Mfahamu Sarah Baartman muafrika aliyefanywa sanamu kutokana na umbo lake

Mfahamu Sarah Baartman muafrika aliyefanywa sanamu kutokana na umbo lake

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,213
Reaction score
2,938
Unajua kuwa kuna mwanamke wa Kiafrika ambaye serikali ya Ufaransa ilimiliki viungo vyake vya siri kama "mali ya taifa" na kuvionyesha kwenye makumbusho kwa miaka 160 baada ya kifo chake? Udhalilishaji alioupata akiwa hai ulikuwa wa kutisha, lakini unyama uliofanywa kwenye mwili wake baada ya kukata pumzi utaliza utu wako. Hii ni siri nzito ya kihistoria ambayo nchi za Magharibi zisingependa uijue, na ndio sababu iliyomfanya Nelson Mandela kupigana vita vya kisheria vya miaka minane kumtoa mwanamke huyu gerezani akiwa tayari ni marehemu.

Kutoka Binadamu hadi "Mnyama"
Mwaka 1810, msichana masikini wa kabila la Khoikhoi nchini Afrika Kusini aitwaye Sarah Baartman, alidanganywa na daktari wa Kiingereza kwenda Ulaya kwa ahadi ya kuwa staa mkubwa kwa sababu ya umbo lake kubwa la asili la makalio makubwa
Alipotua London, aligeuzwa kuwa mtaji wa pesa. Alibatizwa jina la "The Hottentot Venus", akafungwa minyororo shingoni, na kuwekwa kwenye jukwaa ambapo wazungu walilipa pesa kuja kumtazama akiwa uchi na kumgusa kwa vijiti ili kuthibitisha kama umbo lake ni la kweli au ameweka mto.

Baada ya Kifo
Baada ya kuuzwa kwenda Paris na kufariki mwaka 1815 akiwa na miaka 26 tu kwa msongo wa mawazo na magonjwa, ukatili ndio
Wanasayansi wa Ufaransa walichukua maiti yake, wakamkata ubongo na viungo vyake vya siri, wakaviweka kwenye mitungi ya kemikali, na kuvisimamisha kwenye makumbusho ya Musée de l'Homme jijini Paris. Raia wa Ulaya waliendelea kulipia tiketi kuona viungo vya siri vya mwanamke huyu hadi mwaka 1974!

Heshima ya Mwisho
Mwaka 1994, Nelson Mandela alipoingia madarakani, aliitaka Ufaransa irudishe mabaki ya Sarah. Ufaransa waligoma kwa miaka 8 wakidai kisheria mwili wake ulikuwa "mali ya nchi yao." Baada ya shinikizo kubwa la kisiasa, bunge la Ufaransa lilipitisha sheria maalum, na Sarah alirudishwa na kuzikwa kwa heshima Afrika Kusini mwaka 2002—miaka 192 tanzu alipotolewa nchini mwao.

Sarah Baartman aligeuzwa mnyama kwa sababu tu alikuwa na umbo kubwa la makalio makubwa ya asili. Leo hii, dada zetu wanacheza kamari na maisha yao mitaani wakitumia mamilioni kufanya upasuaji hatari wa makalio (BBL) ili wapate umbo lile lile ambalo Sarah alilipia gharama ya utu wake.
 

Attachments

  • _87523034_376392001.jpg.webp
    _87523034_376392001.jpg.webp
    93.1 KB · Views: 18
Wazungu walichoifanyia afrika ni ukatili wa kutisha ila ndio hivo hatuna namna ya kuwafanya
 
Najua stori yote ya Sara.

Najua jinsi alivyochanganywa majina.

Najua magonjwa aliyoumwa.

Ila kila nikikuta sehemu anazungumziwa lazima niangalie picha zake tena.
Sababu za kuangalia picha zake ni zipi, mkuu?
 
Wazungu walichoifanyia afrika ni ukatili wa kutisha ila ndio hivo hatuna namna ya kuwafanya
Namna ipo mkuu tatizo tumejikatia tamaa alafu tunawatukuza sana turudi kwenye asili zetu tuu.
 
Back
Top Bottom