Torrijo alipoingilia kuzuia adhabu zaidi.
Norriega alimaliza adhabu na kurudi kwenye kazi na akaungana na Torrijo na mwenzake Diaz ambao walikua wamehamishiwa kitongoji cha chiriqui. Kulifanyika uchaguzi Mkuu mwaka huo na mgombea alitoka kwenye kitongoji hicho aliyeitwa Arnulfo Arias, na rais wa kipindi hicho Rodolfo Chiari aliamuru Torrijo na kikosi chake wawaharasi Arias na wanachama wa chama chake kupunguza ushawishi wa kwenye chama hicho kwenye uchaguzi huo. Torrijo alimuachia kazi hiyo Norriega ambaye vijana wake waliwakamata baadhi ya wanachama na wafuasi wa chama hicho na kuwatesa na kuwapiga na baadhi yao walilalamika kuwa walibakwa wakiwa mahabusu na kitendo hiki kilimfanya apewe suspension ya siku kumi kitu hiki kinasemekana kiliwafikia wamarekani pia.
Akiwa lieutenant mwaka 1966, Norriega alitumia miezi mingi kwenye kozi kwenye shule moja ya marekani kwenye masuala ya kijeshi huko Fort Gulick maeneo ya Panama canal zone.mwandishi wa habari John Dinges anasema kwamba Torrijo alimpeleka shule kumbadilisha tabia na kuishi kama Torrijo alivyotarajia .Norriega hakufanya vizuri sana kwenye masomo yake ingawaje mwaka 1966 alipandishwa cheo na Torrijo alimpa ofisi kama mpelelezi kwenye ukanda wa kasikazini wa jeshi .Muda mfupi baadae alirudi tena kwenye chuo kile kwa ajili ya kujiendeleza zaidi.kwa kipindi kirefu alishiriki kwenye kozi za operesheni za ardhini ,counterintelligence, intelligence, and jungle operations. pia alichukua kozi za operasheni za kisaikolojia katika chuo cha FOrt Bragg huku Calfonia na kazi yake ilikua ni kwenda kuvuruga chama cha wafanyakazi kilichokua kimeanzishwa na wafanyakazi katika kiwanda cha United fruit company na alifanikiwa kwa kiwango kikubwa hapa nataka niongeze jambo kwamba hata wafanyakazi wa nchi zetu hizi wawe makini ni kina nani wanawaongoza isijekuwa kuna watu wa aina ya kina Norriega kwenye vyama vyao tena wakiwa na nyadhifa za juu. Mkuu wake mpya alifurahishwa kwa kazi nzuri aliyoifanya na alikua ni ant communisti,na alihakikisha Norriega anakua na nidhamu ya hali ya juu.Ripoti zinaonyesha kwamba pamoja na kuwa na shighuli nyingi bado aliendelea kutuma taarifa za kijasusi kwa wamarekani kama awali hasa kuhusu wafanyakazi wa mashamba yale makubwa ya ile kampuni. Uongozi wa Lyndon Johnson ulihitimisha kwamba norriega atakuaja kuwa mtu muhimu wa dhamani kwa kuwa alikua ndio mwanajeshi chipukizi wa maswaala ya kijasusi na nyota yake ilikua inachipua kwa kasi. Norriega aliendelea kuwa namahusiano na chuo alichosoma cha wamarekani mda wake wote na hata alivyokuja kuwa Rais baadhi ya wanajeshi walipewa mafunzo bure kwenye chuo hicho. Norriega aliona ujiko mno kwa mahusiano yake na chuo na inasadikiwa kwamba alikua anavaa ile crest ya chuo mpaka kwenye nguo ya jeshi na hata wakati anakamatwa alikua ameivaa juu ya nguo ya jeshi.

NORRIEGA KUPATA MADARAKA

Arnulfo Arias alichaguliwa kuwa Rais mwaka 1968 baada ya kampeni za nguvu kufanyika.Baada ya kurudi Ikulu tu alianza kulibana jeshi na kuondoa baadhi ya wanajeshi kuwapeleka kwenye vizuizi vya kidiplomasia au kuwastaafisha.Torrijo na wenzake walivyoona hivyo ikabidi ikabidi wafanye mapinduzi yaliyoendelea kwa kipindi cha siku kumi na moja na hata hivyo kuliibuka tena kikundi kingine cha jeshi kikitaka na chenyewe kuchukua Nchi chini ya Martinez Norriega alikua mfuasi mzuri wa Torrijo.Baada ya kuona hivyo yule mgombea urais aliyeshindwa Arias naye aliingia ulingoni kupambana akiwa na wafuasi wake na katika hili Norriega alikua kiungo muhimu kuhakikisha wanatulizwa hawa watu haraka na ilichukua mwaka mzima kuhakikisha wanatula kabisa.Mwishoni mwa mwaka 1969 Torrijo alikua zake mapumzikoni ncini mexico na huku nyuma yalifanyika mapinduzi na yakafanikiwa na Norriega alimkabidhi Torrijo madaraka hayo pamoja na kuwa yeye hakuwepo. Kutokana na hilo Norriega alipewa promosheni na kupandishwa cheo kuwa lieutenant colonel na pamoja na hiyo aliteuliwa kuwa mkuu wa jeshi mwaka 1970 na katika muda mfupi huo wa norriega kupanda vyeo inasemakana zile tabia zake za kishenzi aliziacha na kujirekebisha kabisa.
Torrijo alitumia muda huu kuweka mkataba na wamerekani wakati huo Rais akiwa Jimmy Carter kuhusu umiliki wa panama kanal na mwaka 1999 tayari marekani walikubali kuwwachia canal hiyo.Pamoja na mkataba huo alibadili sheria za kazi na kuruhusu likizo ya uzazi pamoja na kuruhusu haki majadiliano ya pamoja kati ya mwajiri na mwajiriwa (collective bargaining right) na malipo ya ziada vilimfanya akubalike mno na wananchi pamoja na kwamba hakukuwa na uchaguzi.
Norriega alidhibitisha kwamba yeye ni mkuu wa jeshi anayejiweza na katika nafasi yake hiyo aliweza kuwaondoa na kuwaweka kizuizini wanajeshi 1300 ambao aliona ni tishio kwa usalama wa uongozi wa Torrijo. pia alihifadhi mafaili ya wanajeshisa ambao aliona yanaweza kutumika baadae kuwablackmail kuwatishia kama watataka kupigia kelele kitu chochote. Hapa ilionekana kwamba mara nyingi alikua akifanya kazi ya Torrijo na kuulinda utawala wa Torrijo.Mwandishi Frederick Kempe anaripoti kwamba Norriega alihusika na mashambulizi kadhaa ya mabomu yaliyowalenga raia wa marekani na hii ilimfanya mpaka rais Gerald Ford kushawishika kufanya makubaliano upya kuhusu panama canal mwaka 1976. pamoja na hayo huyu jamaa anasadikiwa ndio aliyeamuru mauaji ya mchungaji Hector Gallegos ambaye kazi yake kwenye vyama vya ushirika ilionekana kuwa tishio kwa serikali, Mchungaji huyu mwili wake uliripotiwa kuwa ulitupwa kutoka kwenye Helicopta na kutdumbukizwa baharini.
Ushirikiano kati ya Norriega na marekani uliimarika mno kufikia kwamba jamaa aliingizwa kwenye list ya malipo ya C.I.A. na alikua mtu wa kipaumbelekwenye kupokea malipo mwaka 1971.C.I.A. walimuona kama assert maana alikubali kuuza taarifa za kijasusi za nchi ya Cuba na baadae kuhusu serikali ya Nicaragua wakati huo ikiongozwa na Sandinista. Kuna wakati fulani ubalozi wa Panama Nchini huko Managua ulitumika na makachero wa kimarekani,ingawaje C.I.A. walitambua pia kwamba kwa wakati mmoja Norriega pia alikua akiwauzia Cuba taarifa za marekani. Wakati wa makubaliano kati ya serikali ya marekani na Panama kuhusu Panama canal serikali ya marekani iliamuru wanajeshi wafunge kwa tape eneo hilo lakini Norriega alimhonga mhusika mkuu na yeye ndio akafunga mwenyewe kwa sababu anazojua. Ingawaje baadhi ya maofisa wa C.I.A. walitaka hao waliohusika wachukuliwe hatuana aliyekua mkuu wao ambaye ni George H. W. Bush tukio hili halikuripotiwa popote sio kwenye mahakama za marekani wala kwenye jeshi na hii ilifanyika ili kulinda uhusika wa norriega usije julikana.


itaendelea.........................................
 
kiongozi shusha mzigo maana huyu mtu natamani kumjua sana nasikia nae alikua katili ila aliweza kuwa rafiki na hapo hapo adui wa marekani
 
KIFO CHA TORRIJO

huyu alikufa kwenye ajali ya ndege 31/5/1981 na ajali hiyo ilikua ya kutatanisha baada ya mapambano ya kugombania madaraka kwa muda kutokana na kile kinachosemekana kutokua na mtiririko unaoeleweka wa kimadaraka baina ya maafisa wa jeshi wa ngazi za juu Norriega alijitwalia madaraka hayo.

Alilifanyia mabadiliko jeshi la nchi hiyo na kwa kutumia misaada ya kiya kuwa kifedha kutoka marekani aliliimarisha na kulifanya kuwa la kisasa kabisa. kwa kuwa aliwapandisha vyeo haraka haraka wanajeshi waliongeza utii kwa serikli yake, hata hivyo miaka miwili baadae Norriega alijivika vyeo yeye mwenyewe kuwa colonel wa jeshi ambayo ilimuongezea nguvu kiutawala pia aliviunganisha vikosi vyote pamoja ili kuhakikisha uongozi unakua rahisi. twende taratibu kidogo aliweza tena kumrubuni mkuu wa kikosi cha panamanian armed forces Rubén Darío Paredes, aachie nafasi yake na kumuachia yeye akiwa amemuahidi kwamba atamruhusu kugombea urais wa nchi hiyo kumbuka hapa kulikua na utawala wa kijeshi hivy huo wa baada ya uchaguzi ungekua utawala wa kiraia.

Ingawaje baada ya kuchukua nafasi hiyo alimsaliti mwenzake huyo na alimkamata na kujipatia ujeneral na ukuu wa majeshi yote ya panama na ikumbukwe kwamba akiwa kiongozi wa kitengo cha intelijensia alikitumia kuwaharasi na kuwatishia wapinzani wake pamoja na vyama vya upinzani.

UCHAGUZI WA 1984

Kuliko kuwa Rais aliona awe nyuma ya pazia tu hii ikiwa ni pamoja na kuepuka yale makandokando yanayohusiana na yeye kuwa Rais. hata hivyo hakua na sera inayoeleweka ya kuwaunganisha watu wake zaidi aliwaambia tu kwamba ni uzalendo wa kijeshi kupitia chama chake cha Partido Revolucionario Democrático (PRD) kilitumiwa na Norriega kuwa chama kwa ajili ya kuwaunganisha wanajeshi. Baada ya kutwa madaraka alipitisha sheria namba 20 ambayo ilizuia nchi za kikomunisti kutumia (Panama canal) mlango bahari wa panama na hivyo iliruhusu marekani kuutumia kwa kiwango kikubwa kwa kupitishia silaha na bidhaa nyingine zinazohusu jeshi la panama. sheria pia ilizuhusu kuongezwa kwa jeshi la panama mara tatu zaidi na kulifanya lihusike kwenye shughuli nyingi ambazo hazilihusu jeshi hilo kama uhamiaji, usafirishajirailway na viwanja vya ndege.

katika kipindi hiki ndipo hasa watu wengi walisafirisha mitaji yao tunaweza kusema utoroshwaji wa mitaji kwa kuogopa kwamba inaweza kuchukuliwa na wanajeshi hao.pia alilazimisha kununua vyombo vya babari vya binafsi ili kuhakikisha anazuia ukosoaji na wamiliki waliuza ili wasije wakanyanganywa na serikali kupitia wanajeshi hao. Inasemekana kwamba wakosoaji na wapinzani wa Norriega waliteswa,kunywanywaswa na kudhalilishwakwa mfano gazeti moja binafsi la La Prensa, ndilo lililobaki binafsi ambapo wafanyakazi wake walikua wakikamatwa na kuteswa na kutishwa mara kwa mara na kuna wakati ofisi zilivamiawa na baadhi ya vitu kuharibiwa vibaya na baad ya hapo walilazimishwa kufunga kituo hicho.

mwaka 1984 Norriega aliruhusu uchaguzi wa kiraia kufanyika ila alipoona kwamba wapinzani kupitia Arnulfo Arias walipoonekana wanashinda uchaguzi kwa kishindo tena asubuhi tu mapema Norriega liamuru kusitishwa kwa uhesabuji kura na baadae kutangaza kwamba mgombea wa chama chake alishinda kwa ushindi mwembamba wa kura 1,713 dhidi ya mpinzani wake ingawaje baadhi ya vyomba vya habari huru vinasema kwamba wapinzani walishinda kwa kura zaidi ya 5000 iwapo ingefanyika kwa haki na wazi.Wamarekani walijua huu mchezo wa mjini ila waliamua kuufumbia macho.Utawala wa huyu jamaa ulizidi kuwa wa kizandiki mno hasa pale marekani ilipoonyesha kumuamini na kumtegemea zaidi kwenye kuiteketeza serikali ya Nicaragua chini ya Sandinista pamoja na kuruhusu kufanyika kwa uchaguzi alijua wazi kyuwa alikua anafanya ujanja gani katika hilo.

MAUAJI YA SPADAFORA

Hugo Spadafora alikua mwanafizikia na mwanaharakati aliyekua ametofautiana na Norriega wakati wakiwa chini ya serikali ya Torrijo. Pamoja na kwamba hakuwa mpinzani laki8 ni alikua na anatoka sana povu ndani ya chama hasa la kiukosoaji. Mwaka 1985 alimtuhumu Norriega kuwa anafanya biashara ya madawa ya kulevya naangerudi Panama kugombea uraisi akitokea Coasta Rica.Hata hivyo Norriega alihofia kupoteza uungwaji mkono kutoka kwa watu wa daraja la kati ambao walikua ndio wengi akiwa amewapata kutokana na kuwepo serikalini muda mrefu toka enzi za Torrijo. Hata hivyo Spadafora alitekwa akiwa mpakani mwa Costa arica na kuteswa, na kuuwawa na kuwekwa kwenye mfuko wa kusafirishia vifurushi baadae maiti yake iligunduliwa, ingawaje familia yake na baadhi ya wadau walishinikiza kufanyika kwa uchunguzi ila shinikizo halikuleta tija kwani Norriega akiwa ufaransa alikataza kufanyika kwa uchunguzi huo. Kifo cha Spadafora kilibadili muonekano wa Norriega kwa Marekani kwani waliona fika kwamba huyu mtu sio assert tena bali liability wale watu wa biashara wanaelewa vizuri tu hapa. majasusi wa marekani waliamini wana ushahidi wa kutosha kumweka hatiani Norriega kwa mauaji hayo. ushahidi huo unatokana na kunaswa kwa mawasilianao ya wiretap kutoka maeneo ya Chiriquí Province kwa kamanda, Luis Córdoba akisema "We have the rabid dog", na Norriega alijibu "And what does one do with a dog that has rabies?"

OPERESHENI YA MADAYA YA KLEVYA NA SILAHA

Tarehe 12|6|1986 Seymour Hersh aliandika makala ya tuhuma dhidi ya Norriega kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya na utakatishaji wa fedha .Makala hiyo ilisema kwamba Norriega amekua akijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kwa muda wa miaka ishirini katika nchi ya kolombia.Hersh alimrekodi afisa mmoja wa Ikulu ya marekani akisema kwamba kupunguza shughuli za biashara ya madawa ya kulevya kutapunguza pia usafirishaji wa madawa hayo duniani. Ripoti iliyoandaliwa na U.S. Defense Intelligence Agency ilieleza kwamba Norriega alikua na kikosi maalumu kwa ajili ya kusimamia biashara yake na kikosi hicho kilikua na wanajeshi ambao ni washiriaka wake wa karibu. Mwaka 1985 shamba la mimea ya kutengenezea madawa ya kulevya liligundulika katika mpaka kati ya kolombia na Panama, na ilionekana kwamba moja ya wahusika wa shamba hilo ni Norriega. Pamoja na hayo serikali ya washngton inaamini kwamba Norriega anasambaza silaha kwa kundi la M:19 la wapiganaji ambao walitokea Panama na kwenda cuba kabla ya kushambulia pwani ya kolombia. Kwenye majadiliano ya kitabu kimoja mwaka 1990 uongozi wa Norriega ulielezea kwamba uliiuzia serikali ya cuba pasopoti 5000 kwa ajili ya kutumika na majasusi wa nchi tya cuba, mwaka 1980 na kuendelea kujihusisha katika biashara hizo moja kwa moja kulipungua na badala yake alijihusisha na biashara halali na hili lilitumika kama sehemu ya kutakatishia fedha zilisotokana na biashara hiyo haramu. Majasusi wa kimarekani wanaamini kwamba Norriega amehifadhi fedha nyingi katika benki za ulaya zilizotokana na biashara hiyo na pia anamiliki nyumba za kuishi moja ikiwa ipo Panama na nyingine ufaransa Utajiri wake unakadiriwa kuwa kiasi cha dola millioni 772 wakati akiwa anaendelea na biashara na kati ya shillingi millioni 200 na 300 wakati akitolewa madarakani.

Barletta and Herrera

Huwezi kuzungumzia habari yoyote ya Norriega bila kuzungumzia hawa watu wawili na yaliyotokea wakati wao. Rais Barletta alitembelea jiji la New York na mmoja wa waandishi wa habari aliulizia kuhusu kifo cha Spadafora na hili swali lilimfanya aahidi kulichunguza suala hiloatakaporudi nymbani Panama. Suala la kushangaza ni kwamba alipofika tua Panama alipofika panama alikamatwa na kupelekwa makao makuu ya jeshi na kuamuriwa kujiuzulu hapa ndio unatakiwa kuelewa ni nani anatawala na nani anaongoza. Baada ya kutangaza kujiuzulu nafasi yake ilichukuliwa na makamu wake wa wakati huo ambaye ni Eric Arturo Delvalle. akiwa kama mwanafunzi wa kipindi hicho wa George Shultz Barletta alionekana mtu muhimu sana kwa marekani na kuondolewa kwake madarakani kulizorotesha sana uhusiano wa Norriega na Marekani. kipindi kifupi baada ya kifo cha Torrijo Norriega aliweza kufanya makubaliano na deputy Colonel Roberto Díaz Herrera kwamba yeye ataondoka kwenye kiti chake na mwaka 1987 na Diaz angechukua nafasi yake . Kweli muda ulipofika Norriega alifanya hivyo na cha kushangaza ni kuwa baada ya Herrera kuchukua nafasi tu alianza kumtuhumu Norriega kwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, kuvuruga uchaguzi wa 1984, kumuua Spadafora na pia Torrijo kwa bomu lililotegwa kwenye ndege yake. Habari hii ilibadilisha kabisa mtazamo wa raia wa panama ambao waliingia barabarani kuandamana kumpinga Norriega kwa malaki maana inakadiriwa zaidi ya 25% ya wananchi wa panama walishiriki maandamano hayo. Norriega bila kusita alimkamata Herrera na kumpa kwesi ya uhaini na pia waandamanaji walikiona cha mhenga mtemakuni. Seneti ya marekani ilipitisha makubaliano yaliyomtaka Norriega kujiuzulu mpaka hapo Herrera atakapohukumiwa kutokana na kesi yake aliyofunguliwa. Badala yake Norriega alituma maafisa na watumishi wa serikali kwenda kuandamana na kuweka kambi nje ya ubalozi wa marekani, marekani walichofanya ni kufutilia mbali miasaada yote ya kijeshi waliyokua wakiisaidia nchi hiyo na C.I.A. walikata mara moja mshahara wa Norriega. Bila msaada wa Marekani Panama ilishindwa kulipa madeni yake ya Nje na hivyo uchumi wa nchi hiyo ulishuka kwa 20% kwa mwaka huo.

MAHUSIANO YA C.I.A. NA MSAADA WA MAREKANI PANAMA

Norriega alikua kama kiungo muhimu cha jeshi la Nicaragua na misaada kutoka marekani kwa kipindi kirefu sana, hii ikijumuisha silaha na fedha. Pamaoja na hayo alisaidia C.I.A. kuweka kitengo cha maridhiano nchini panama na ukiachana na hilo aliweza kusaidia serikali ya Salvado kwenye kuwaondoa watu wenye mrengo wa kushoto. Pamoja na hili inasadikiwa pia kwamba Norriega alifanya mchakato wa kusaidia kikundi cha wapinzani kupata silaha na Irani mwaka 1980 ambapo silaha na fedha zilipelekwa Iran chokochoko hizi za Iran ziliitwa the Iran Contra affair. Kutokana na taarifa kutoka kwenye dayari ya Oliver Northinasemekana Norriega alimuahidi North kwamba yeye Norriega atasaidia kumuua kiongozi wa kikundi cha Sandista ili na eye North amsaidie kuimarisha uhusiano na marekani ambao ulikua umelegalega mno. Kwenye kesi ya Norriega 1991-92 norriega alikua analipwa kiasi kikubwa cha fedha. Kwa makisio inasadikika alilipwa fedha yote kama $ 320,000. Mwandishi kemp anasema ni kiasi cha $110,000 kwa mwaka wakati waandishi wengine wakisema ni $ 200,000 kwa mwaka. Inasadikiwa kwamba mambo mengi yalikua yanafahamika ila marekani ilikaa kimnya kwani waliona wataharibu aseti yao hiyo. Pia marekani walijua kwamba ikitokea mtu mwingine akiwa kiongozi hapo Panama na kuwa na nguvu kama Norriega basi hawezi kukubali jeshi la marekani kuwepo hapo wala mwingiliano uliopo. Pamoja na kujua kua Norriega alikua anahusika na biashara ya madawa ya kulevya mkurugenzi wa C.I.A.William Webster alimzungumzia norriega kama mtu muhimu kwenye mapambano dhidi ya madawa ya kulevya. Hapa ona ndugu msomaji kwamba madawa ya kulevya sio ishu ya jana wala juzi ni kitambo mno na kuna watu wamefumbiwa macho kutokana na umuhimu wao kwa muda huo ila haikua rahisi kuwaacha daima muda wao ulifika na walisogezwa kwenye vyombo vya sharia. Muda huwa suluhisho la mambo mengi sanakila jamnbo likipewa muda kila kitu kitajidhihirisha tu. Hata watoto wa simba wakizaliwa hufanana na wa mbwa ila baada ya muda ndio utajua huyu ni wa simba wala sio mbwa, na simba dume na jike wakiwa watoto unaweza wafananisha ila baada ya muda sharubu zikiota basi dume huonekana mubashara. Turudi taratibu kwenye hii habari yetu kwamba wamarekani walimchukulia Norriega kama kiungo muhimu kwenye vita ya madawa ya kulevya hasa maeneo ya kusini mwa marekani.

Katika moja ya kikao cha komitii ya masenata iliyokaa mwaka 1988 kuhusiana na masuala ya madawa ya kulevya na operesheni za kimataifa walihiytimisha kwamba tukio la General Manuel Antonio Noriega linawakilisha kufeli kwa hali ya juu kwa sera ya marekani ya mambo ya nje kwa wakati huo. Kwa kipindi chote cha mwaka 1970 mapaka miaka ya 1980, Norriega alikua anajikusanyia madaraka yote ya nchini kwake huku akicheza kwa utaalamu wa hali ya juu na sera ya marekani ya mambo ya nje. Pamoja na hayo maafisa wa C.I.A walilazimika kufumbia macho mambo maovu aliyokuwa akiyafanya kama rushwa ilitopindukia na biashara ya madawa ya kulevya hata lile la kuonekana kama mfanyabiashara maarufu wa madawa ya kulevya kwenye kundi la Medelini Cartel, ambapo kwa wafuatiliaji wa mambo ukienda kwenye historia ya mfanya biashara maarufu wa dawa za kulevya PubloEscoba utaona kundi hili lilikua chini yake. Norriega aliweza kujitengenezea himaya yake iliyojulikana kama "the hemisphere's first 'narcokleptocracy' na sehemu pekee alipoweza kutakatishia fedha zake ni Bank of Credit and Commerce International.

Mwaka 1988 kwenye kampeni za urais aliyekuwa mgombea wa chama cha Democratic mgombea Michael Dukakis alimtuhumu mgombesa kutoka Republic aliyewahi kuwa mkurugenzi wa C.I.A wakati huo akiwa makamu wa Rais George H. W. Bush, kwa mahusiano ya karibu na muuza madawa yta kulevya wa Panama Norriega. Mwandishi Kemp anaelezea kwamba 1990 marekani ilisaidia kutoa mafunzo makali kwa maafisa wa Norriega kiasi kwamba ilimfanya aweze kuitawala Panama vizuri na kuuita uhusiano huu kama "sordid marriage of convenience".

UCHAGUZI WA 1989

Mahusianao baina ya C.I.A. na marekani ulizorota kama ilivyoelezwa baada ya yote kugundulika na pamaoja na hayo kulikua pia na uuzwaji wa siri za kijasusi kwa mahasimu wa marekani, achilia mbali uuzwaji wa madawa ya kulevya. Mwandishi Hersh anasema kwamba mwaka 1986 iligundulika kwamba pamoaja na mambo mengine Norriega alikua akimuuzia Fidel Castro wa Cuba taarifa za kiintelijensia. 1988 kwa mara ya kwanza kabisa jina la Norriega lilitajwa kwenye mahakama za marekani kwa makossa ya kusafirisha na kuuza madawa ya kulevya. Baadhi ya maafisa wanadai kwamba pamoja na mambo mengine huyu mtu alikua anaijeuza Panama kama platform ya cocaine kwa ukanda wa latini America kwa ajili ya kupeleka U.S na kuruhusu fedha zinazotokana na biashara haramu ya madawa ya kulevya kuwekwa katika benki za panama. Katika mwaka huo huo kuna jaribio la kumpindua lilifanyika likiongozwa na Delvalle ila lilishindwa.

Uchaguzi wa mwezi wa tano mwaka 1989 ulitawaliwa na figisu nyingi. Vyama vya muungano vya PRD vikiongozwa na Carlos Duque ambaye ni mchapishaji wa gazeti kogwe la La Estrella de Panamá. Vyama vilivyobaki viliunganisha nguvu zao kwa kuwaweka wagombea kwa tiketi ya pamoja ambao ni Guillermo Endara, mwanachama wa chama cha Arias' Authentic Panameñista Party, pamoja na mgombea mwenza wake Ricardo Arias Calderón (hausiani na Arnulfo Arias) na Guillermo Ford.

Kutokana na chanzo cha Guillermo Sanchez, walijua kwamba Norriega ana mpango wa kuchakachua uchaguzi ila hawakuwa na ushahidi hasa kwenye uhesabuji wa kura. Walikuta ka mwanya kadogo toka kwenye katiba ya panama sheria ndogo ya uchaguzi. walijiunga na kanisa katoliki na kutengeneza vituo 4,000 vya kujumlisha matokeo kutoka kwenye vituo kabla hayajafika kwenye kituo kikuu cha wilaya. Norriega alitumia karatasi feki za matokeo akishirikiana na watu wake toka kwenye vituo vyao vya kufanyia tally ila walichelewa maana kila wakitaka kuchakachua walikuta matokea halisi na halali yalishafika. Ilionekana dhahiri kwamba kwenye matokeo halali ya uchaguzi waliyokua wanatoa watu wa upinzania kupitia mgombea wao Endara alikua anashinda kwa kishindo kikubwa zaidi ya hata kile cha uchaguzi uliopita 1984 akiwa mbele ya mpinzani wake kwa umbali wa kura zaidi ya tatu kwa moja. Badala ya kutangaza matokeo Norriega alifuta matokeo (hapa nakumbuka mbali kweli) akidai kwamba uchaguzi uliingiliwa na nchi za nje na kumtangaza Deque kuwa mshindi wa uchaguzi huo ambaye ndiye alikua mshirika wake. Aliyewahi kuwa Rais wa marekani Jimmy Carter, alikataa kuwa hakuna nchi iliyoingilia uchaguzi huo ,wakati huo yeye alikua muangalizi wa uchaguzi toka nje. Norriega aliendelea kudai uchaguzi umegubikwa na udanganyifu wakiwa wanakubaliana pamoja na Bishop Marcos G. McGrath. Siku iliyofuata baada ya uchaguzi Deque alikua anajua ameshindwa vibaya na hivyo kukataa kuendelea na mchakato. Endara, Arias Calderón, na Ford wao waliingia mjini kwa mbwembwe kuelekea sehemu iliko ikulu ya Nchi hiyo kwa msafara wa magari, mara walivamiwa na kikosi cha kijeshi cha Norriega. Arias Calderón alilindwa na kikosi hicho ila hawa wengine walipewa mkong’oto wa nguvu na picha za ford zilitolewa kwenye magazeti ya siku iliyofuata akionekana na shati lake likipepea kama Hamo Rapa alivyoona bastola ila yeye shati lililowa damu (guayabera shirt covered in blood) picha zilisambaa dunia nzima. Hata hivyo Norriega akamuweka jamaa yake wa karibu Francisco Rodríguez kuwa kaimu Rais baada ya mwaka 1984 na 89 ingawaje Marekani ilimtambua Endara kama Rais mpya. Hizi figisu za Norriega za kuzuia matokeo ya uchaguzi yalisababisha kutokee jaribio lingine la kupindua serikali mwaka 1989. Baadhi ya maafisa waandamizi chini ya Norriega walimpinga waziwazi ila mapinduzi yalizuilika kiraisi na maafisa watiifu kwa Jenerali Norriega.Baada ya jaribio hilo alijitangaza mwenyewe kwamba yeye ndio kiongozi mkuu wa nchi hiyo na hamna kenge yeyote kuleta za kuleta, wale waliokua wamefanya jaribio la kutaka kumpinduo walipelekwa kwenye kambi moja ya kijeshi nje ya jiji la panma na kuteswa na kuuwawa.

KUELEKEA KWENYE VITA NA MAREKANI

Tarehe 15/12/1989 chama kinachotawala na kumuunga mkono Norriega kilitangaza hali ya hatari ya vita kati ya Panama na U.S. Pia ilimusimika rasmi Norrega kuwa ndio Mkurugenzi mkuu wa serikali ya Panama kwenye masuala yote. Pia Norriega alikazia maneno hayo akisema kwamba hali hiyo imekuja baada ya matendo ya marekani yanayokinzana nae na sio hali ya hatari kwa panama na raia wake. Majeshi ya Panama yanatajwa kuwaharasi wanajeshi wa marekani pamoja na raia wake waliokua panama mara kwa mara. Matukio matatu yaliyotokea karibu na kipindi cha uvamizi wa marekani Panama na kutajwa na Rais wa marekani wa wakati huo George H. W. Bush kuwa ni chanzo cha uvamizi ni pamoja natukio lililotokea 16/12/1989 ambapo raia wanne wa marekani wakiwa katika gari yao wakipita karibu na makao makuu ya chama cha PDF likiongozwa na Norriega mtaa wa El Chorrillo karibu kabisa na jiji la Panama depatimenti ya ulinzi ya marekani inasema kwamba raia hao hawakuwa na silaha yoyote na tena kwenye gari binafsi na walijitahidi kutoka kwenye eneo la tukio bila kuleta matatizo . Lakini walizungukwa na kundi la raia na wanajeshi wa jeshi la nchi hiyo. Robert Paz aliyekua mwanajeshi wa jeshi la maji wa marekani alipigwa risasi na kufa papo hapo. Pamoja na hayo mmarekani mmoja na mpenzi wake walioshuhudia tukio hilo walichukuliwa na kwenda kuteswa na kuwa harasi.

MAREKANI WAITWANGA PANAMA

Tarehe 20/12/1989 marekani waliamua kuivamia Panama. Ingawaje mauaji ya raia wake ambaye pia alikua mwanajeshi wa jeshi la maji ilikua pia nia sababu lakini vita hii ilishaandaliwa kwa kipindi kirefu tayari. Inasadikiwa kwamba hii ndio ilikua vita kali zaidi toka baada ya uvamizi wa Vietinamu na ilikua na wanajeshi 27,000 na ndege 300. Serikali ya Bushi ilikua imepanga mashambulio mepesi tu kwa kutumia silaha za kawaida ila baadae ilionekana kwamba haifai watumie mashine za kisasa ili kufanya shambulio lenye tija. Jeshi la marekani lilitageti gari ya Norriega binafsi na inaelezewa kwamba baadhi ya nyumba katika jiji la Panama ziliharibiwa kutokana na mabomu ya jeshi la marekani. Colonel Luis del Cid aliondoka na wanajeshi wakikosi chake na kukimbilia milimani maeneo ya nje ya jiji la David baada ya kutega mabomu ya ardhini kwenye uwanja wa ndege. Ingawaje inasemekana pia hii ilikua moja ya njia za kufanya makubaliano na jeshi la marekani pia Cid alionelea kwamba hawawezi kupigana na marekani na hivyo kufanya mazungumzo ya kujisalimisha. Inasadikiwa wanajeshi wa marekani 23 mpaka 60 walikufa na 300 mpaka 845 walijeruhiwa kwenye uvamizi huo. Raia wengi waliuwawa kwenye uvamizi huo na mpaka leo haijulikani idadi kamili ya raia waliopoteza maisha. Serikali ya marekani iliripoti vofo 250 vya raia ila waangalizi wengine wanasema ilikua ni kati ya vifo 3000. 29/12/1989 baraza la usalama la umoja wa mataifa lililaani uvamizi huo baada ya kukutana na kuzungumzia uvamizi huo kwa kusema ni kitendo cha kuvunja sheria za kimataifa. Inasemekana baada ya huu uvamizi kulitokea vitendo vingi vya wizi ambapo inakadiriwa kwamba polisi walishindwa kufanya kazi yao. Hata hivyo kiasi cha wizi kinakadiriwa kuwa kiliharibu karibu nusu bilioni fedha za kimarekani ambapo baadae marekani ilijazilipa fedha hizo kwa ajili ya mategenezo. Asilimia 92 ya wananchi waliwaunga mkono wamarekani na 76% walitamani marekani ingevamia wakati wa jaribio la mapinduzi ili iwe rahisi kupindua serikali iliyokuwepo. Mwanaharakati Barbara Trent anasema kwamba katika utafiti uliofanyika kwa wananchi wanaoongea kingereza wengi walitamani kuisapoti U.S.

KUKAMATWA KWA GENERAL NORRIEGA

Tarehe 3/1/1990 Gen. Manuel Noriega alikamatwa na jeshi la marekani kiteno cha kupambana na madawa ya kulevya (Drug Enforcement Administration)(DEA). taarifa hizi zipo kwenye makala inayoelezea operesheni Nifty Package.Gen. alijaribu kutumia njia nyingi mno za kujibadilisha ili asitambuliwe na kukamatwa na jeshi la marekani, ikiwemo kubadili muonekano, sauti na mengine ya aina hiyo. Ndani ya siku kumi baada ya kuvamiwa kwa Panama aklijaribu kutoa vitisho kama vile kwenda msituni huko na kuanzisha vita ya msituna ila baada ya kufikiria kujificha kwenye balozi wa Cuba au Nicaragua na kukuta zote zimezingirwa na jeshi la marekani alikimbilia kwenye eneo la kanisa (ambao ni ubalozi wa Vatikani) ambapo kulikua na makubaliano kwamba ubalozi huo hautavamiwa. Ndani ya siku tano alijificha hapo akisoma Biblia kama mfuasi wa mchungaji kibwetele akiomba mungu moto usimuwakie enzi kanisa lile lilipoteketezwa ila moto uliendelea kuwawakia. Ubalozi huu wa Vatikani ulimuhifadhi muda wote huo ambapo majeshi ya marekani yaliweka kambi nje kwenye eneo la wazi ambalo waliligeuza kuwa sehemu ya kutua Helikopta zao na huku wakila mziki mkubwa kusheherekea ushindi ambapo huu mziki ulimshinda Norriega pamoja na kwamba alikua ndani. Ingawaje ilipofika tarehe 3 /1/1990 aliamua kujisalimisha na kupelekwa marekani kwenye kesi yake.

upload_2017-8-2_14-24-20.png




Kesi yake ya nchini marekani

Mwezi wa nne mwaka 1992 kwa mara ya kwanza Norriega alisimamishwa kizimbani huko Miami, Florida marekani kwa makosa nane ikiwemo kupanga njama za kufanya biashara ya madawa ya kulevya, kufanya biashara hiyo na utakatishaji wa fedha. Hapa ndio yuel “muhenga aliyesema kila kitu kina mbabe wake” alianza kukumbukwa. Kwa ubabe wake alitaka kujitetea mwenyewe bila wakili kwa kile kinachodhaniwa kwamba alitaka kumwaga ugali baada ya mboga kumwagwa na US wenyewe kwa kusema alikua anatumika na C.I.A. Serikali ilakataa kutoa siri za kwamba norriega liwahi kulipwa, kwa kuwa taarifa hizo zilikua siri. Ingawaje ilikua ngumu kumziba mdomo norriega kwani aliongea. Wakati wao marekani walisema walimlipa kiasi cha $220,000 yeye alisema ni zaidi ya $10,000,000 na aliomba aruhusiwe kusema kazi aliyokua amepewa kufanya na marekani. Hata hivyo walitupilia mbali madai hayo ya Norriega kwamba hayahusiani na kesi ya msingi na pamoja na hayo shahidi namba moja kwenye kesi hiyo alikua Floyd Carlton ambaye aliwahi kusafirisha mzigo wa unga wa norriega kupitia bahari.

Taarifa ambazo zilitupiliwa mbali na mahakama hiyo ni pamoja na madai ya ukaribu wake na afisa mmoja wa CIA ambaye alitambulika kama Oliver North na kukutana kwake na George H. W. Bush vyote hivi vilitupiliwa mbali. Baada ya kesi kuisha alikata rufaa kwenye mahakama kuu ya rufaa, na hata hivyo mahakama haikubadili hukumu ingawaje ilisaemea yale malipo aliyolipwa norriega kwamba yana maslhi kwa nchi hivyo hayana shida na sheria za nchi hiyo. Pamoja na jitihada hizi zote Norriega ilipofika 16/09/1992 alihukumiwa kifungo cha miaka 40 jela na baadae ikapunguzwa kuwa 30.


Kabla hajaaanza rasmi kutumikia kifungo chake alipelekwa mahabusu ya Federal Correctional Institution, Miami, in Dade County, Florida na hapa alipewa kitambulisho namba 38699-079 nasehemu alipokua akishikiliwa palikua sehemu nzuri tu kiasi cha kuwa na jina la utani la "presidential suite" ndani ya gereza hilo. Kitokana na kifungu namba 15 cha sheria za kimataifa baraza lililokaa Geniva (Under Article 85 of the Third Geneva Convention) Norriega alichukuliwa kama mfungwa wa kivita achilia mbali madai mengine yaliyopelekea kukamatwa kwake ikiwamo biashara haramu ya madawa ya kulevya. Kwa hali hiyo inamaana kwamba huyu mfungwa alikua na selo yake peke yake yenye vifaa vya umeme pamoja na vifaa vya kufanyia mazoezi. Inasemekana kwamba alikua anatembelewa na mchungaji wa kilokole kwani alidai kuwa alikua ameokoa. 15/5/1990 norriega alitembelewa na mtumishi wa mungu mwenye asili ya hispania ambaye pia alishawahi kuwa wakili Clift Brannon akiwa na mtafasiri wa kihispaniola, Rudy Hernandez, waliruhusiwa kukaa na Norriega kwa masaa sita ambapo Norriega alimwandikia Brannon barua ambayo naiweka hapa kwa lugha ya malkia kama ilivyo:


“On completing the spiritual sessions that you as a messenger of the Word of God brought to my heart, even to my area of confinement as Prisoner of War of the United States, I feel the necessity of adding something more to what I was able to say to you as we parted. The evening sessions of May 15 and 16 with you and Rudy Hernandez along with the Christian explanation and guidance were for me the first day of a dream, a revelation. I can tell you with great strength and inspiration that receiving our Lord Jesus Christ as Savior guided by you, was an emotional event. The hours flew by without my being aware. I could have desired that they continue forever, but there was no time nor space. Thank you for your time. Thank you for your human warmth, for your constant and permanent spiritual strength brought to bear on my mind and soul. – With great affection, Manuel A. “


Kifungo cha Norriega kilipunguzwa tena toka miaka 30 jela mpaka miaka 17 kutokana na kuwa na muendelezo wa kuonyesha tabia nzuri alipokua huko. Nafikiri hii ilichangiwa na selo yake ambayo ilikua ya hadhi ya Rais hivyo hata kukaa hapo tabia ingebadilika tu. Hivyo na sisi tujitahidi tuwe na jela nzuri zenye hadhi ila watu waonyeshe tabia nzuri, ingawaje ikiwa na TV kubwa na kiyoyozi vijana watatamani kuendelea kukaa huko badala ya kuondoka hata baada ya kumaliza vifungo vyao. Hivyo kifungo chake kiliisha 9/9/2007.


KESI YAKE YA UFARANSA

Serikali ya ufaransa iliomba ikabithiwe Norriega kwa kuwa alikua na kesi ya utakatishaji fedha kwa nchi hiyo mwaka 1999. Serikali ya ufaransa ilidai kwamba Norriega alitakatisha kiasi cha $ milioni 3 zilizopatikana kwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya kwa kunuinulia nyumba mjini paris. Hata hivyo alihukumiwa bila kuwepo mahakamanio ingawaje sheria za ufaransa zinamtaka mtuhumiwa kuhudhuria mahakamani atakapopatikana hivyo kesi yake ilisikilizwa upya. Alihukumiwa kifungo cha miaka kumi jela. Mwezi wa nane mwaka 2007 serikali ya marekani ilimkabithi kwa serikali ya ufaransa na baada ya kumaliza kifungo chake huko. Pia huko panama walimhukumu kifungo cha muda mrefu bila yeye mwenyewe kuwepo mahakamani kwa makosa ya kutesa binadamu na mauaji, pia kukiuka haki za binadamu. Pamoja na mambo mengine ufaransa ilisema isingempa heshima ya kuwa mfungwa wa kivita. Ingwaje serikali ya panama ilimuhukumu kwa kosa la mauaji mwaka 1995 paoja na kwamba yeye hakuwa mahakamani alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.

20/2/2010, mwanaseheria wa Norriega alifanya makubalianao na serikali ya markani ili kuzuia mteja wake asipelekwe ufaransa ingawaje mahakama ya marekani ilikataa kusikiliza ombi lake. Mwanasheria huyo alikua na matumaini kwamba mahakama italipa kipaumbele ombi lake hilo lakini lilitupiliwa mbali. Baada ya kutupiliwa mbal kwa ombi la mwanasheria huyo 22/3/2010 kinga ya kutokusafirishwa iliondolewa na kumfanya Hilary Clintoni akiwa secretary of state akasaini hati ya makubaliano ya kumpeleka ufaransa. 26/4/2010 Norriega alisafirishwa kwenda ufaransa ingawaje mwanasehria wake alikua kashatangulia kwa ajili ya kufanya mazungumzo na serikali ya ufaransa. Hata hivyo Norriega alipelekwa gereza ambalo mwanasheria wake alilalamika kwamba halikua na hadhi ya mtu kama huyo na kwa umri wake isingefaa pia, bila mafanikio serikali ya ufaransa haikumpa renki ya kuwa mfungwa wa kivita hivyo alibaki hapo hapo .7/72010 wakati sisi tukisheherekea sikukuu ya sabasaba yeye Noriega alikua akipokea hukumu yake ya miaka saba jela na hata hivyu nyumba aliyokua amenunua ya thamani ya euro 2.3 millioni au $ 3.6 ilitaifishwa. Ikumbukwe kwamba jaji alikua akifikiria kifungo cha miaka kumi ila akaona sio sahihi.


MARADHI NA KIFO CHA JENERALI NORRIEGA



Ndugu msomaji kama tulikua pamoja toka mwanzo utakumbuka kwamba kuna makosa bado alisomewa kule nyumbani pamoja na kutokuwepo kwake mahakamani lakini ilimlazimu kutumiokia kifungo. Serikali ya ufaransa ilitaka kujitoa wasiwasi kwamba kweli Norriega anahukumiwa ndiopo iruhusu nchi nyingine kumchukua hivyo baada ya hukumu mwaka 2011 alikabidhiwa kwa serikali ya Panama na huko alipelekwa kwenye gereza la El Renacer kutumikia kifungo chake cha miaka 20. Ambapo mwaka 2012 alitolewa gerezani na kupelekwa katika hospital ya St tomaskwa kuwa na shinikizo la damu na hata hivyo alikutwa na uvimbe kwenye ubongo mwaka 2012.

2017 alihamishiwa kwenye kifungo cha nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya kumfanyia upasuaji wa kuondoa uvimbe huo. mwezi wa tatu 2017 alipata matatizo makubwa kwenye ubongo wakati wa upasuaji kuondoa uvimbe huo ambapoalibaki kwenye hali mbaya sana.

Kama ilivyo ada haina mbabe haina mtukutu wal mtukufu ilipotimu muda wa Israel 29/5/2017 akiwa na umri wa miaka 83 shujaa na Jenerali alitangazwa amekufa na Rais wa wakati huo wa nchi ya panama Juan Carlos Varela tena kupitia akaunti yake ya twita. Watoto wake wa kike pamoja na ndugu walimzika kwa heshima zote R.I.P.



PICHA YA NORRIEGA KWENYE TAIFA LA PANAMA

Baadhi ya watu hufikiri hufikiri Norriega ni dicteta na wengine humuona kama shujaa wa wakati huo aliyetumia mbinu kuwa mwajiriwa wa CIA na kujipatia fedha kupitia biashara haramu ya madawa ya kulevya, Pamoja na kuwa na nguvu za kiutawala katika nchi hiyo ya Panama kwa kipindi chote hicho. Wengine humuita shujaa kama mimi nilivyomuita hapo juu kama unanifuta kwa makini ndugu msomaji. Makala moja ya gazeti la The Atlantic ilimuelezea Norriegana kifo chake kwa kumfananisha na Castro au Augustino Pinocheti walisema kwamba wakati Castro alikua adui na Pinochet rafiki yeye,Norriega aliweza kuwa adua na rafiki kwa wakati mmoja. Wenyewe wamuita mjanja wa wamarekani katika ukanda wa marekani ya kusini walimjenga wenyewe wakamlea na baadae wakamuondoa. Pamoja na kumuondoa huyu muuza madawa ya kulevya bado waliendelea wengine na hichi ndicho kinatafsiriwa kama kushindwa kwa sera za marekani huko marekani ya kusini.

Norriega alikua anajiita El man na wakati fulani alijiita pineple face. Alionekana mtu wa masuala ya kishirikina pia kwani alipokamatwa alikutwa na baadhi ya viotu talsman vinavyooonyesha nae ni mdau wa mambo ya kisumbawanga hivi.

Mwisho 2/8/2017
J.C.Simba
 
Back
Top Bottom