Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
NI NANI HUYO.
Kwa majina anafahamika kama Amarjeet Sada kijana aliyezaliwa mwaka 1998 huko nchini India katika familia ya kimasikini.
Inaelezwa kuwa mauaji yake alianza kuyafanya kuanzia mwaka 2006 hadi 2007 hapo akiwa na umri wa miaka saba tu lakini kabla ya kuanza mauaji hayo kuna vitu vilionekana kutokuwa sawa kwa Amarjeet navyo ni,
Inasemekana Amarjeet hakuwa mtoto aliyependa kuchangamana kabisa na watoto wenzake na mara nyingi alikuwa ni mtu wa hasira za hovyo na kali sana pindi anapokuwa anasemeshwa na wenzake yaani ni alikua akikasirika bila sababu za msingi.
MAUAJI ALIYOYAFANYA MTOTO AMARJEET SADA
Muhanga wa kwanza wa Amarjeet alikuwa ni binti mdogo wa miaka sita na inaelezwa kuwa binti huyo alikuwa ni binamu yake kwani alikua ni mtoto wa shangazi yake.
Siku ya tukio inaelezwa kuwa Amarjeet na binti huyo waliachwa pamoja nyumbani wakiwa wanacheza na mama yake Amarjeet ambae alikua ametoka na kwenda sokoni.
Sasa basi inaelezwa yule binti alijihisi usingizi na akaamua kulala kitendo kilichomfanya Amarjeet aanze kumchokoza kwa kumfinya finya binti yule ambae alianza kulia kwa sababu ya kufinywa kule.
Cha ajabu ni kuwa badala ya Amarjeet kuhairisha zoezi la kumfinya binti yule ndio kwanza aliamua kuchukua tofari na kuanza kumpiga nalo kichwani kwa nguvu kwani alitaka kumfanya yule binti alie zaidi.
Amarjeet alidai kuwa alikua anafurahia kusikia kilio cha kuomba msaada alichokitoa binti yule.
Baada ya kuwa amemaliza kumuua yule binti Amarjeet alizunguka nyuma ya nyumba na kumzika binamu yake huyo na pale wazazi wake waliporudi na kumuuliza aliko binamu yake Amarjeet hakusita kuwaonesha alipokuwa amemzika binamu yake.
Wazazi wake kwa kuhofia kumpoteza mtoto wao ikabidi wawadanganye wazazi wa yule mtoto kuwa amepata ajali na kufariki na waliwaomba sana wazazi wale wasili ripoti tukio lile polisi bila kujua walikuwa wanafuga mnyama mkali nyumbani kwao aliyekuwa ameshanusa tayari harufu ya damu na ndio maana hakupata shida kumuua dada yake na hiyo ilikuwa ni miezi kadhaa baadae tangu atoke kumuua binamu yake.
Inaelezwa kuwa wakati wa mauaji yake ya kwanza Amarjeet, mama yake mzazi alikua ni mjamzito hivyo baada ya miezi kadhaa alijifungua binti wa kike.
Ilikua ni furaha ilioje kwa wanafamilia wale lakini kwa Amarjeet yeye hakuelewa ni namna gani angeweza kuishi na huyo mtoto ambae muda mwingi alionekana kuzipa tabasamu nyuso za wazazi wake kitu kilichomfanya asimwelewe zaidi dada yake huyo.
Siku moja mama yake mzazi alijisahau na kupitiwa na usingizi huku nyuma akiwaacha Amarjeet na mdogo wake wakicheza.
Mama huyo alilala kwa muda kabla ya kuja kushituka baadae na kugundua kuwa ameshachelewa tayari kwani Amarjeet alikua ameshamnyongelea mbali mdogo wake huyo.
Kama ilivyokuwa mwanzo wazazi wake wakaamua tena kuitunza siri hiyo bila kumwambia mtu yeyote yule kwa madai ya kumlinda kijana wao mdogo.
Kama waswahili wasemavyo za mwizi ni arobaini basi siku za kukamatwa kwa Amarjeet ziliwadia na hiyo ni baada ya Amarjeet kuamua kumuiba mtoto wa mwalimu shuleni mtoto aliyekuwa na umri wa miezi sita tu tangu kuzaliwa kwake na kama ilivyokuwa kawaida yake Amarjeet alimnyongelea mbali yule mtoto na kisha kumzika.
Juhudi za kumtafuta mtoto yule zilianza na kwa kuwa watu wa mtaani pale walikuwa wameshaanza kumuhisi vibaya Amarjeet ilibidi akamatwe na kuhojiwa na bila kuogopa Amarjeet alikiri kumuiba mtoto yule na kumuua na kisha kumzika.
Cha ajabu na cha kustaajabisha inaelezwa kuwa wakati Amarjeet anatoa ushahidi ule hakuwa hata akiogopa wala kuonekana kujutia kitendo alichokuwa amekifanya na badala yake aliomba apatiwe biskuti ale kwani alikua ana hamu nazo.
Kwa sasa inaelezwa Amarjeet Sada alishaachiwa huru kutoka gerezani alikokuwa amefungwa lakini hakuna ajuaye Amarjeet alielekea wapi lakini kuna taarifa tu zinazodai Amarjeet alibadili jina ndio maana imekuwa kazi kujua aliko mtoto huyo KATILI kuwahi tokea.