Mfahamu kipa aliyefunga Hat Trick

Mfahamu kipa aliyefunga Hat Trick

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
33706760_1815215678500479_7628906552526635008_n.jpg


JOSE LUIS CHILAVERT
===================
Magoli 67 na hatrick 1
Yawezekana likawa ni jina geni kwenye masikio yako ila si ajabu wala sio dhambi.Lakini kwa wale walio kitambo kwenye mpira wa dunia hii kutokana na umri na ufuatiliaji wao bila shaka si jina geni kwao.
:
Miaka ile ya tisini wakati dunia imetawaliwa na makipa wa kizazi cha kina Oliver Khan,David Seaman,Fabian Barthez,David James,Taffarel,na wengineo kulikua na mtu mmoja kutoka Paraguay akijulikana kama "BULLDOG" na maanisha JOSE LUIS CHILAVERT.
:
Golikipa huyu na kapteni wa zamani wa Paraguay alifanikiwa kuchezea nchi yake michezo 74 kuanzia 1989 mpaka 2003 na kufanikiwa kuifungia magoli 8.
Chilavert pia ameiwakirisha nchi yake kwa kucheza mashindano ya kombe la dunia mara mbili 1998 na 2002 yote akiwa ndio kiongozi wa timu yaani kapteni tena kapten mbabe sio mnyongemnyonge.
:
Kinachomtofautisha na makipa wengine wa kidunia ni uwezo wake wa kufunga kwa kupiga mipira iliyokufa na penati kiasi cha kua ndio golikipa wa pili duniani kwa kufunga magoli nyuma ya Rogerio Ceni wa Brazil.
Chilavert amefunga magoli 67 kwenye maisha yake ya mpira wa ushindani.
Lakini pia ndio golikipa pekee duniani kufunga hatrick mwaka 1999 akiichezea Vèlez ya Argentina dhidi ya Ferro Carill Oeste kwenye ligi kuu ya nchi hiyo.
:
Kwangu mimi huyu ndio golikipa wangu wa mfano wa muda wote.
Natumai watu kama kina Karius watasimama imara na kupambana na changamoto zinazowakabiri na kuja kua mashujaa wakubwa baadae kiasi cha kusahau machungu wanayoyapitia hivi sasa sababu ili ufanikiwe ni lazima ukutane na misukosuko mizito duniani.
Wasalaaam......
© Raphael Lighongo
 
Hiyo hattrick alipataje kwenye hyo mechi?
 
Najiuliza tu, hivi mbabe kama Oliver khan ndio yupo golin Benzema angethubutu hata kumsogelea kweli?
 
Back
Top Bottom