Mfahamu Stan Van De Buys aliyejifunga hat-trick ndani ya mechi moja

Mfahamu Stan Van De Buys aliyejifunga hat-trick ndani ya mechi moja

Mchezaji wa kimataifa kutokea Ubelgiji aliyepata umaarufu mkubwa kwa kujifunga magoli matatu (hat-trick) ndani ya mechi moja
Stan van de buys aliyekuwa akiichezea timu ya Germinal ekeren.

mnamo msimu wa 1994 -1995 kwenye ligi ya Ubelgiji (The Belgian Jupiler league), timu ya Anderlecht ilijinyakulia ubingwa mnono wa magoli 3-2 dhidi ya Germinal ekeren hali ya kuwa magoli yote yalitokana na kujifunga kwa staa Van de buys. Tumfananishe na mchezaji gani hapa Bongo?

Yule wa kuitwa Ninja, maeneo ya Otopoloni
 
Huyo aliweka rekodi...! Ila kuna uzi mmoja hapa kuna jamaa alimaliza dk 90 uwanjani bila kugusa mpira....! Kuna watu wana rekodi we acha
Yaani ile story huwa naiona kama fiction tu, DK 90 bila kugusa mpira kocha anakuangalia tu au hiyo mechi haikuwa na sub?
 
Huyo aliweka rekodi...! Ila kuna uzi mmoja hapa kuna jamaa alimaliza dk 90 uwanjani bila kugusa mpira....! Kuna watu wana rekodi we acha
Nilipoona ona huu Uzi nkawa nawaza kituko kingine cha mpira ambacho niliwah kukisoma hapa jf,umenikumbusha..........ila huwa nashangaa iliwezekanaje dk 90 bila kugusa
 
Pierre ISSA wa south Africa
World cup 98 France alijifunga mechi mbili..
Halafu akapata timu huko huko ufaransa ikamsajili
 
Back
Top Bottom