WilsonKaisary
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 392
- 949
MFAHAMU KWA UFUPI DONNIE YEN
"wale wa season mtupishe kidogo"
Donnie yen mcheza sinema maarufu katika tasnia hii ya filamu Duniani.
Mcheza sinema huyu ambae amezaliwa 27/7/1963 jimbo la Guangdong huko Guangzhou inchini China. Kazi zake hii ya kucheza filamu aliianza katika mji wa Hongkong, kwa sasa ana umri wa miaka (57).
Donnie Yen au jina lingine anafahamika kama (yen ji-da) alisoma elimu ya martial arts, uongozaji wa filamu, utengengenezaji wa filamu. Lakini pia yeye ni mcheza michezo ya kweli kama Karate, Taekwondo, Kickboxing na kumfanya kufahamika ulimwenguni sana.
Mcheza filamu huyu ameoa mara mbili mke wa kwanza alifahamika kama Zing Ci-leng(1993-1995) na kuachana nae, ilipofika mwaka 2003 alioa Lizzy Wang.
Donnie Yen amejaliwa kupata watoto watatu wa kliume wawili ambao ni man zeok yen, James Yen na wa kike Jasmine Yen.
Wazazi wa Donnnie yen baba ni Klyster Yen, mama Bow-sim mark.
Mcheza filamu huyu alianza kuwa maarufu miaka ya 1983 mpaka sasa ameshafanya filamu kama Dragon Cage (2006), Special ID (2013) Ice Man (2014), Kung Fu Jungle (2014), Flash Point (2007) na hii filamu maarufu ya IP MAN zilizotoka kuanzia mwaka 2010 na ya mwisho imetoka mwaka huu inaitwa IPMAN4 ipo sokoni.
Donnie Yen amepata tuzo zaidi ya saba 7 ktk tasnia hii ya filamu na hata ktk michezo yake ya kweli ya ngumi.
Zingatia kuwa michezo mingi ambayo Donnie Yen na Jackie Chan huicheza ktk filamu zao huwa wanafanya kweli kwakua wao wamesomea michezo hiyo ya ngumi na Taekwondo, karate.