Joseph Gadiel
JF-Expert Member
- Dec 23, 2022
- 407
- 713
Tarehe 18 Septemba, Kanisa linaadhimisha maisha ya Mtakatifu Yosefu wa Cupertino, mtu wa imani ambaye labda alikuwa maarufu zaidi kwa uwezo wake wa kupaa. Baba yake, seremala masikini, alikufa kabla ya kuzaliwa kwake na mama yake, ambaye hakuweza kulipa deni, alipoteza nyumba yake na akamzaa Joseph kwenye zizi huko Cupertino, Italia mnamo Juni 17, 1603.
Joseph alianza kuwa na maono ya ajabu alipokuwa na umri wa miaka saba, na mara nyingi alipotea kwa ulimwengu unaomzunguka hivi kwamba watoto wengine walimdhihaki wakimpa jina la utani, "mdomo wazi" kwa tabia yake ya kutojali.
Alikuwa na hasira vibaya sana, akiwapa wengine maonyo kwamba yeye ni bubu na asiyefaa kitu. Kando na hayo, alikuwa akivutwa na msisimko kila mara kiasi kwamba haikuwezekana kwake kuwa makini na kazi zilizokuwapo. Hivyo, alipopata kazi, aliipoteza haraka sana.
Hatimaye alifanikiwa kupata kazi ya kutunza ng'ombe katika nyumba ya watawa ya Wafransisko huko Cupertino. Alipojitambua na kuona mwenendo wa maisha yake alivutiwa na maisha yale, Hivyo iliamuliwa kwamba aanze kusomea ukuhani.
Joseph alikuwa mwanafunzi maskini sana, hata hivyo wakati wa mtihani wake wa mwisho, mtahini alitokea kumuuliza swali juu ya mada moja anayoijua vizuri. Alipita na kufaulu vuzuri katika ukuhani.
Yusufu alitiwa ujuzi wa kimungu ambao ulimfanya kuwa na uwezo wa kutatua baadhi ya matatizo magumu zaidi ya kitheolojia.
Siku moja alipokuwa akiadhimisha misa katika hali ya kushangaza, Waumini walimwona akipaa kuelekea juu darini pasipo yeye kujua,Alipofungua macho alijiona akielea hewani, Baada ya kushuka chini alipoendelea na misa hali hiyo iliendelea kujirudia ikapelekea waumini kuogopa na hata kuleta taharuki kwa kuhofia jambo waliloshuhudia.
Kwa miaka 35 iliyopita ya maisha yake kama padre hakuweza kuadhimisha Misa hadharani kwa sababu mara nyingi, katika hali isiyokuwa ya kawaida, alinyanyuliwa hewani alipoingia katika hali ya rohoni, ambayo ilifanyika karibu kila Misa. Ilichukua marejeo madogo tu ya kitu chochote kinachohusiana na Mungu ili hali hii iweze kushawishiwa ndani yake.
Licha ya kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine, kwa sababu ya usumbufu aliousababisha kutokana na hali hiyo.
Alifariki tarehe 18 Septemba 1663 na kutangazwa mtakatifu mwaka 1767 na Papa Clement XIII. Yeye ndiye mlezi wa wasafiri wa anga na wanafunzi wanaojiandaa kwa mitihani.