Mfahamu T.O Kihombo 2006 aliyepata Degree yake ya Kwanza baada ya Miaka 11

Duuuuuh hii hatareeeh sana lol.
 
Duuuuuh hii hatareeeh sana lol.
Hii ndio SIASA inayofanywa na SERIKALI inayoongozwa na CHAMA CHA MAPINDUZI yaani CCM, kwa upande wa SEKTA YA ELIMU.

Na sio SIRI, ubora wa ELIMU YA TANZANIA 🇹🇿 umeshuka sana! Umeshuka kwa sababu gani? ELIMU YA TANZANIA 🇹🇿 imeshuka kwa sababu ya kuruhusu SIASA kwenye SEKTA YA ELIMU.

Hivi unafahamu kuwa, tangu TANZANIA 🇹🇿 imepata UHURU kutoka kwa MUINGEREZA, hakuna JINSIA YA KIKE iliyowahi kuongoza MTIHANI WA TAIFA!

Ndio! Hakuna JINSIA YA KIKE iliyowahi kuongoza MTIHANI WA TAIFA.

Kwa kutumia VITABU VYA WAHITIMU, vinavyoonesha watahiniwa wote waliofanya MITIHANI YA TAIFA kuanzia mtihani wa taifa wa darasa la nne! Mtihani wa taifa wa darasa la saba! Mtihani wa taifa wa kidato cha pili! Mtihani wa taifa wa kidato cha nne na mtihani wa taifa wa kidato cha sita hakuna JINSIA YA KIKE iliyowahi kuongoza MTIHANI WA TAIFA.

Hawa wote JINSIA YA KIKE wanaotangazwa kuwa wamefanya vizuri kitaifa huwa wanatangazwa kimakosa. Na hii ndio SIASA! Narudia tena, hii ndio SIASA!

Ndio maana hawa VIONGOZI WA UPINZANI tunawashangaa! Tena tunawashangaa sana! Kwa sababu kabla ya kudai KATIBA MPYA, kuna vitu ambavyo hawa WANASIASA WA UPINZANI walitakiwa KUIUMBUA na KUIKEMEA serikali ya TANZANIA 🇹🇿 dhidi ya matendo yasiyokubalika yanayofanywa kwenye sekta mbali mbali za SERIKALI ikiwemo hii SEKTA YA ELIMU.

Sasa hawa VIONGOZI WA UPINZANI unakuta wameandaa mkutano wa hadhara kwa ajili ya kutaja ORODHA YA MAFISADI. Hao MAFISADI wanawafahamu wao tu, sisi wengine wala hatuwafahamu 😂😂

Lakini hawa hawa VIONGOZI WA UPINZANI wanashindwa kuandaa mkutano unaohusu ELIMU na waandishi wa habari kwa nia ya kutaja orodha ya WANAFUNZI BORA 😂😂

Sasa ni nani ambaye ana nafuu kati ya CHAMA CHA MAPINDUZI yaani CCM na VIONGOZI WA UPINZANI 😂😂?

Ni bora CHAMA CHA MAPINDUZI yaani CCM, kwa sababu hawa VIONGOZI WA UPINZANI tulionao TANZANIA 🇹🇿, wao wanaangalia MASILAHI yao kwanza! Kama hakuna MASILAHI, hawa VIONGOZI WA UPINZANI hutawasikia wakizungumza wala kujadili hoja ambayo haiwanufaishi.

Kwahiyo JUKUMU lililopo mezani, kama MZAZI au MLEZI unatakiwa kujipanga na kukabiliana na madhaifu ya SERIKALI YA TANZANIA 🇹🇿 yaliyopo kwenye SEKTA YA ELIMU.
 
Kheeeeh haya makubwa sasa, wee umejuaje haya yote?
 
Kheeeeh haya makubwa sasa, wee umejuaje haya yote?
Sasa kwani ni UONGO? Hawa VIONGOZI WA UPINZANI kuna vitu walitakiwa kuvidai kabla ya kuanza kudai KATIBA MPYA!

Kwa sababu KATIBA MPYA inajumuisha mambo mengi. Sio suala la UCHAGUZI MKUU tu!

Unaweza kupata KATIBA MPYA lakini bado ukashindwa kwenye UCHAGUZI MKUU. Matokeo yake, tunaweza kuanza kurekebisha baadhi ya vipengele kama ilivyo kwa taifa la KENYA 🇰🇪.

Sasa ni nini ambacho hawa VIONGOZI WA UPINZANI wanatakiwa kufanya kwa wakati huu uliopo?

Jambo la msingi ni kutanguliza MASILAHI YA TAIFA kwanza, mengine baadae. Ninaposema MASILAHI YA TAIFA sio UZALENDO UCHWARA [ 😁😁 ].

Ninamaanisha hivi kila taasisi na kila sekta iliyo chini ya SERIKALI YA TANZANIA 🇹🇿 waipitie na kufahamu mapungufu yote ya kisheria, ili wanapokuja kwa WANANCHI waje na HITIMISHO la kudai KATIBA MPYA.

Hii ikiwa ni tayari wameshaona mapungufu yote yanayofanywa na SERIKALI iliyopo madarakani.

Sasa, kwa maelezo yote hapo juu, hiki CHAMA CHA WALIMU TANZANIA yaani CWT [ Tanzania Teachers Union ] majukumu yake ni yapi kwenye SEKTA YA ELIMU? Ina maana hiki chama cha CWT kipo kwa ajili ya kusimamia MASILAHI ya walimu tu?

Na MASILAHI ya wanafunzi ni nani ayesimamia? Ni nani anaye hakikisha kuwa wanafunzi wametendewa haki kwa kupata kile walichokijibu kwenye MITIHANI yao ya TAIFA?

Sasa haya mambo ndio waliyotakiwa kuyajadili VIONGOZI WA UPINZANI, kwa kupitia kila SEKTA, halafu ndio waje na HITIMISHO la kupata KATIBA MPYA.
 
Mkuu Angalia data zako vizuri, km kumbukumbu zangu zitakuwa vizuri mwaka kidato cha 6 mwaka 2012 aliongoza msichana kutoka feza girls

Mwaka 2015 kidato cha 4 aliongoza msichana

Mwaka juzi kidato cha 6 aliongoza msichana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasema hivi - hiyo ndio SIASA! Narudia tena hiyo ndio SIASA kwenye SEKTA YA ELIMU inayofanywa na SERIKALI inayoongozwa na CHAMA CHA MAPINDUZI yaani CCM.

Kwa kutumia VITABU VYA WAHITIMU vinavyoonesha watahiniwa wote waliofanya MITIHANI YA TAIFA na waliopangwa kwa UFAULU kuanzia mwanafunzi wa kwanza mpaka mwanafunzi wa mwisho kitaifa, vinaonesha hakuna JINSIA YA KIKE wala MWANAFUNZI KUTOKA SHULE BINAFSI aliyewahi kuongoza kwenye MITIHANI YA TAIFA.

MITIHANI YA TAIFA inajumuisha kuanzia mitihani ya darasa la nne! Mitihani ya darasa la saba! Mitihani ya kidato cha pili! Mitihani ya kidato cha nne na mitihani ya kidato cha sita.

Sasa basi, kwa UDANGANYIFU unaoendelea kufanyika pale BARAZA LA MITIHANI yaani NECTA [ NECTA | Home ] unasababisha UBORA WA ELIMU kushuka, kwa sababu wanafunzi wanapewa vyeti walivyoandikiwa MATOKEO YA UFAULU ambayo hawakustahili.

Na hali hii inasababisha hata ubora wa VYUO VIKUU vya TANZANIA 🇹🇿 kushuka, kutokana na kuchukua wahitimu wa SHULE ZA SEKONDARI wasiokuwa na MATOKEO HALISI.

Na mifano ipo mingi tu! Tukiwauliza hawa NECTA | Home zipo wapi taarifa za mwanafunzi aliyeongoza kidato cha nne mwaka 2007? Tukiwauliza tena, zipo wapi taarifa za mwanafunzi aliyeongoza kidato cha sita mwaka 2010? Tukiwauliza tena na tena, zipo wapi taarifa za mwanafunzi aliyeongoza kidato cha sita mwaka 2015? Majibu yake utakayoyapata ni tofauti kabisa na MATOKEO yaliyoandikwa kwenye VYETI VYA KUHITIMU vya hawa wanafunzi.

Hii ni SAMPULI ndogo tu, tena ya wale wanafunzi waliongoza kitaifa. Bado kuna maelfu ya wanafunzi wanateketea kwa MFUMO MBOVU WA ELIMU YA TANZANIA 🇹🇿.

Sasa hapa ni nani wa kulaumiwa? Ni nani anayestahili kuchukuliwa hatua? Je, ni NECTA | Home au Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia au Home | PO-RALG ? Na nafasi ya CHAMA CHA WALIMU TANZANIA 🇹🇿 yaani Tanzania Teachers Union ni ipi? Kwa jinsi inavyoonekana hizi taasisi zote za ELIMU zinafahamu zinachokifanya yaani hizi taasisi zote zina malengo yanayofanana.

Na hii ndio ilikuwa turufu kwa VIONGOZI WA UPINZANI kuonesha uwezo wao wa KISIASA kama ikitokea watapewa jukumu la kuongoza nchi.

Lakini sasa hivi hawa VIONGOZI WA UPINZANI wamekuwa kama WATOTO WADOGO 😂😂😂

Wimbo ulioshika chati baada ya UFISADI ni KATIBA MPYA! KATIBA MPYA! KATIBA MPYA! KATIBA MPYA 😂😂😂

Yaani hawafahamu kabisa kutumia madhaifu ya SERIKALI kama fursa ya wao kujiimalisha kisiasa.
 
Na kuwa na subira hadi mwaka 2022, yaani mwaka ujao pale ambapo hii taasisi ya kimataifa ya UNESCO itakapotoa orodha ya nchi kwa viwango vya UBORA WA ELIMU,

Nabashiri, kwa nchi za AFRIKA YA MASHARIKI yaani KENYA 🇰🇪, UGANDA 🇺🇬, RWANDA 🇷🇼, BURUNDI 🇧🇮 na TANZANIA 🇹🇿.

Nchi ya kwanza kwa UBORA WA ELIMU kwa upande wa AFRIKA YA MASHARIKI itakuwa ni KENYA 🇰🇪, ikufuatiwa na UGANDA 🇺🇬, RWANDA 🇷🇼 na nchi zitakazochuana zitakuwa ni BURUNDI 🇧🇮 na TANZANIA 🇹🇿.
 
Hii ndio SIASA inayofanywa na SERIKALI inayoongozwa na CHAMA CHA MAPINDUZI yaani CCM.

Na huu ni mkakati wa SERIKALI inayoongozwa na CHAMA CHA MAPINDUZI yaani CCM.

Sasa hivi kunaonekana kama hakuna ajira kabisa, lakini kuna mkakati wa kuwachukua wale wanafunzi waliongoza kihalali na kuwapatia ajira kulingana na taaluma zao walizosomea.

Hawa wanafunzi waliosoma shule za St Marian, St Francis sijui Feza wataendelea kuisoma namba 😂😂

Mimi binafsi, nilivyorudi TANZANIA 🇹🇿 nilienda moja kwa moja kuripoti WIZARA YA MAMBO YA NDANI, kwa sababu huko nilipokuwa walisema mimi ni mtumishi wa SERIKALI YA TANZANIA 🇹🇿 na ninatakiwa kurudi TANZANIA 🇹🇿.

Hivyo nilivyofika pale HQ wakaniambia nikaripoti kwa DAS ili nipangiwe kazi za HALMASHAURI kwa upande wa maji 😂😂

Na mimi kwa jinsi nilivyo, Aah! Nilienda mara moja tu kuripoti OFISI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA, kipindi hicho alikuwa ni Mama Zainab Telack. Na sijaenda tena!!

Kwa sababu hiyo ndio SIASA wanayoifanya CHAMA CHA MAPINDUZI yaani CCM kwa upande wa SEKTA YA ELIMU - hawa watu ni MASHETANI WEUSI.

Na hata hawa VIONGOZI WA UPINZANI huwa wana papasa tu, ile SIASA yenyewe huwa hawaifanyi.
 
Itakuwa SoMo la Gs alipata 38/100
Na ukitaka kufahamu kuwa tatizo la ajira limetengenezwa na SERIKALI yenyewe.

SERIKALI yenyewe ndio inawashauri SEKTA binafsi kutuma taarifa za wanao omba ajira kwenda TAMISEMI ili kuhakiki vyeti.

SERIKALI hiyo hiyo ndio inaleta majibu tofauti na yale yaliyoandikwa kwenye vyeti vya wanao omba ajira.

Sasa swali linakuja, haya matokeo ya kwenye vyeti vya wanao omba ajira walikuwa wanayotoa wapi kipindi hawa walipokuwa wanafunzi 😂😂

Maana hali ni tofauti kabisa! Unakuta mtu ana DIVISION ONE kwenye cheti halafu TAMISEMI inaleta ana DIVISION FOUR!

Au unakuta mtu ana DIVISION THREE kwenye cheti halafu TAMISEMI inaleta ana DIVISION ONE!

Yaani kuna sintofahamu kubwa sana inayoendelea kwa WAHITIMU wa TANZANIA ndio maana WAHITIMU wengi wanakosa ajira angali ajira zipo.
 
Nyie huyo Charles Mandela amekuja from future au past through time travel

Anaishi dunia ya kwake kabisa.

Yawezekana pia Ni bipolar[emoji15]
 
Nyie huyo Charles Mandela amekuja from future au past through time travel

Anaishi dunia ya kwake kabisa.

Yawezekana pia Ni bipolar
Hapana! Bado muda upo! Sote tunaishi dunia hii hii, sema tunatofautiana mazingira ila kuna baadhi ya vitu tunashea. Kama HEWA nini, you know 😂😂
 
Maelezo mengi afu ujinga
 

umeandika nini sasa hapo mkuu
E
History ya ELIAS KIHOMBO inataka kufanana na ya WILLIUM JAMES SIDIS
Tupe hii
 
Shida ya elimu ya tz mwl ni anayepata ufaulu mdogo ,mie pia ni kati ya watu waliofaulu vizur sanaa na nilipenda kuwa mwl lkn dah nilisoma mambo mengine

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Imepita miaka takribani miaka 17 sasa, tangia Tanzania ilipopata kumshuhudia mwanafunzi alieshindikana katika masuala ya Elimu hapa namzungumzia,Tanzania One (2006) Elias Kihombo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2006 akitokea shule ya sekondari Tosamaganga wengi wanapenda kuiita Tosa Boy's

Mwaka 2006, Necta ilimtangaza mwanafunzi Elias Kihombo kutoka Tosamaganga Secondary School kuwa ndo kipanga wa mwaka huo akiwapita wanafunzi wenye akili zaidi waliovuma toka shule kongwe na special schools kama Kibaha, Ilboru, Mzumbe, Kilakala, Tabora Boys etc ukweli ni kwamba Elias Kihombo hakuwa maarufu kwa kipindi hiko na wengi walisikia tu story zake haswa kwa Wanafunzi wa Mzumbe Boys ambao Mara nyingi walipata kumuona katika mazingira yao.

Kumbuka kwamba Elias Kihombo hakupewa Priority kubwa sana ya kuwa T.O wa Advance Level kutokana pia na matokeo yake ya Kidato cha Nne (4) kuonekana kuwa ya kawaida sana, Kihombo alifanikiwa kupata Division One (1.14) akiwa na Physics-A Chemisrty-A Biology na Mathematics-B, Ndipo mwaka huo 2003 alipata kuchaguliwa Tanga Technical school iliyopo mkoa wa Tanga (tetesi), lakini baadae aliamua kurudi tena katika shule yake ya zamani yaani Tosamaganga Secondary kuendelea na masomo yake ya Advance Level. Alimaliza hapo hapo akifanikiwa kuwa mwanafunzi wa kwanza toka Tosamaganga kwa Advance Level kuwa mwanafunzi bora kitaifa, Alifanikiwa kupata maksi za juu sana na kupata Division One (1.3)

Physics-A
Chemistry-A
Advanced Mathematics-A

October 2006 Alichaguliwa kujiunga na University of Dar Es Salaam (UDSM) akiwa kama T.O kusoma Bachelor of Science In Telecommunication Engineering (4years) na tetesi zinasema alifanikiwa kupata ufadhili wa masomo yake chini ya kampuni ya Airtel.

Siku zilienda na alikuwa karibu kumaliza Elimu yake ya chuo kikuu, huku akipata madili mengi ya kufundisha Tuition maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam na shule nyingi za sekondari ndani ya Tanzania, hasa shule za Advance.

Lakini baada ya Miaka 4 kupita ikiwa miezi michache tu imebaki ya kumaliza chuo, Tanzania One Kihombo alidisco chuo na hivyo kumfanya asifanikiwe kupata degree yake ya kwanza mwaka huo 2010, lakini wengi wanasema hakupaswa kudisco chuo lakini ndivyo ambavyo Hatima yake ilipoishia hapo (tetesi )

Moja kati ya maneno ambayo wengi wanamnukuu aliyopata kuyasema ndani ya Miaka hiyo, alisema "Duniani walionipita kwa akili ni watu wawili tu wa kwanza Mola, wa pili ni Mzungu" hapa ndipo hatima yake inavyosemekana ikafungwa na wakuu wake lakini wengine wanasema vingine.

Elias hakutaka kwenda chuo chochote kile na ndani ya Miaka hiyo mitatu baada ya kudisco chuo, yaani 2011, 2012 na 2013 alikuwa anazunguka shule mbalimbali za sekondari Tanzania kupiga mapindi ya Physics na Chemistry na kwelii huyu jamaa alikuwa ni Invisible katika masomo hayo mawili, Japo Pure Mathematics alikuwa hafundishi kabisa kwasababu alikuwa anasema "Siwezi kufundisha Somo rahisi duniani kama Pure Mathematics, Mimi nafundisha Physics na Chemistry tu"

Ndipo baada ya Miaka mitatu kupita (3) T.O aliyetukuka zaidi katika vinywa vingi vya wanafunzi wa Tanzania, kutokana na ufundishaji wake na kuwaita wanafunzi wake Nyumbu na kuwa na Jeuri zaidi ya Akili zaidi ya watu wengine, alifanikiwa kurudi tena ndani ya University of Dar Es Salaam safari hii akiwa ameamua na amezamilia kuchagua kozi nyingine Mpya kabisa iliyoanzishwa mwaka huo 2013 hapohapo Udsm iliyoitwa (Bachelor of Science In Petroleum Engineering). Hii kozi ilikuwa inachukua wanafunzi 20 pekee Tanzania nzima tena wale waliosoma PCM tu (Physics, Chemistry na Advanced Mathematics) na waliopata Marks za juu kabisaa.

Baada ya Miaka 4 kupita, ndipo July 2017, T.O Elias Kihombo alifanikiwa kumaliza Degree yake ya kwanza (Bachelor of Science In Petroleum Engineering) na mnamo November 2017 Elias Kihombo alifanikiwa kutunukiwa Degree yake ya kwanza akiwa ndani ya University of Dar Es salaam baada ya Miaka 11 kupita.

Hapa imepita Miaka mingi tangia, 2006 Engineer Elias Kihombo alivyotangazwa kuwa Tanzania One lakini ilimchukua Miaka mingine 11 mpaka kutunukiwa Degree yake ya kwanza. Huyu ndiye The Best Of The Best, Eng Elias Kihombo Mwanafunzi aliyepata kutokea Tanzania kuwa na uwezo mkubwa darasani. Nlsikia jinsi ambayo eng elias alikuwa na kipaji cha kufundisha kuanzia asubuhi mpk jioni na kusitokee hata swali moja liliomtolea nje .siku ambayo alisolve maswali kuanzia saa moja hadi saa nne hakuna swali lililo msumbua saa tano hadi saa nane hakuna swali lililo msumbua saa tisa hadi saa kum na mbili hakukua na swali lililo msumbua tuliendelea na mwendo huo kwa muda wa wiki moja . Itabaki historia ktk maisha ya wanafunzi na elimu ya Tanzania kwa ujumla.

Lakin leo tunavyozungumza Elias Kihombo hatunaye tena duniani alifariki Mwaka 2020. Inasemekana kifo chake ni kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili. Tunahitaji kuwa Karbu na Mungu wakati wote kwan safari yetu ipo mikononi mwake. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…