free prisoner
Member
- Jun 11, 2020
- 15
- 11
Wengi wanamfahamu punda kuwa ni mnyama anayefanya kazi, jamii za Tanzania hasa mkoa wa arusha na manyara wanamtumia punda kwa ajili ya kubeba mizigo yao, wengi wao humbebesha punda mzigo mgogoni kama magunia ya mahindi, mkaa maji na kuni. Punda amekuwa ni nyenzo muhimu katika usafirishaji wa mizigo yao, katika mikoa ya ziwa Mnyama kazi punda amekuwa ni tegemezi kubwa sana kwa kazi mbalimbali za kusafirisha mizigo, ukienda migodini utawakuta wanabeba maji, matimba na mawe.
Punda amekuwa akifanya kazi ya kubeba tofali kwenye matanuru na kupeleka kwa wanunuzi, punda amekuwa akibeba magogo maeneo ya porini, Ni Jamii ndogo sana tanzania inayokula kitoweo cha nyama ya punda. Lakini je, tumewahi kujiuliza kuwa kwa nini viwanda vya punda vya shinyanga na dodoma vinachinja mamia ya punda kisha kufunga na kupeleka nje ya nchi? Je, umewahi kujiuliza faida yake ipo wapi?
Je, Wizara inaona kusafirishwa kwa bidhaa za mnyama punda ni mali ghafi zenye thamani kubwa sana kwani wanasema kuwa mazao ya punda ni mali ghafi za viwanda vya kutengeneza dawa mbalimbali huko nje. Je, Wizara ilishafanya utafiti huo? Nikisoma kwenye mitandao kwa wale wanaomtetea mnyama punda wanasema punda ni mnyama aliye na thamani kubwa sana kwani mazao yake kama ngozi na nyama ni viungo muhimu sana katika kutengeneza madawa mbalimbali. je? wahusika wanajua hilo?
(WATANZANIA TUAMKE TUTUNZE MALI ZETU)
Mimi nipo huru, Wachina wanamaliza punda zetu.