Panzi Mbishi
JF-Expert Member
- Mar 8, 2021
- 2,231
- 2,904
Kumbe mgoma alifanya yeye dah!Kafanya ngoma nyingi but beat ya balozi "Kwenye Chati" hakutakuja kutokea banger kama lile..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe mgoma alifanya yeye dah!Kafanya ngoma nyingi but beat ya balozi "Kwenye Chati" hakutakuja kutokea banger kama lile..
Hardmad - TamalaHANA MAKUU.sijawahi kumsikia kwenye skendo.na nimekuja kumjua ukubwani.japo nilikuwa nasikia jina lake kwenye nyimbo.
Miikka Mwamba kama angekuwa kafanya albamu ya Saida Karoli na ule wimbo wa Eno Maiki tu tayari angekuwa kaingia katika list ya ma producers bira kabisa kufanya kazi Tanzania.Mwaka 1993 MIIKKA ALEKSANTERI KARI akiwa anaipambania elimu yake ya chuo kikuu
.View attachment 2991728
Ndipo anapewa Information kuwa anapaswa kuja nchini TANZANIA haraka iwezekanavyo.
Taarifa ile ilimtaka MIIKKA kuwasiri TANZANIA akiwa na watu kadhaa Walifika TANZANIA na hapo wakapokelewa na mtu aliyejitambulisha kama Captain JOHN KOMBA.
View attachment 2991740
Captain JOHN KOMBA aliwachukua kina MIIKKA moja kwa moja mpaka nyumbani.
Kisha walivyofika hapo MIIKKA akaambiwa
"kuanzia sasa utakuwa unaishi hapa"
MIIKKA akaanza kuishi hapo, lakini siku kadhaa mbele akapelekwa mpaka Tanzania one theatre, ndio hiyo band ya music mnaiita "TOT"
Kwa kuwa MIIKKA alikuwa na utaalamu wa vifaa vya music hapo akatakiwa kufanya kazi fulani zinazohusiana na music.. Akiwa hapo TOT akaweka urafiki wa siku kadhaa na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la KENNY.
KENNY ni shabiki wa music wa kofokafoka, hivyo hakupaswa kuambatana naye kwakuwa hiyo si kazi iliyomleta, ila MIIKKA aliweka urafiki wa siri.
Lakini hata hivyo MIIKKA hakujua kuwa. Kazi hiyo ikiisha anapaswa kurudi nchini kwao FINLAND mara moja.
Baada ya kazi hiyo kuisha, MIIKKA alifanya kama maagizo yalivyo mtaka..
Naam! MIIKKA alirudi nchini kwao FINLAND, ila akiwa FINLAND ndipo. Anasikia anapaswa kuambatana tena na watu kadhaa mpaka nchini ZAMBIA, huko kuna documentary fulani wanapaswa kwenda kufanya.
View attachment 2991751
Safari hiyo ikaanza mara moja Ila wakiwa njiani MIIKKA akabadirisha usafiri na kuchukua usafiri ambao ulimleta mpaka nchini TANZANIA. Alipofikia TANZANIA akamtafuta KENNY,
View attachment 2991752
KENNY akampokea MIIKKA, Kisha akamtambulisha kwa rafiki yake aliyeitwa TONY..
hivyo awamu hii tunaweza kusema wenyeji wa MIIKKA walikuwa ni KENNY na TONY.
MIIKKA akaanza kuonyeshwa chocho za jiji la DAR ES SALAAM lakini. hata hivyo maisha ya getogeto hayakuwa poa sana, pesa ilikata day after day.
MIIKKA akawaza nini cha kufanya, ndipo akamshitua TONY kuwa yeye anaweza ku-produce music.
Yaani kama wakipata sehemu basi wanaweza kutengeneza kipato cha kujikimu..
TONY akaamua kumpeleka. MIIKKA moja kwa moja mpaka zilipo studios za MJ RECORD,
TONY akawaambia wale majamaa aliowakuta pale MJ RECORD kuwa..
Oyaa huyu mtu ni nomaa anaweza ku-produce music mbaya, mchukueni.
Wale majamaa wakasema mpaka wafikishe ujumbe kwa bosi. wao ambaye ni MASTER J.
View attachment 2991753
Hivyo TONY na MIIKKA waliombwa kuondoka, kwamba ujumbe wao ungefikishwa kwa bosi na wangejibiwa siku kadhaa mbele.
Lakini masiku yakasonga bila majibu yoyote.
TONY na MIIKKA wakaona ukimiya nao ni jibu, ndipo TONY alipoamua. Kumpeleka MIIKKA kwa bosi mwingine..
Bosi huyo ambaye alikuwa akimiliki Studios za FM RECORD baada ya kumuona MIIKKA akavutiwa naye na kumpa kazi moja kwa moja... Hapo ndipo historia ya music inapoanza kuandikwa na MIIKKA
MIIKKA akafanya kazi na watu kama
Dully Sykes- julieta
Solid Ground Family-Athumani Mlevi
Zahrani Ft Complex-Tupa Mawe.
Kisha akafanya albam nzima ya saida karoli iitwayo maria salome
lakini hata hivyo. Mwaka 2002 MIIKKA akafanya kazi na msanii MAD ICE wimbo ukaitwa Baby Gal.
Wimbo huu ulivuma mnoo
Moja ya vitu ambavyo MIIKKA alikuwa akivifanya mara zote, akiwa anatengeneza mdundo nikuacha instruments zishike nafasi na beat itembee. Umaarufu wa MIIKKA uliongezeka Na hapo akaanza kujiita MIIKKA MWAMBA..
Yaani majina yake halisi ni MIIKKA ALEKSANTERI KARI, hivyo alibadili jina lake la mwisho ambalo ni KARI liwe kwa Kiswahili na tafsiri yake ni MWAMBA, that's why akajiita MIIKKA MWAMBA.. MIIKKA akaanza kuzungumzwa na kutajwa kama producer chipukizi na hatari kwa ukanda wa East African.
Jambo lililofanya mtu mzima ZIGGY DEE avutike kutoka nchini UGANDA na kuja kufanya naye wimbo ulioitwa ENO MAIKI... Kama huujui wimbo huo wa ZIGGY DEE perhaps unapaswa kutazama vizuri line ya umri wako.
Huu ni wimbo uliamsha hisia za watu, miaka hiyo ulibamba mbaya kwenye makumbi ya starehe club🙌🏻
Na kumfanya MIKKA kuzidi kuzungumzwa kama producer anayekuja kwa kasi
Jambo hili likafanya Wasanii wengi waliokuwa wanajitafuta kwenye game, wamuibukie MIIKKA pale FM RECORD na kuomba kufanya kazi naye.
Alipendwa na wengi, sababu MIIKKA alikua mpole na muelewa lakini pia ni producer aliyempa muda mwanamuziki.
Likewise kwa D KNOB. Wakati ambao D KNOB anajitafuta, akaibukia kwa MIIKKA akamsumbua sana pale, brother najua brother najua.
View attachment 2991754
Basi MIIKKA akaamua kutengeneza beat na kumpa D KNOB ili aifanyie mazoezi.
Kisha MIIKKA akapata safari, akarudi nchini kwao FINLAND. Huku nyuma D KNOB akawa na kazi ya kuandika mistari na kufuta..
Katika uandishi wake wote huo wa kufuta-futa akasahau kuweka chorus.
MIIKKA alivyorudi tu TANZANIA D KNOB akawa wa kwanza kufika studio brother tayari nimemaliza..
MIIKKA akachukua. beat ileile ya D KNOB na kumwambia aimbe ili amsikie..
D KNOB si ndio akaanza kuflow sasa, MIIKKA akashangazwa na alichokisikia na kubaki anacheka..
Unujua alicheka nini, alicheka baada ya kusikia wimbo hauna chorus.
Miaka hiyo ilikuwa ni kitu cha ajabu sana..🙌🏻. Lakini MIIKKA akamshauri D KNOB wajaribu kuweka chorus mwanzo wa nyimbo na mwisho wa nyimbo..
Na baada ya wimbo ule kuachiwa ukawa ni habari nyingine, jambo ambalo hawakulitegemea... MIIKKA akawa gumzo, jambo lililofanya studios tofauti za bongo kutamani kufanya kazi naye..
MIIKKA alikuwa na uwezo wa ajabu wa kutumia instrumental moja ndani ya beat nyingi tofauti.
Na bado instrumental ikaendelea kuleta radha tofauti. Mfano kwenye beat ya wimbo wa MAD ICE Uitwao baby gal. Mule ndani kuna instrumental fulani inafanana na malimba.... Likewise ukija kwenye wimbo wa D KNOB Uitwao Elimu mtaani. Mule ndani kuna instrumental inayofanana na malimba.... Kama hiyo haitoshi ukisikiliza wimbo wa saida karoli uitwao mapenzi kizunguzungu, Mule ndani kuna instrumental inayofanana na malimba...
Lakini ukisikiliza hizi nyimbo zote kila wimbo unakupa radha tofauti🙌🏻
Itoshe kusema MIIKKA alikuwa mwamba kweli..
Aishi sana popote alipo🙏🏼.
Wimbo wa saida karoli chambua kama karanga na eno mike kafanya mbonaMiikka Mwamba kama angekuwa kafanya albamu ya Saida Karoli na ule wimbo wa Eno Maiki tu tayari angekuwa kaingia katika list ya ma producers bira kabisa kufanya kazi Tanzania.
Ukisikikiza beat za albamu ya Saida Karoli, ukisikikiza beat za Eno Maiki, kama unaujua muziki, utagundua unasikikiza kazi ya producer anayejua anachofanya.
Lakini alifanya kazi nyingi sana nzuri, zenye vionjo vya Kitanzania. Miikka alikuwa anaweka vionjo fulani vya muziki wa asiki kwenye hip hop kwa namna ambayo hakuna producer mwingine yoyote wa Tanzania aliyeweza kufanya.
It was so ironic kwamba producer mzungu ndiye katupa muziki mzuri wenye vionjo vya Kitanzania.
Miika Mwamba sijui kaachiwaje mpaka kaondoka lakini jamaa aliupandisha muziki wa Tanzania mpaka watu wa Kampala wakawa wanamuita "Mzungu wa Tanzania".
Najua kafanya albamu ya Saida Karoli na Eno Maiki.Wimbo wa saida karoli chambua kama karanga na eno mike kafanya mbona
Kuondoka sababu ni mmiliki na boss wake wa FM studio aliyokua anafanya kazi Mzee Muta alikua hamlipi vizuri na kwa wakati. Sasa badala ya kulipa direct kwa ofisi ikabidi muwe mnakubaliana na miika bila boss kujua. Sababu zingine ni minor tu
Pia kwaya alikua anafanya sana, kina cosmas chidumulo zile nyimbo zilizotamba yeye ndio alitengeneza.Najua kafanya albamu ya Saida Karoli na Eno Maiki.
Nasema kwamba kama hizo ndizo zingekuwa kazi zake zote alizofanya Tanzania tayari angekuwa legend, lakini kafanya zaidi.
Hayo mambo ya malipo huwa tunajizibia wenyewe. Miikka alikuwa producer wa kiwango cha kimataifa na huyo Mzee Muta angejua kukaa naye vizuri wangekamata soko kubwa na kufanya kazi nzuri sana, kimataifa.
Ila tamaa ya kupata pesa haraka bila ya kuwa na vision ya nuda mrefu inatunyima mambo mengi mazuri.
biggestkaka.co.ke