Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 520
- 2,930
Anaitwa Bantu Stephen (Steven)Biko alizaliwa tar 18/December/1946 huko Tarkastad Afrika kusini akafa tar 12/sept/1979,Pretoria Afrika ya kusini.
Ni mtoto wa tatu ,Baba yake ni Mzingaye Mathew Biko ,mama yake ni Alice Mamcete Biko,Dada mkubwa Bukelwa,kaka Khaya,mdogo wa kike Nobandile baba yake kabla hajajiuzulu alikuwa police kipindi hiko.kabila la familia yake ni Xhosa kwao ni mji wa Ginsberg.
Mwaka 1961 alianza kusomea udaktari (medicine) chuo cha University of Natal ,alipofika alichaguliwa moja wa kiongozi na muwakilishi wa wanafunzi ( Students Representative council).Ila hapo vyuoni kwao kulikuwa na Jumuiya (organization) ya wanafunzi vyuo vyote nchi nzima inaitwa National Union of south African students (NUSAS) ,ambapo uongozi wa chuo ulikuwa na mahusiano na umoja huu.
Umoja huu NUSAS lengo kuu ilikuwa kupinga ubaguzi wa Rangi (Apartheid) ila hakuwa imara sababu ulikuwa umeshikiliwa (Dominated)na wazungu ,kuanzia wingi ,na hata kukithamini fedha ni za wazungu hata maamuzi yalitawaliwa na wingi wa wazingu.
Biko hakupendezwa na hilo ila alichukizwa saana 1967 Julai ,NUSAS iliandaa mkutano wa viongozi wa wanafunzi Chuo cha RHODES huko Graham'stown ,ila walipofika vyumba vya kulalia viliandaliwa tuu kwaniaba ya wazungu na Wahindi ,Blacks akini BIKO waliambiwa wakalale kanisani ,nje ya chuo pale .
Hii ilipelekea Biko kwa kushirikiana na Rafiki zake weusi 1968 kuanza harakati kuunda Jumuiya yao,ila 1969 (Rasmi)Julai Jumuiya yao huru ya wanafunzi iliundwa,iitwayo SOUTH AFRICAN STUDENTS ORGANIZATION (SASO) Biko akiwa Rais wake wa kwanza kitaifa.akiwa na lengo la kuwaonganisha wanafunzi weusi kupinga ubaguzi wa Rangi,na kujiona Rangi nyeusi ndio Rangi bora kuliko zote.aliruhusu uwanachama kwa Wanafunzi weusi tuu ili kuwa na nia madhubuti.
Biko katika harakati zake alivutiwa sana na Mwanafalsafa Frantz Fanon ,na Black power movement (Black Americans) akina Dubois ,Robert William, Malcolm X,katika hii Jumuiya yao ya SASO walianzisha IDEOLOGY (itikadi) iliyowaongoza kupinga ubaguzi wa Rangi iitwayo "BLACK CONSCIOUSNESS" lengo ni kuondoa Nadharia (Mentality) ya Inferiority ya unyonge dhidi ya Rangi nyeusi ,ili kuleta ujasiri ,na majivuno dhidi wa Zungu waliodharau Rangi nyeusi., walianzisha slogan ya "BLACK IS BEAUTIFUL" wakiiga kutoka kwa BLACK AMERICANS miaka yao ya 1960 .
1971 August ,kuna mkutano ulifanyika ulioitwa "Development of African Community conference" uliofanyika mji wa Edendale ,ukilenga kuweka pamoja makundi yote ya watu weusi kupinga ubaguzi.1972 walianzimia kuunda umoja wao mwingine unaoitwa "Black People's Conventions"(BPC) ukikusanya makundi tofauti tofauti wanafunzi (SASO ya Biko),makundi ya vijana na makabila tofauti tofauti, makundi ya kidini ,na watu kutoka pande mbalimbali za Dunia (Globally).Rais wake wa kwanza alikuwa Amayatula na ilikuwa na wanachama 4000 na ilikuwa ikifanya kazi pamoja na SASO ambayo iliendelea kupata wanachama kutoka vyuo na shule mbalimbali Afrika ya kusini.
Ilikuwa ikijipatia fedha kupita michango kutoka kwa wanafunzi, mashirika ya kidini na watu wa nje BLACK AMERICANS (Anglo American Corporation). 1972 Biko alialikwa kumtembelea kiongozi wa PAC Robert Sobukwe ,akakutana na kiongozi wa chama cha Unity Movement, Fikile Bam pia akatakiwa na kiongozi Griffiths Mxenge wa ANC kuona na Oliver Tambo wa ANC lengo ni kukusanya nguvu kupinga apartheid (ubaguzi wa Rangi).
SASO ilikuja na Sera mbalimbali kupinga vikali aina ya elimu inayotolewa kwa waafrika kuwa sio elimu ya kiafrika ni ya kikoloni, migomo na maandamano yakapangwa ,hii ilikuja kuchichewa zaidi baada ya mwanachama wa SASO ,Abraham Onkgopotse Tiro kufukuzwa shule 1972 baada ya kukosoa utawala wa chuo na wakikoloni ,migomo migomo ikaanza kushika kasi .mwaka mmoja baada ya migomo migomo !
1973 ,serikali ikatambua kuwa Biko na hiyo itikadi yao ya BlackConnciousnes kuwa tishio,kumbuka hii itikadi ya Black Consciousness ilikuwa tayari imesambaa kwa wanafunzi wengi na ndio ilipelekea hata SOWETO UPRISING 1976.
1973 serikali ilimzuia Biko kujihusisha na shughuli zozote za kiharakati na wakamuweka under ban yaani chini ya katazo la masharti ,akakatazwa asiongee kwa umma,akakatazwa asiwe mwanachama wa jumuiya yeyote,media zilikatazwa hata zisirushi maneno yake,na alikatazwa asitoke nje ya mji wa kingwilliam (kingwiliam town) .kipindi chote akiwa chini ya katazo jumuiya ya SASO ilichagua viongozi wengine ,biko alitaka kuepuka Cult Personality katika taasisi SASO isionekane ni yeye tuu.
1977 ,17 august baada ya Machafuko ya SOWETO ya 1976 yaliyohusisha wanafunzi, Biko alivunja Amri ya kusema asitoki nje ya Kingwiliam Town yeye akatoka na rafiki yake Peter Cyril Jones kutaka kwenda Capetown ,kuonana na kiongozi wa unity movement aitwaye Neville Alexander ila Neville alikataa kuonana nae sababu alihisi Biko anafuatiliwa na Security service.
Inasemekana kuwa security service walikuwa wanajua safar yake ya Capetown, Biko na Jones wakaamua kurudi Kingwiliam Town ,wakiwa njian Jones akiwa anaendesha Gari ,Biko akiwa seat ya nyume walisimamishwa katika kizuizi (Police Road Block)cha police hiyo tar 18/august 1977 karibu na Grahamstown ,Jones aliamrishwa ashuke ,Gari likakaguliwa wakafungua mlango wa nyuma wakamtoa Biko ,Jones anahadisia anasema alimuangalia Rafiki yake BIKO ila alionekana kutabasamu tuu bila wasiwasi ,hiyo ndio ikawa mwisho kumuona Rafiki yake.
Jones alipelekwa kituo cha Police cha Algoa alikaa siku 533 alitoka 1979 ,na Steve Biko akapelekwa kituo cha police cha walmer Police station, alikamatwa kwa kosa la kukeuka agizo la kutokutoka nje ya Kingwiliam Towns wote wakashikiliwa kwa mahojiano chini ya kifungu cha 6,cha sheria ya ugaidi ya 1967 ya kuweka ndani kwa kigezo cha mahojiano (sect.6 of 1967 Terrorism act without trial for the purpose of interrogation).
Biko alipigwa na kuachwa uchi akiwa kituoni,September 6 ,alisafirishwa hadi makao makuu ya police huko Sanlam akihojiwa kwa Massa 22 ,akiwa na pingu mikononi na miguuni(Hand and legcuffs) ,alikuwa akipigwa sana kila police takriban police 10,akapata tatizo la ubongo (Brain lesions) ,akisimamishwa na kufungwa ukutani juu chini ,kwa muda wa siku 20 alikuwa lockup (cell) akiwa uchi .
Police walimuita Daktar baada ya hali ya Biko kuwa Mbaya ,Dr.Lang akikuja na kusema uongo kuwa hana tatizo lolote ,waliendelea kumpa kichapo hadi walipoita Daktar mwingine Dr.Benjamin Tucker aliyeshauri hali ya Biko sio nzuri anatatizo la Ubongo hivyo apelekwe hospital ya wafungwa huko Pretoria .ila police walikataa.
Ila ilpofika tar 11 sept 1977,hali ya Biko ikawa mbaya zaidi ,police wakamchukua na kumuweka nyuma ya Gari lao LANDROVER ,akiwa na pingu mguuni ,mkononi na akawa ajifahamu akiwa uchi.kumpeleka Mji wa Pretoria (ilipo hospital ya wafungwa) kutoka Port Elizabeth,kituo cha polisi cha walmer police station.umbali wa miles 740 (Km 1190) masaa 12 njiani na Gari.
Walipofika ,kesho yake akiwa cell ya Pretoria alifariki Dunia tar ,12,sept, 1977. ,tatizo likiwa ni Uremia,Kidney failure,Intraval Blood Coagulation.
Kifo chake kilishtua ulimwengu ,hadi Rais wa marekani Jimmy carter alikemea vikali,wanafunzi, wanasiasa ,watetezi ulimwenguni .
Msiba wake ulifanyikia kingwiliam stadium, uwanjani mwaka 1977,sept 25 watu takribani 20000 blacks na wazungu walihudhurua,mabalozi wa mataifa 13 ,Viongozi wa kidini Anglican Desmond Tutu , matishits yaliandikwa jina lake,mabango,msiba ulikuwa mzito sana .
Alizikwa kwao Ginsberg.
Mkuu wa police anaitwa Jimmy Kruger alikuja toa taarifa kuwa BIKO hakupigwa wala hakuuwawa ila aligoma kula ,(hunger strike ) watu waliponga na kukataa, mwaka huo huo SASO ikafutwa(Banned ) ,na BCP zikafutwa .
Biko aliamsha hisia kali za wanafunzi na blacks South Afrika kudai uhuru na kupinga Ubaguzi wa Rangi ,hisia kutoka kimataifa zilizidi kupinga ubaguzi wa Rangi.
Baada ya Uhuru South Afrika ,1994 mwaka 1995 iliundwa Tume iitwayo Truth and Reconciliation commission(TRC) kuchunguza ,vifo vya watu hasa kifo cha STEPHEN BIKO BANTU wapo waliokamatwa nakukiri mfano ,police Colonel Gideon Nieuwoudt alikiri kuwa kweli walimuwa Biko .
Mandela alipata kumuheshimu sana Steven Biko ,na kumzungumzia mema kuwa walimuwa sababu alikuwa mwiba dhidi ya Ubaguzi wa Rangi hadi sasa Bado anakumbukwa na kuheshimika sana ,Duniani.kama mpambanaji dhidi ya ubaguzi wa Rangi.
Abdul Nondo.
abdulnondo10@gmail.com.
Reference.
*Black students politics in higher Education.1968-1990.
*Steven Biko by Barstein .
*l write what l like by Steven biko edited by Desmund Tutu.
Shukran!oooh