tzhosts
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 403
- 510
Katika ulimwengu wa biashara,kuna aina mbili za wateja
Kuna wateja ambao ni LOYAL na wateja ambao ni ROYAL mteja ambaye hayuko katika kundi moja katia ya hili basi sio mteja.
Mteja ROYAL ni mteja yoyote yule ambaye ananunua kwako kwa mara ya kwanza au mara kwa mara-Ndio maana kuna msemo mteja ni mfalme.Mteja wa pili ni yule ambaye ananunua kwako mara kwa mara yaani ni loyal kwako.
Sasa hawa wateja wawili ndio wa muhimu sana kwenye biashara yako na ukiwapoteza hao basi utawapoteza wateja wengi zaidi.
Hata hivo kuna wateja wengine ambao bado sijawapa jina ila wanakua na tabia ya kuja dukani kwako na kukuelekeza namna ya kufanya biashara yako kwa maslahi yao.Mfano(Mteja anakwambia mbona kwa fulani tunauziwa bei hii?)Kama anauziwa bei hio si aende akanunue huko?Aina hii ya mteja ikiwezekana usimuuzie kabisa huduma au bidhaa yako.Ukimuonea huruma sana Mwambie Nenda kanunue Pale kwa bei ya chini uje uniuzie mimi.Akija na mzigo wake mwambie peleka kwako ukatumie wote.
Kwa nini nasema huyu ni mteja wa kupotezwa na kupotezewa?Ni kwa sababu yeye anataka kukufundisha wewe jinsi ya kufanya biashara yako bila kujali maslahi yako.Unapofanya biashara,una malengo na unaelewa ni nini unataka kupata,Mtu anapokupangia BEI anakosa adabu.Kupangiwa bei ni tofauti na kuomba discount-Mteja anaeomba discount sio sawa na anayekupangia bei.
Kila heri