Ila hapo ulipotolea mfano wa binti wa St francis kuuza juice kwa Forest Mbeya, kuna dots naanza kuziconnect,
Inanikanganya Sana kuna dada namjua kasoma o level na advance private na kote huko kapata div 1, sijui matokeo yake ya mzumbe yalikuwaje ila kifupi ni kwamba amekanyaga pale sekretarieti ya ajira miaka nenda rudi hapati ajira mpaka sasa yupo sehemu lakini naona kama she doesnt deserve,
Hivi hili swala technically linakuaje mkuu Mandela?
Hayo ndio madhaifu ya NECTA tunayosema hapa, tatizo halipo kwa huyo muhitimu au Chuo Kikuu [ Mzumbe ] alichosoma.
Tatizo lipo Baraza la Mitihani yaani NECTA na kituo chake cha mtihani yaani shule.
Kwa sababu, matokeo ya Chuo Kikuu hayafanyi muhitimu kuajiriwa au kutoajiriwa.
Bali matokeo ya shule ya msingi na shule ya sekondari ndio yanayotoa taswira kamili ya muhitimu kuajiriwa au kutoajiriwa.
Matokeo yanayosoma kwenye vyeti yakiwa tofauti na matokeo yanayosoma kwenye vitabu vya wahitimu, ajira inakuwa ni ngumu kupata au kutoajiriwa kabisa.
Kwa sababu inaonekana kuna udanganyifu, hayo ndio madhara ya " REPRESSION AND FALSIFICATION OF ACADEMIC RESULTS".
Na sio wahitimu wa shahada tu, hata ukiwa na Masters, PhD au Profesa. Bado matokeo ya sekondari yanakuwa na nguvu ya kufanya kupata ajira au kutopata ajira kabisa.
Kwa mfano halisi, miaka ya nyuma sio zamani sana ni hivi karibuni tu! Kuna mwanasiasa wa TANZANIA [ PhD ] alienda nchini Kanada na kuanza kuuza duka [ Supermarket ] huko ughaibuni. Huyu ni PhD kabisa!
Na asingelikuwa Rais kumteua kuwa afisa mwandamizi wa ubalozi wa TANZANIA huko ughaibuni angelikuwa anauza duka mpaka leo, ingali ajira zipo.
Sasa ukiangalia "ACADEMIC BACKGROUND" ya huyu PhD, kwanza hajawahi kuajiriwa popote zaidi ya kufanya kazi ya kanisa na baadae alifanikiwa kujiunga na siasa mpaka akawa mgombea urais mwaka 2010.
Bado matokeo ya huyu PhD alipokuwa sekondari yanaonesha kuna kasoro, kama unavyofahamu shule za sekondari za seminari. Huwa kuna "REPRESSION OF ACADEMIC RESULTS" kubwa sana. Hayo ndio madhara yake.
Kwa hiyo kwa upande wa TANZANIA, Baraza la Mitihani yaani NECTA ndio injini ya Elimu ya TANZANIA. Hapo ndio ipo hatima ya muhitimu yoyote aliyesoma TANZANIA.