Mfahamu T.O Kihombo 2006 aliyepata Degree yake ya Kwanza baada ya Miaka 11

Yaani huo ndio ukweli na uhalisia! Kuna mambo mengine hata kuyaeleza humu yanatia ukakasi, ni bora kukaa kimya na kufanya kile unachoona kinafaa kwa maisha ya baadae. Lakini ukweli utabaki kuwa ukweli, kuwa TANZANIA sio sehemu salama kwa wanafunzi wa shule za msingi na shule za sekondari.
 
Ngoja niwape siri nyingine, huwa wanasema hivi:

"TANZANIA inafananishwa na binti kigoli [ndio asili ya ule usemi unaosema TANZANIA is a virgin land ]. Kwa hiyo unaweza kuchezea sehemu zote za mwili wa binti kigoli, lakini hauruhusiwi kuchezea matiti ya binti kigoli kwani hadhi itashuka, matiti yakitelemka."

Sasa matiti ni nini? Matiti ni Baraza la Mitihani la TANZANIA [ NECTA ], yaani hauruhusiwi kugusa au kujadili matokeo ya mitihani ya wanafunzi wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita.

Matokeo yatakayoamuliwa na kutangazwa na NECTA, hakuna mtu au taasisi yoyote itakayoweza kupindua matokeo ya wanafunzi isipokuwa idhini ya Rais.

Ndio maana hata hawa wanasiasa huwa hawajadili bungeni matokeo ya wanafunzi yaliyokwisha kutangazwa au kutotangazwa na Baraza la Mitihani, yaani NECTA.

Hiyo ndio TANZANIA!!.
 
Kuna mwaka 2011 kama sikosei, mbona yalijadiliwa bungeni nakumbuka mpka yalitolewa upya matokeo,
Yalikuwa ni ya kidato cha nne, kuna watu yalibadilika na kunawatu yalibaki vile vile,
Sijui sheria gani umeitumia kusema eti matokeo ya necta hayajadiliwi bungeni?
 
Jaribu kufuatilia kwa makini, utagundua ninachokueleza hapa. Hata namna ya kuwasilisha hoja bungeni, kuna mambo hayawezi kujadiliwa bila ya idhini ya Rais kupitia Waziri mkuu na Baraza la Wawaziri. Ijapokuwa Bunge ni mhimili unaojitegemea.

Mfano halisi ni mikataba ya madini au mikataba ya mafuta na gesi! Pamoja na kelele zote zinazopigwa bungeni, ulishawahi kuona Mkataba wa Madini au Mkataba wa Mafuta na Gesi?

Sasa inawezekana kuwa matokeo ya kidato cha nne, mwaka 2011 yalijadiliwa kwa msaada wa Wizara ya Elimu yenyewe kupitia idhini ya Rais.

Na kuna kipindi au miaka fulani wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa huwa wanakaribishwa na kupongezwa bungeni, na miaka mingine huwa hakuna. Nikimaanisha sio miaka yote wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa wamekuwa wakipongezwa na Bunge.

Sasa anayefanya hivi, huwa sio Bunge ni maamuzi ya NECTA kupitia Wizara ya Elimu. Waziri wa Elimu ndio anayehusika na shughuli zote zinazohusu Elimu pale Bungeni. Na sio tofauti!
 
Ulikuwa unataka unione Forbes [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ila hapo ulipotolea mfano wa binti wa St francis kuuza juice kwa Forest Mbeya, kuna dots naanza kuziconnect,
Inanikanganya Sana kuna dada namjua kasoma o level na advance private na kote huko kapata div 1, sijui matokeo yake ya mzumbe yalikuwaje ila kifupi ni kwamba amekanyaga pale sekretarieti ya ajira miaka nenda rudi hapati ajira mpaka sasa yupo sehemu lakini naona kama she doesnt deserve,

Hivi hili swala technically linakuaje mkuu Mandela?
 
Kihombo Elias aliacha tulikula Wali wiki nzima aisee miaka hiyo. Headmaster alitoa bonus kwamba Vijana mtakula wali wiki nzima kwa kitendo cha kupata T.O.
Naaam, nami nilikuwepo Form V 2006....
 
Bruh hapo umegusa wasongo wengi sana haijalishi walipotoka...kwa kifupi sahv ajira ni ngumu sana degree zilizopo mtaani ni maelfu me maelfu na hali yazidi kua mbaya siku hadi siku
 
Embu nieleweshe hapa kwanini wanafanya hivi... ukiweka hiyo makala tafadhali ni tag
 
Acha uongo.
 
Hayo ndio madhaifu ya NECTA tunayosema hapa, tatizo halipo kwa huyo muhitimu au Chuo Kikuu [ Mzumbe ] alichosoma.

Tatizo lipo Baraza la Mitihani yaani NECTA na kituo chake cha mtihani yaani shule.

Kwa sababu, matokeo ya Chuo Kikuu hayafanyi muhitimu kuajiriwa au kutoajiriwa.

Bali matokeo ya shule ya msingi na shule ya sekondari ndio yanayotoa taswira kamili ya muhitimu kuajiriwa au kutoajiriwa.

Matokeo yanayosoma kwenye vyeti yakiwa tofauti na matokeo yanayosoma kwenye vitabu vya wahitimu, ajira inakuwa ni ngumu kupata au kutoajiriwa kabisa.

Kwa sababu inaonekana kuna udanganyifu, hayo ndio madhara ya " REPRESSION AND FALSIFICATION OF ACADEMIC RESULTS".

Na sio wahitimu wa shahada tu, hata ukiwa na Masters, PhD au Profesa. Bado matokeo ya sekondari yanakuwa na nguvu ya kufanya kupata ajira au kutopata ajira kabisa.

Kwa mfano halisi, miaka ya nyuma sio zamani sana ni hivi karibuni tu! Kuna mwanasiasa wa TANZANIA [ PhD ] alienda nchini Kanada na kuanza kuuza duka [ Supermarket ] huko ughaibuni. Huyu ni PhD kabisa!

Na asingelikuwa Rais kumteua kuwa afisa mwandamizi wa ubalozi wa TANZANIA huko ughaibuni angelikuwa anauza duka mpaka leo, ingali ajira zipo.

Sasa ukiangalia "ACADEMIC BACKGROUND" ya huyu PhD, kwanza hajawahi kuajiriwa popote zaidi ya kufanya kazi ya kanisa na baadae alifanikiwa kujiunga na siasa mpaka akawa mgombea urais mwaka 2010.

Bado matokeo ya huyu PhD alipokuwa sekondari yanaonesha kuna kasoro, kama unavyofahamu shule za sekondari za seminari. Huwa kuna "REPRESSION OF ACADEMIC RESULTS" kubwa sana. Hayo ndio madhara yake.

Kwa hiyo kwa upande wa TANZANIA, Baraza la Mitihani yaani NECTA ndio injini ya Elimu ya TANZANIA. Hapo ndio ipo hatima ya muhitimu yoyote aliyesoma TANZANIA.
 
Bruh hapo umegusa wasongo wengi sana haijalishi walipotoka...kwa kifupi sahv ajira ni ngumu sana degree zilizopo mtaani ni maelfu me maelfu na hali yazidi kua mbaya siku hadi siku
Tatizo sio kuwa na idadi nyingi za wahitimu wa shahada. Tatizo ni ubora wa wahitimu wa shahada husika.

We do need qualitative number of graduate degrees, and not quantitative number of graduate degrees.

Kuna vyuo vikuu vinatoa shahada kwa wanafunzi wasiokuwa hata na vigezo vya kusoma shahada.

Na mifano iko mingi kabisa, kuna vyuo vikuu vina "PRE ENTRY COURSES" kabla ya kujiunga na masomo ya shahada. Lakini sote tunafahamu kuwa "PRE ENTRY COURSES" hazipo kwenye mitaala ya kufundishia ya TANZANIA.

Kwa upande wa TANZANIA, baada ya masomo ya sekondari huwa kuna astashahada, stashahada, shahada, uzamiri nakadhalika.

Hii "PRE ENTRY COURSES" ni biashara, matokeo yake wanapatikana wahitimu wasiokuwa hata na sifa ya kusoma shahada.

Kuna wanafunzi walisoma michepuo ya EGM na PCB lakini walienda kuchukua fani za uhandisi ijapokuwa sote tunafahamu kuwa hawa wanafunzi wa michepuo hii hawana vigezo vya kusoma fani za uhandisi.

Sasa muajiri gani ataajiri muhandisi aliyesoma EGM au PCB?

Kama ukipata ajira itakuwa ni bahati sana na pengine unaweza hata usiajiriwe kabisa!

Sasa hapa taasisi inayohusika ni TCU [ Tanzania Commission of Universities ] na sio NECTA. Hii TCU inabidi itoe semina elekezi kwa wahitimu wa sekondari au ikibidi vyuo vikuu viruhusiwe kudahili wanafunzi kama zamani ili kuondoa kasoro zinazofanyika sasa hivi.
 
Unaposema mimi niache uongo! Inabidi wewe utueleze ukweli ni upi! Hapa tupo Jukwaa la Elimu na mimi ndio mdau husika [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mdau husika?
Wengine waliomo humu siyo wadau husika?
Unapotosha umma wa wana-jamiiforums.
 
PCM wengi ni wahasibu pia na wanasoma kwenye reputable universities kama udsm mzumbe nk what do you expect?mtu hajawah hata kusoma book-Keeping/commerce /economics lakini kisa tu kafaulu hesabu anaenda kusoma bachelor of commerce in accounting nk
 
PCM wengi ni wahasibu pia na wanasoma kwenye reputable universities kama udsm mzumbe nk what do you expect?mtu hajawah hata kusoma book-Keeping/commerce /economics lakini kisa tu kafaulu hesabu anaenda kusoma bachelor of commerce in accounting nk
Nadhani sasa hivi tunaanza kuelewena. Haya ndio madhaifu ninayosema mimi!

Halafu huko UDSM kuna nini? Afadhali hata Mzumbe!

Mimi ni muhitimu wa UDOM! Na hao wanafunzi wa UDSM ndio niliowaburuza tukiwa sekondari!

Hapa ni NYUMBANI! Hata Nyangema anafahamu hili πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…