Mfahamu jangili Chapuga aliyeitikisa Serikali miaka ya 2005- 2012

Mfahamu jangili Chapuga aliyeitikisa Serikali miaka ya 2005- 2012

fullcup

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Posts
809
Reaction score
2,204
Huyu jamaa stori zake hazifanani sana na akina Jombi ambao walikuwa wakitikisa Mbeya Mjini maana yeye alijikita porini. Alikuwa akifanya uwindaji haramu katika hifadhi ya Ruaha upande wa Mbarali akitokea kata Moja inaitwa Madibira.

Huyu jamaa na wasaidizi wake walikuwa wakinyoa para (zungu) wakati wakiingia hifadhi na ilikuwa ni lazima kunyoa tena iwapo zitaota kabla hawajatoka. Huyu jamaa wakati akitafutwa na askari alikuwa hapatikani kirahisi. Alikuwa na uwezo wa kujibadilisha Maumbo mbalimbali kwa kutumia madawa Kama vile kuwa mwanamke, kichuguu, nyati, Mzee na wakati mwingine jiwe.

Inasemekana aliua askari wengi sana miaka hiyo. Alikuwa anafanya shughuli za ujangili kwa kujiamini sana mpaka wajomba wakawa wanamuogopa. Mara ya mwisho alikuta ujumbe nyumbani kuwa anaombwa na Rais awasaidie askari pori kuimarisha ulinzi kutokana yeye kuyafahamu maeneo mengi ya hifadhi na maficho ya majangili kwa malipo makubwa.

Akakubali na kuanza kuwa sehemu ya askari pori na akilipwa hela ndefu. Kumbe ulikuwa mtego, inasadikika wakati wa kuchoma sindano za kujikinga na magonjwa gani sijui malaria yeye walimpiga sumu hakumaliza miaka miwili wakala wali maharage na arobaini ikawa ndio mwisho wake.
 
Mwamba sana huyu mjomba, alikua anaua nyati halafu anachukua maini tu.
 
Maeneo kama malangali, Mapogoro, Ikoga, Ihefu, Mayota, Walumba wanamjua vzur huyu mwamba
 
Maeneo kama malangali, Mapogoro, Ikoga, Ihefu, Mayota, Walumba wanamjua vzur huyu mwamba
Jamaa alikuwa mtu wangu wa nguvu.Akituuzia Sana nyama pori.Siku moja alituibukia akiwa kwenye umbo la paka.Kila mmoja alipigwa na bumbuwazi.
 
Back
Top Bottom