Mfahamu Geoffrey Mosiria, Magufuli wa Jiji la Nairobi

Mfahamu Geoffrey Mosiria, Magufuli wa Jiji la Nairobi

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Hivi karibuni ameibuka mtu mmoja nchini Kenya anayefahamika kama Geoffrey Mosiria. Huyu ni kiongozi wa Serikali ya Kaunti ya Nairobi ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na namna anavyotekeleza majukumu yake kwa vitendo, jambo ambalo wananchi wengi wanaona ni tofauti na baadhi ya viongozi wengine.

images (16).jpeg


Geoffrey Mosiria ni nani? Huyu ni Afisa Mkuu (Chief Officer) anayesimamia Idara ya Ushirikishwaji wa Wananchi na Huduma kwa Wateja (Citizen Engagement and Customer Service) katika Kaunti ya Nairobi.

Ameonekana kupendwa sana mitandaoni kutokana na mtindo wake wa kushuka moja kwa moja mitaani na kushughulikia kero za wananchi, hasa zinazohusiana na mazingira, usafi wa jiji, changamoto za makundi yaliyo katika mazingira magumu kama machokoraa, pamoja na watu wanaokabiliwa na utegemezi wa dawa za kulevya, akishirikiana na mamlaka husika kuwasaidia kurejea katika maisha ya kawaida.

Hivi karibuni alijikuta katika mvutano baada ya kugundua kuwa nyumba moja jijini Nairobi ilikuwa ikimwaga maji taka ya chooni katika mitaro ya maeneo ya makazi. Tukio hilo lilizua mabishano baada ya mwenye nyumba kupinga hatua zilizochukuliwa, huku baadhi ya kauli zilizotolewa zikizua mjadala mkubwa kuhusu jamii ya Wasomali na suala la uwajibikaji wa usafi wa mazingira.

Pamoja na mijadala hiyo, Geoffrey Mosiria ameendelea kupata umaarufu kutokana na kujitokeza kwake mara kwa mara katika maeneo yenye changamoto na kushughulikia matatizo yanayowagusa wananchi moja kwa moja. Wakenya wengi wameanza kumwona kama kiongozi anayefanya kazi kwa vitendo, huku baadhi yao wakianza hata kutoa maoni kuwa anaweza kuwa na nafasi kubwa zaidi katika uongozi wa taifa siku zijazo.

Mtazamo wake wa kuwa karibu na wananchi, kupambana na changamoto za kila siku na kuonyesha uwajibikaji katika kazi yake umeongeza ushawishi wake mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kama Tiktok na kumfanya azidi kufuatiliwa na wananchi wengi.


View: https://vt.tiktok.com/ZS4QoXEah/
 
Huyu jamaa alikuwa mazingira na alisumbua sana Jiji Hilo haswa haswa Night clubs za Nairobi, Ni uchungu sana
 
Ila pia nimpende publicity ndio mana Kila wakati anakuwa na camera
Publicity na camera ni kama evidence endapo itatokea shida

Mfano unakuta kuna wakati anakabiliana na wavunja sheria, ambao wanataka kugeuza kibano hili yeye ndio aonekane mwenye makosa, kukiwa na evidence ya tukio kwa video ni rahisi ku-defend

Pili video ni kama motisha kwa wengine, unaweza kuambukiza uwajibikaji kwa watu wengine kupitia video... mfano watu wakiona video zake za watu wasiotumia madaraja ya juu kuvuka barabara, watajua kumbe ni makosa.

Publicity kwa dunia ya teknolojia ni kitu cha kawaida as long as uvungi au hau-feki uchapa kazi wako... Magufuli pia alipata Publicity baada ya clip zake kuwa zinaangaliwa
 
Back
Top Bottom