Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
1) Flamingo wanauwezo wa kuhisi mvua ikiwa umbali wa km 500.. Sio flamingo wote wana uwezo huo isipokuwa ni Flamingo kutoka bara la afrika hasa wanaopatikana nchini Namibia
2) Neno flamingo ni neno la kihispania flamenco lenye maana ya moto... Na sababu ya kuitwa hivyo ni kutokana rangi ya manyoya yao (pink au rangi ya machungwa)
3) Flamingo husakata rumba katika michakato ya kutafuta mwenza.... Ndio flamingo wa kike na wakiume huwa na tabia ya kudance ili kuwavutia wenza na wanapopata wapenzi huwa ndio huyo huyo mmoja hadi kufa
4) Flamingo aliyepevuka ana urefu wa kati ya futi nne hadi tano
5) Kuna aina sita za flamingo lakini huwezi kutambua kama haujafundishwa tofaut zao
6) Flamingo wa kike na wakiume hukaa juu ya yai karibia mwezi kwa wakati wa kutotoa
7) Flamingo wana chakula maalum kwa ajili ya watoto wao ambapo chakula hicho huzalishwa kwenye makoo yao... Chakula hiko ndio watu huita ni maziwa... Huwa ni ya rangi ya pinki na hufanya hivyo kwa kati ya siku 5 hadi 12 baada ya kutotoa
8) Nchi ya Bahamas wanamtumia flamingo kama ndio ndege wa taifa
9) Flamingo mwenye rekodi ya kuishi miaka mingi aliishi kwa miaka 83 katika zoo ya Adelaide nchini Australia... Flamingo huyo alifariki mwaka 2014
10) Kwa mwaka wanataga yai moja tu
11) Flamingo wanaweza kupaa kilometers 56 kwa saa moja
12) Umri wao wa kuishi ni kati ya miaka 20 hadi 30 (lifespan)
13) hutumia asilimia 30 ya muda wao wa siku kwa ajili ya kujisafisha mabawa yao
14) Flamingo anapotaka kupumzika husimama kwa mguu mmoja
15) Kuna zaidi ya mifupa 19 kwenye shingo ya Flamingo
16) Flamingo huwa na amani akitembea na wenzake kwa kundi kubwa kuliko wachache