Mfahamu 'Ringberia Kanyaboya' wa Kariakoo alivyosababisha uwepo wa neno 'Kanyaboya'

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Kisa cha mchezo wa kanyaboya ulioingia mjini miaka ya themanin nakitu mjini Dar na hususani sehemu za Kariakoo.





Kwanza ni lazima niweke wazi maana ya neno hilo lilipotokea na kwanini usanii au wizi wa kiaina fulani uitwe Kanyaboya.

Ringberia Kanyaboya ni jamaa fulani wa kutoka nchini Burundi, kama mtakumbuka kuwa aliibuka mjini Dar miaka ya themanini na kitu akidai kuwa yeye ni mpiganaji ngumi wa kulipwa na alitafutiwa mapambano makubwa hapa nchini lakini baadaye ikajulikana kuwa si chochote ni muongo na hajawahi kupigana sehemu yoyete ile duniani na tayari aliisha kula pesa za watu na kutokomea gizani pasi ya kujulikana sehemu alipokwenda.

Mpaka hivi leo ukimfanyia mtu usanii wa kumuibia kwa njia ya udanganyifu watakuita umemfanyia mtu Ukanyaboya. Nimewahi kufanya kazi ndani ya soko la Kariakoo ambako company niliyokuwa naifanyia kazi kufungua ofisi ndogo ndani ya soko hilo,nili bahatika kujifunza mambo mengi mle ndani na nimeshuhudia huo ukanyaboya jinsi unavyoendelea hususani katika mtaa wa Tandamti na nyamwezi ambao umepakana na soko pale mbele ya maduka ya washihiri,

Targeti ya wezi hao ni watu kutoka miji midogo midogo wanaoingia mjini kutafuta mashati ya ndege, kama mnavyokumbuka fesheni ya mashati ya ndege ilivyoingia miaka ya mwisho sabini na tisa na kuendelea.

wizi wenyewe ni ka hivi, kwanza unamuona mtu kasimama mbele ya duka na shati la ndege analionyesha kuwa analiuza kwa bei poa, na mara unaona anatokea wakuja kuulizia bei ya hilo shati la ndege na kupewa bei yake na baada ya kupatana kwa muda jamaa anakubaliana na bei ya mnunuzi , yule jamaa anayeuza shati hayuko peke yake ni timu ya watu wawili mmoja ana simama mbali kidogo na hao wawili na mambo yakiwa tayari humpa sign yule jamaa yake aje na kijifurushi kilichojazwa matambara mabovu ndani yake kinacho fanana na kile kilichokunjwa na shati la ndege


wakati wakuja anahesabu fedha ili kulilipia shati la ndege wale wawili tayari wameisha peana sign na yule mwenye shati la boya huja nalona kumpatia mwenzie kiujanja pasi na wakuja kuona baada ya hapo hulipia shati feki na kukabidhiwa mzigo wake wenye vitambara vibovu ndani yake ,nimeshuhudia wizi wa aina hii mbele ya macho yangu na kunawakati ilikuwa ni part ya entertainment yangu wakati jamaa zangu wakija nitembelea pale ofisini kwangu kama hatuna la kufanya huwachukuwa kwenda kuwapa burudani ya bure pale nje ya soko,ni kamchezo kabaya sana yaani mtu anapigwa Kanyaboya akiamini kuwa kweli amenunua shati la ndege ,kama mnavyojua mtu akiisha nunua kitu kipya kuna wakati atataka kukifungua na kukiangalia vizuri,yaani ni ka ma uchawi unamuona mtu kama hatua kumi anajaribu kufungua kile kifurushi alichonunua akiamini mle ndani kuna shati lake la ndege akikifungua kile kifurushi anakuta ni matambara na uchafu mweingine ndani yake,

utamuona mtu anaangalia pale alipotoka kulinunua lile shati na tayari jamaa wameisha yeyuka gizani ,wakuja yule atakuja na kujaribu kumtafuta mtu aliyemuuzia shati pasi na kujua amuulize nani,yaani ni mchezo unaosikitisha sana na ni burudani moja ya kuchekesha sana ninatamani ka ningeweza kuufanyia document kwenye film yaani kurekodi kila hatua jinsi mtu anavyolizwa pesa yake ni kichekesho kikubwa
 
KANYABOYA

Kanya Boya ni BOXER bondia wa ngumi za kulipwa wa Burundi

Bondia huyu Felix Kanyaboya kati ya Miaka ya 1986 / 1987 alikuja kucheza Tanzania , Alikuwa anafikia Hotel za Kariakoo.

Bondia huyu alikuwa na Mikwala mingi saana na siku ya Mechi anatoka Hotelini Kariakoo anatembea kwa Miguu akiwa kavalia kabisa Gloves , ring bout, Gum sheed, anapiga shadow box njia nzima na watu wanamshangilia mpk Railways Club Gerezani

Akipanda Ulingoni Round zake 2 tu kapigwa KO mbaya , ndipo Jina lake likavuma KANYABOYA

Anajifanya anajua ngumi, mbwembwe nyingi akipanda Ulingoni anapigwa ndio jina likakuwa KANYABOYA
 
Unamjua "KANYABOYA"?

Kanya Boya alikuwa bondia wa ngumi za kulipwa kutoka Burundi. Bondia huyu, jina kamili Felix Kanyaboya alikuja Tanzania kati ya Miaka ya 1986/1987. Alikuwa anafikia Hotel za mitaa ya Kariakoo...

2/ Sifa yake kubwa ilikuwa ni mikwara, kama Mandonga. Siku ambayo alikuwa na pambano, alitokea hotelini mitaa ya Kariakoo na kutembea kwa mguu akiwa amevalia kabisa gloves, viatu na gum shield. Alipasha njia nzima huku akipiga hewa, akirukaruka na watu walipiga shangwe za kutosha na kumsindikiza hadi pale Railway Club Gerezani Kariakoo. Sasa pambano kuanza ulingoni, hachukua hata raundi 2, akachapwa KO za haja.

Alipigwa na Habibu Kinyogoli na Omari Yazidu Omari kama mtoto

Basi Kuanzia hapo, ndio likazaliwa asili ya neno KANYABOYA Tanzania.

 
Mwananyamala posta eeh, Manzese kariakoo, Tandika shule ya uhuru baba, ogopa kanyaboya..!! NIMEKUMBUKA MBALI SANA
 
Umetisha mzee.
 
Kwa mara ya kwanza Bi. Mama umetoa positive comment kwa mtu alietoa elimu ya jambo.

Maana daima kama si kukosoa uandishi basi huwa ni dhihaka.
Unanisoma kwa uoga tu.

Unayodhani wewe siyo "positive" ndiyo "positivity" yenyewe hiyo. Usifikiri kukubaliana na kila uharo ndiyo kuwa "positive".
 
Unanisoma kwa uonga tu.

Ubayodhani wewe siyo "positive" ndiyo "positivity" yenyewe hiyo. Usifikiri kukubaliana na kila uharo ndiyo kuwa "positive".
Uharo kama huo uliouandika hapo.
 
Alikuwa bondia wa ngumi za kulipwa kutoka nchini Burundi,

Bondia huyu Kanyaboya alikuja Tanzania kati ya Miaka ya 1986/1987 na Alikuwa anafikia Hoteli za mitaa ya Kariakoo,

Sifa yake kubwa huyu bwana ilikuwa ni mikwara,

Yaani Siku ambayo alikuwa na pambano alitoka hotelini mitaa ya Kariakoo na kutembea kwa Miguu akiwa ameshavalia kabisa Gloves , ring bout na Gum shield,

"Alipasha" kwa kupiga "shadow box" njia nzima na watu wanamshangilia mpaka pale Railways Club Gerezani,

Sasa kituko alikuwa akipanda ulingoni, Round zake 2 tu anapigwa KO mbaya na akina Habibu Kinyogoli, na Omary Yazidu,

Kuanzia hapo Jina la KANYABOYA likavuma na kuwa maarufu.

#Jifunze #Elimika #Furahi

#tupe maoni yako kuhusu kanyaboya😃
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…