Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Habari ya uzima WanaJF; pole kwa wagonjwa na walio na afya muendelee kuwa afya njema zaidi. Kama ilivyo Kawaida yangu kuleta nyuzi au makala za kuongezeana maarifa kwenye mambo mbalimbali. Hivyo leo Naomba nilete kwenu uzi huu unaomhusu mtu maarufu katika taaluma wa kuleta ufafanuzi wa masuala ya kiroho pamoja na mambo ya Giza.
NB: Sina dhamira yoyote ya kumbadilisha mtu Imani yake kwa kile nitakachokiweka humu; na endapo ilitokea hivyo Naomba niombe samahani sana mwanzoni.
Tarehe 17 mwezi wa Januari Mwaka 1881, Dunia ilipata nafasi ya kushuhudia uzazi wa Harry Price. Muingereza aliyekuwa na taaluma kadha wa kadha; akiwa ni mtafiti wa masuala ya mizimu pamoja na mizuka ndani ya nyumba mbalimbali za wakazi wa Uingereza. Lakini alikuwa ni mshauri kwenye kesi mbalimbali za masuala hayo.
Alipata elimu ya awali katika shule ya Waller Road Infants School Kisha alienda kwenye shule ya Haberdashers' Aske's Hatcham Boys School. Akiwa na Miaka 15 alianzisha kikundi cha Carlton Dramatic Society ambacho kilijihusisha na sanaa za maigizo. Humu Harry akiwa mtoto aliandika visa vingi ikiwemo; Kisa chake cha kushuhudia shughuli za kimangara kwenye Nyumba moja iliyoko Shropshire.
Bwana Mkubwa Prive alidai kuwa alianza kuona vivuli vya watu usiku; Vivyo hivyo akiwa amelala aliweza kuona viumbe mbalimbali ambao hakuweza kuwatambua wakizunguka chumbani mwake. Vyote hivi alivishuhudia akiwa na Miaka 15 tu.
Alipofikisha Miaka 20 aliona kuna haja ya kuwaumbua wale watu wapigaji, mfano; waongo pamoja na watapeli ambao hutumia picha pamoja na maelezo ya kitapeli ili kujenga hofu kwa jamii. Alitumia nguvu na muda mwingi akifanya utafiti juu ya watapeli hao. Jambo ambalo kiukweli lilizaa matunda na kuanza kupata maadui wengi tu.
Ili kulinda taswira yake ilimpasa kubadilisha taarifa za maisha yake mwanzoni pamoja na za familia yake. Alidai kuwa alikuwa ni mtoto wa familia ya kitajiri kutoka Shropshire Ingawa taarifa sahihi ni kuwa New Cross kwenye familia ya Baba aliyekuwa akiuza karatasi kwa ajili ya barua.
Mwaka 1925 Price alifungua maabara maalumu Kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina kuhusu kesi zote zinazotolewa na watu kuhusu masuala ya kiimani. Lakini marafiki zake waliokuwa ni wapigaji wa pesa kupitia uongo au utapeli kwa watu katika matamasha au maonesho. Hivyo walibadilika na kuwa maadui zake mpaka kufa kwake. Huyu Bwana ilikuwa ni ngumu sana kumuamini mtu tu kwa sababu eti ametokewa na kitu au amesikia sauti ya ajabu. Mpaka afanye udadisi wa kina.
Price alifanyia utafiti tuhuma zote kwa usawa na kama ilikuwa na ukweli basi alionesha kuwa Ina ukweli Ingawa tuhuma nyingi hazikuwa na ukweli na zilikuwa na malengo ya upigaji wa pesa tu na umaarufu.
Mwaka 1920 Bwana Mkubwa Harry Price alijiunga na Chama cha Utafiti wa Masuala yenye Utata (Society for Psychical Research) na alitumia ujuzi wake wa mazingaombwe kuwaumbua watu waongo na watapeli.
Alikuwa mwanachama wa vyema vingi tu mfano; Magic Circle, National Laboratory of Psychical Research, American Society for Psychical Research, University of London Council for Psychical Investigation pamoja na The Ghost Club.
Tarehe 29 Machi 1948 Price alipatwa na shambulio la ghafla la moyo na kufariki nyumbani kwake huko Pulborough, Magharibi mwa Sussex akiwa na Miaka 67.
Makala zake pamoja na tafiti zake zilihamishiwa kwenda kwenye chuo kikuu cha Londo kati ya mwaka 1976 na 1977 na Mjane wa Harry Price.
Mpaka anafariki alikuwa amesaidia watu wengi sana na kujipatia maadui wengi ambao aliwaumbua.
Nasaha kubwa pamoja na Imani ya Bwana Harry Price ni kuwa sio kila tukio linamahusiano na upande wa Pili yaani mashetani, mapepo au roho chafu hivyo inapaswa mtu kuwa makini na ikiwezekana fanya utafiti na udadisi wa kina.
Moja kati ya picha bandia iliyofanyiwa utafiti na Harry Price.
Naomba niishie Hapo wanajukwaa. Mpaka Wakati Mwingine tena.
Asante sana @Mshana Jr @Lumumba @Madame B na wengine.