Mfahamu Hussein Shekilango, aliyepewa barabara Dar (Bamaga - Urafiki) kutambua mchango wake kwa Taifa

Mfahamu Hussein Shekilango, aliyepewa barabara Dar (Bamaga - Urafiki) kutambua mchango wake kwa Taifa

Kumbe inaelekea siku za nyuma mpaka sehemu, barabara, jengo kupewa jina la mtu kulikuwa na maana kwa kujitolea kwa ajili ya taifa. Je, hii inafanyika hivyo siku hizi?
Zamai ilikuwa ngumu sana kunadili jina la eneo au barabara. Hii barabara ya nyerere ilikuwa Pugu na uwanja ulibaki kuitwa wa dsm mpaka alipkufa ili wapate justifcation ya majina yso kutumika. Mtu barabara imejengwa kwa kodi halafu unataka kujpata umaarufu. Nchi nyingine barabara zina namba N 1 N2 nk
 
Kumbe inaelekea siku za nyuma mpaka sehemu, barabara, jengo kupewa jina la mtu kulikuwa na maana kwa kujitolea kwa ajili ya taifa. Je, hii inafanyika hivyo siku hizi?

Ocean Road imekabidhiwa Obama kama shukran ya kuitembelea nchi yetu. Old Bagamoyo road ishabatizwa Mwai Kibaki. Siku hizi rair wa nje akija tunamzawadia barabara.

Usisahau JK na Mkapa bado hawajakabidhiwa barabara. Wao bado wanatesa na madaraja tu.
 
Hivi Asprin, Kikwete nae akifika kenya au Marekani anakabidhiwa?
 
Last edited by a moderator:
Hivi kuna yeyote amewahi kujiuliza Shekilango ni nani mpaka barabara kubwa jijini DSM ikapewa jina lake?

Naomba mwenye historia na wasifu wa Shekilango atuwekee. Naamini siko peke yangu ambaye hatuna taarifa zake.

Hussein Shekilango alikuwa Waziri wa Nchi katika OFISI ya WAZIRI MKUU; alipata ajali ya NDEGE huko UGANDA May 1980


*** SOMA habari chini utaelewa kwanini Hiyo Barabara ilipewa JINA LAKE


The Victoria Advocate - Google News Archive Search
 
Hivi kuna yeyote amewahi kujiuliza Shekilango ni nani mpaka barabara kubwa jijini DSM ikapewa jina lake?

Naomba mwenye historia na wasifu wa Shekilango atuwekee. Naamini siko peke yangu ambaye hatuna taarifa zake.

Aliwahi kuwa rdd iringa na baadae waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu. Mhe Shekilango alifariki kwa ajali ya ndege.
 
Mhh! Mkuu the Boss ninavyojua mimi kwa lugha ya kisambaa, neno SHE maana yake ni baba fulani mfano She-kilango
yaani Baba Kilango, Shelukindo baba lukindo,Shemahonge baba mahonge, Shekiondo babakoindo,Shekifu baba kifu, Shemboko baba mboko nk. kama ilivyo kwa wapare Se maana baba fulani mfano senkoro baba nkoro, Senkondo baba nkondo, Sekione baba kione n.k.
 
hata mimi nimeshawahi kusikia hizo habari za zuberi, sijui alikuwa ni nani. au ndo kwenye hiyo njia yakutokea hadi mapango ya amboni nini? nilienda amboni tukaambiwa kuna njia ya chini kwa chini kutokea arusha.

Nasikia huyo Zuberi aliliwa na Simba,ukabaki mguu tu,na huo mguu ulikutwa eneo lile,ndo maana pakaitwa mguu wa Zuberi!
 
Na ni msambaa wa Lushoto kijiji kinaitwa kialilo, makazi yake bado yapo mpaka leo.
 
Watu wa zamani mjini wote wanafahamu huyu alikuwa katika baraza la mawaziri miaka ya themanini alifariki kwa ajali ya ndege ndogo na hiyo ni kumbukumbu, ukitaka kujua zaid mtoto wake tall hivi anakaa hapa kuwait-mbezi tankibovu kwa juu kidogo mtafute kama inakukera au unataka kujua zaidi.
 
JE WAJUA?

HUSSEIN RAMADHANI SHEKILANGO, SHUJAA ALIYEKUFA AKIIJENGA UGANDA

Jijini Dar es salaam kuna Barabara Mashuhuri kama 'Shekilango Road', ikianzia maungio ya Barabara ya Morogoro eneo la Nyumba za NHC mkabala na Kiwanda cha Urafiki, ikipitia Mitaa yote ya Sinza na kuishia Maungio ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kituo cha Bamaga.

Ni watanzania wachache wajuao kuwa Barabara hiyo ya Shekilango imepewa jina Maalum kwaajili ya heshima ya Ndugu Hussein Ramadhani Shekilango, aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, akishughulika zaidi na mambo ya Utawala, wakati wa Uongozi wa Rais Julius Nyerere na Makamo wake Aboud Jumbe Mwinyi.

Hussein Shekilango alichaguliwa na Wananchi wa kwao kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Jimbo la Korogwe Mjini, Mkoani Tanga katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975, akiachia nafasi yake ya Zamani ya Meneja Mkuu wa Shirika la Usagishaji Nchini (NATIONAL MILLING CORPORATION).

Mwaka huo huo akachaguliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Utawala) akiwa chini ya Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu, ndugu Rashid Mfaume Kawawa.

Mwaka 1977 yalifanyika Mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri Nchini, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kulinda Taifa, Ndugu Edward Moringe Sokoine aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu akichukua nafasi ya Kawawa, Shekilango akabakishwa katika nafasi yake lakini akiwa na bosi mpya.

MATATIZO YA UGANDA

Mara baada ya Mapambano ya Vita vya Kagera, Mwanzoni mwa mwaka 1979 Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania vilifanikiwa kumng'oa Madarakani Dikteta Amin wa Uganda na kumpachika Ndugu Yusufu Lule kama Rais wa Muda wa Taifa hilo Jirani. Lule hakudumu sana madarakani kwa kuwa mwezi Juni, 1979 naye aling'olewa madarakani kwa kutofautiana na Baraza la Ushauri la Taifa la Nchi hiyo juu ya uteuzi wa nafasi za Mawaziri, na nafasi yake kuchukuliwa na Ngudu Godfrey Binaisa.

Miezi kadhaa baada ya kuchukua madaraka kwa Binaisa katika Serikali ya Uganda bado mambo ya kuendesha nchi hiyo hayakuonekana kwenda vizuri, Changamoto za kujenga upya nchi hiyo iliyoharibiwa na vita zilikuwa kubwa, huku Jeshi jipya la nchi hiyo likiwa na kashfa ya kufanya ukatili kwa wananchi na pia kushiriki kwenye uhalifu na uporaji. Ili kuimarisha mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo ilimbidi Rais Nyerere ambaye bado vikosi vya Jeshi lake vilikuwa havijaondoka Uganda, ampeleke Waziri Hussein Ramadhani Shekilango kwenda kusaidia mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo.

Mwezi Mei, 1980 ilizuka sintofahamu kubwa katika Utawala wa Uganda, Rais Godfrey Binaisa alimuondoa Jeshini Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Nchi hiyo (zamani akiitwa Chief of Staff) Ndugu David Oyite Ojok na kumteua kuwa Balozi wa Uganda Nchini Algeria, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni nidhamu mbaya ya Jeshi la nchi hiyo hasa kwenye masuala ya Ukatili kwa wananchi na Uporaji.

Uamuzi huo wa Rais Binaisa haukumfurahisha Kiongozi huyo Namba 2 wa Jeshi la Nchi hiyo, hivyo alikataa Uteuzi mpya, na wanajeshi waliokuwa Watiifu kwake wakatangaza kumuondoa Madarakani Rais Binaisa aliyekuwa akilindwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika Hekalu la Rais la Entebbe. Misururu mirefu ya Magari ikaonekana katika Jiji la Kamapala, ambapo Wanajeshi watiifu kwa David Ojok walikuwa wakiyapekuwa magari yote yaliyokuwa yakitoka na kuingia ndani ya jiji hilo ili kuhakikisha hakuna silaha, huku pia wakikiteka Kituo cha Redio cha Taifa cha Nchi hiyo.

Wanajeshi wafuasi wa Ojok waliweka vizuizi katika barabara zote za Jiji la Kampala na kuamua kuyalinda majengo yote nyeti ya Serikali likiwemo Jengo la Nile Mansion Hotel ambalo ndilo lililokuwa na Ofisi nyingi za Wizara nyeti za Serikali ya Nchi hiyo.

Kung'olewa kwa Binaisa kulifanywa na Tume maalum ya Watu sita, ambayo ilikuwa ni sehemu ya Baraza la Ushauri la Taifa lililomng'oa Rais Lule, huku matendo ya Tume hiyo pamoja na Ojok kwenye wiki hiyo yakihusishwa zaidi na Rais Milton Obote aliyekuwa ughaibuni, ambaye aling'olewa Madarakani na Amin mwaka 1971. Obote alikanusha kuhusika na matendo hayo ya Ojok yaliyokuwa yakiteteresha hali ya ustawi wa nchi hiyo japo haikubadili ukweli kuwa marafiki hao lao lilikuwa moja.

katika hali ya matatizo yote hayo, Waziri Hussein Ramadhani Shekilango pamoja na Balozi Kilumanga waliamua kupanda Ndege kwenda kumpa habari za namna hali halisi ya mambo ilivyo nchini humo Rais Nyerere ambaye alikuwa kwenye Ziara ya Kiserikali Mkoani Arusha. Safari hiyo ndiyo ikawa mwisho wa maisha yao.

Ilikuwa siku ya huzuni mno kwa kumpoteza Waziri huyo damu changa, Tarehe 11 Mei, 1980, ndege ya Kijeshi iliyowachukua Shekilango, Balozi Kilumanga pamoja na Wanajeshi wanne wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ilianguka katika vilima vya Jiji la Arusha na Abiria wote kupoteza Maisha, wakiacha huzuni na majonzi mazito kwa Watanzania.

Msafara wa Rais ukakatisha ziara na shughuli ya Mapokezi ya Miili ya Mashujaa wetu hao ndiyo ikawa Ratiba rasmi, huku Rais Nyerere akionyesha kwa dhati namna alivyohuzunishwa kwa kumpoteza Waziri huyo Mchapa Kazi kwa Taifa. Majonzi zaidi yakiwa kwa Wanakorogwe waliopoteza Kijana wao Msomi wa Makerere aliyejitolea kuwatumikia kwa dhati.

Shekilango alizikwa Kijijini kwao Jitengeni, Korogwe, Mkoani Tanga, huku akisindikizwa na umati mkubwa wa watu, mpaka leo akibaki Mbunge kipenzi cha watu wa Korogwe na akisifika Serikalini kwa hatua yake ya kurudisha Madaraka Mikoani. Kwa kumuenzi kuna Shule yenye jina lake Jimboni Korogwe.

Mamlaka za Uongozi wa Jiji la Dar es salaam kwa kutambua mchango wa Shekilango kwa Taifa, ikaamua kuipa Barabara mpya iliyokuwa inajengwa wakati huo jina la Shekilango ili kumuenzi shujaa huyu.

Mola amlaze Pema Hussein Ramadhani Shekilango

1452703577368.jpg
 
Back
Top Bottom